Katiba mpya,wananchi na wadau tuangalie maeneo haya kwa kina - Tanzania kwanza

Binafsi naona dhahiri mapendekezo ya katiba mpya ya muungano imedhamiria kuvunja muungano wenyewe! Serikali moja INATOSHA!
 
CCM = ASP + TANU ==> Serikali Mbili.
Ndani ya Serikali 3, Hakuna CCM, Ndani ya Serikali Moja CCM ipo, ila hapa CCM - Bara wanajua Kabisa kuwa Zanzibar (Mtaji wao) Hawatakubali huo Muundo.
Ndo Maana CCM wanahaha kushawishi watu Muungano wa Serikali 2, watafanya kila Hila kushinikza hili, ni Kama Kuku anayekata Roho akijaribu Kupigania Uhai wake wakati Tayari keshalekezwa Kibra na Kisu kikali kishapita Shingoni Mwake.

Sema Noooooooo to Serikali Mbili, Sema Ndio to Serikali Tatu, na ikishindikana Serikali tatu Sema Ndio to Serikali Moja.
Otherwise, Let Zanzibar and CCM go
Full stop
 
serikali iwe moja , rais mmoja, nchi moja, sarafu moja kama mliweza kuunganisha vyama kwann isiwe serikali? km wazenji hawataki basi wasepe zao sisi hatutaki walalamishi na tumechoka na ngonjera zao.
Hizo hoja nyingine mf. majeshi, sera za sarafu naunga mkono hoja.
Mwisho ndio umebadili tabia yako ya matumizi mabaya ya madaraka na kufanya siasa chafu ama bado?
 
Kwa mara ya kwanza umeonge "POINT" na nimekupa "LIKE", kumbe sometimes akili yako inafanya kazi....
 
Kama serikali tatu ni gharama, kwanini serikaliya CCM imeongeza majimbo, wilaya na mikoa? Katika serikali tatu, Zanzibar na Tanganyika zitakuwa na magovernor , Rais na makamu wake ni wa Jamhuri tuu no PM. Delete vyeo vya ukuu wa Mkoa/wilaya.
 
Hata muundo wa serikali tatu vijana nawaomba mliangalie kwa utulivu bila jazba ya kelele za ndugu zetu wa upande mwingine kusema wananyonywa pia ..........................

Well said ila jifunze kutumia Lugha isiyomkwaza mtu.
 


Hata mimi nakubaliana na wewe.

Analysis yake iko very poor kwa mtu mwenye madaraka makubwa sana nchini kupitia chama twawala. Alichofanya hapa ni kuweka vipengere ambavyo anadai vinaweza kuwa na utata ............... kitu ambacho nakubaliana naye kwa kiasi fulani. Lakini kwa cheo chake na elimu yake tunayoambiwa ya First class in Economics hakutakiwa kuishia hapo kama akina Nape wenye elimu za kuungaunga. He could have gone deeper!!

Nasubiri analysis yake ya gharama za serikali tatu!!
 
Haya ndiyo mambo ambayo kwa sasa Watanzania tunatakiwa tuyape uzito katika maongezi yetu ya kila siku.

Tatizo lililopo kwenye hii rasimu ni kunataka kujenga nyumba ya gorofa kwenye msingi wa nyumba za tembe.

Hata tume ya Jaji Warioba haikuwa na choice kutokana na kufungwa mikono na hadidu za rejea na matokeo yake ndiyo haya.

Kwa nini wananchi wasiulizwe kwanza kama wanataka kuendelea na hili 'dudu' Muungano, na kama wengi watakubali basi waseme ni muungano gani wanapenda uwepo ili tume ipate political legitimacy.

Hata waingereza pamoja na kuwa na nguvu kiuchumi na pia katika banking sector, waliona haiwezekani kuwa na muundo wa benki kama huu wa Jaji Warioba.

Kwenye eneo la majeshi halina complement. Huwezi ukawa na majeshi ya aina zaidi ya moja ukategemea hakutakuwa na mitikisiko katika nchi ya demokrasia changa kama Tanzania.

Huu muungano uliopo na unaopendekezwa katika misingi hii ni kaput.
 
Halafu sura yako inatisha! Kweli muuaji ni lazima ufanane na kazi yako. Damu za watu zimetapakaa mikononi mwako.
 

Japo sikupendi kwa jinsi unavyoichukia CDM, kwa hili nakupa hongera. Mara watuite wanyonyaji, nk. Tanganyika kwanza.
 
.. Mkuu umenena SERIKALI MOJA TU, ndiyo inayotufaha kwa sasa.
 
Halafu sura yako inatisha! Kweli muuaji ni lazima ufanane na kazi yako. Damu za watu zimetapakaa mikononi mwako.
Jadiri hoja siyo sura za watu kama huwezi unaweza ukawa mjumbe msomaji wa mabandiko.
 
Hivi ndugu yangu Mwigulu unaona unatenda haki kutetea serikali mbili? Sina imani na mtu yeyote anayesema tubaki hivi hivi Mhe. Kwa upande wa Uchumi ni serikali moja ila mbawaogopa wazenji kwa kukubaliana nao ati serikali mbili!!! Fake Tanganyikans will accept two gvts. Aidha iwe moja au ziwe tatu mbili hapanaaaaaaaaaaaaaaaaa
 

...mkuu uko juu, tunahitaji Tanzania MOJA yenye serikali moja, nchi moja, Taifa moja, bunge moja, na dola moja:
- Rais moja
- Makamu wa rais mmoja
- Waziri Mkuu mmoja
- Baraza la mawaziri moja
- Katiba Moja
- Uwakilishi wa UTAIFA mmoja
- Kila kitu mfumo mzima uwe kwenye kofia moja,KWA SASA NDIYO DAWA pekee.
 
Japo sikupendi kwa jinsi unavyoichukia CDM, kwa hili nakupa hongera. Mara watuite wanyonyaji, nk. Tanganyika kwanza.
Mkuu tuweke vyama pembeni tuangalie maslahi yetu ya muda mrefu kwa faida ya vizazi vijavyo

Kama mmoja anaruhusiwa kudai haki yake kwa nini na sisi tusidai Tanganyika yetu?
 
Reactions: SG8
Leo umeongea point. Nakuunga mkono 100% Tanganyika kwanza...
 
Katika siku ambazo nimeona pumba zimeandikwa leo ndio nimeona!! Nyie vikina ccm sio kama mnauchungu sana na hii nchi!! Nyie lengo lenu ni kulinda kura zenu za kule zenji sasa mtake msitake kama si serikali moja basi hapa ni kwenda kwenye serikali tatu!! Kiukweli kifo cha ccm nakiona kabisa!!!! Inamaana hao mlio wachagua wala swala hilo hawakuliona mpaka mlione wenyewe kama vipi nyie wenyewe ndio mjilahumu!!!! Hatudanganyiki kabisa
 
GOOD OBSERVATION, si wakati muafaka kuwa na majeshi matatu, benk tatu za serikali na serikali tatu
 
Huyu Pimbi, mbona leo kuna vikosi kule Zanzibar na hatujapigana , am hujui kuwa kuna KMKM, na vingine? Kamtoe Ludovick magereza kwanza.

ukiambiwa kwa mfano mama yako ndio pimbi utasemaje
 
mwigulu kaleta mada nzuri acha watu waoneshe maoni yao na muelekeo wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…