Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama serikali tatu ni gharama, kwanini serikaliya CCM imeongeza majimbo, wilaya na mikoa? Katika serikali tatu, Zanzibar na Tanganyika zitakuwa na magovernor , Rais na makamu wake ni wa Jamhuri tuu no PM. Delete vyeo vya ukuu wa Mkoa/wilaya.Other things Remain Constant,
Vijana na watoto wetu ndio tunategemewa kuitumia zaidi katiba mpya. Mabaraza yanaanza, kama wadau nawaomba TUISOME RASIMU, TUTAFAKARI, TUJADILI, TUTOE MAONI KWA KUITANGULIZA TANZANIA MIOYONI MWETU. SIO KULENGA KULIKOMOA KUNDI FULANI AU UPANDE FULANI WA NCHI.
Nawashauri tuyaangalie maeneo kwa kina. Kwa kuanzia tuangalie:
A) Ibara ya 223(1) inasema kutakuwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania litakalokuwa na mamlaka ya kusimamia ulinzi na usalama.... Ibara ya 232(1) inasema bila kuathiri mashariti ya katiba hii, nchi washarika wa muungano wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama .... ktk maeneo yao.
Pili ibara ya 227(1) kutakuwa na Jeshi la Polisi la jamuhuri ya muungano litakuwa na jukumu la ulinzi wa wa watu wao, Ibara ya 232 inaongelea vikosi vya washirika kuhusika na ulinzi wa watu wao Pia 233 (1) kutakuwa na idara ya usalama wa Taifa wa jamuhuri ya muungano ... Ibara 235 inasema bila kuathiri masharti ya katiba hii, nchi washirika wanaweza kuanzisha idara za usalama.
Analysis, swala la usalama ni nyeti muundo huu utategemea tu mazingira na busara ya viongozi. Vinginevyo nirahisi vikosi vya muungano kupigana na vya nchi washirika kufuatia maelekezo ya viongozi wao siku wakitokea sio wataifa.
B) ibara ya 217(1) kutakuwa na benki kuu ya jamhuri ya muungano na majukumu yameainishwa...... ibara ya 218 serikali washirika zitakuwa na BENKI ZAO zakusimamia sera za kifedha na kibenki
Analysis; hakuna namna unaweza kuwa na monetary policy tatu ktk nchi moja ukafikia malengo. Ni kama gari kuwa na sukani tatu na madreva wa tatu at per, the will miss the right direction.
C) ibara ya 1(1), 1(2) na 57(1) zinazungumzia shirikisho, nionavyo mimi ni makosa. Jamhuri ya muungano ni nchi sio shirikisho. Kupata shirikisho ni sharti kwanza nchi washirika tupige kura kama tunataka kujiunga na shirikisho au laa kama tulivyokataa la afrika mashariki.
Hata muundo wa serikali tatu vijana nawaomba mliangalie kwa utulivu bila jazba ya kelele za ndugu zetu wa upande mwingine kusema wananyonywa pia bila kuangalia mungano wa serikali mbili kuwa ni msimamo wa CCM. TANZANIA BARA ITAKUWA NA SERIKALI MBILI YAANI YA BARA NA YA MUUNGANO ambayo haitahusika na maisha ya watanzania bara kupitia mambo yenye mguso wa moja kwa moja. NITAWALETEA SIKU NYINGINE IMPLICATION ZAKE KIUCHUMI KWA TAKWIMU NA JINSI KODI ITAKAVYOPANDA KUKIDHI NYONGEZA YA SERIKALI. BE BLESSED
Hata muundo wa serikali tatu vijana nawaomba mliangalie kwa utulivu bila jazba ya kelele za ndugu zetu wa upande mwingine kusema wananyonywa pia ..........................
Hii analysis yako iko verry poor, ukizingatia lengo na madhumuni yako.
Kwanza Mchakato wa kuanzisha Katiba mpya mlikuwa hamuutaki kwa sababu itapunguza ulaji na mapango yenu yote ya kufanya uhalifu pamoja na ufisadi...
Ninauhakika nyinyi mnahofu kubwa sana ya kuwa na katiba mpya yenye vyombo vya sheria, ulinzi, Usalama na Uchaguzi huru kwani kufanya hivyo ninauhakika mtashindwa kupendelewa na hatimaye kufikishwa mahakamani na pengine kufungwa kwa sababu ya uovu mnaoufanya.
Wanganyika wanachotaka ni Tanganyika yao na Zanzibar wanachotaka no Zanzibar yao yenye mamlaka kamili nyinyi manataka serikali mbili ambayo imekuwepo tangu 1964 mpaka leo na mnataka kuendelea nayo kivipi???
Nyinyi hamna nia njema na Katiba mpya kwa sababu hamna uchungu na waTZ mko tu kwa ajili maslahi yenu tu na watanzania hawako tayari kudanganyika safari hii.
Mimi ni TANGANYIKA KWANZA mengine baadae.
Lakini kwa jinsi inmavyoonekana Tanzania inaweza kuwa na majeshi ya ulinzi matatu, hapo ndio matatizo yatakapoanzia kwa sababu kila mtu ataiona ana comand upande wake.
Mimi nadhani ni vyema kila nchi ijetegemee kivyake na tubaki marafiki kama kenya na sie . ... Mbona EAST AFRICA ilivunjika?
Mbona Sudan imegawanyika?
Hizi ndoa zenye manung'uniko kila kukicha ndio matokeo yake siku moja unakuta mzazi mmoja kwatilia sumu familia nzima ili wote wakose.
TANGANYIKA KWANZA!
.. Mkuu umenena SERIKALI MOJA TU, ndiyo inayotufaha kwa sasa.Kama unavyosema ni kweli hatuwezi kuwa na monetary policy tatu... Hapa mpango mzima ni Serikali moja tu kama wale wa Zenji hawawezi tunasema let Zanzibar go, sitaki serikali tatu, Gari itakuwa vipi na misikanio mitatu!? Mpango mzima ni Tanzania moja...
Jadiri hoja siyo sura za watu kama huwezi unaweza ukawa mjumbe msomaji wa mabandiko.Halafu sura yako inatisha! Kweli muuaji ni lazima ufanane na kazi yako. Damu za watu zimetapakaa mikononi mwako.
kama Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 Tukapata Tanzania. baada ya miaka50 ya majaribio tulitegemea huu muungano ukomae na kuwa serikali moja, ili tutamke kwa jeuri kuwa kuna nchi moja, Taifa moja, serikali moja, bunge moja, na dola moja. kwa hiyo ifikapo 26/4/2013 tungeizika zanzibar rasmi kama tulivyoizika tanganyika miaka hamsini iliyopita. Kama tutarudi kwenye serikali tatu au kuendelea na serikali mbili, mimi naona hakuna haja ya muungano, hapo ndoa imeshindikana hapo kila mmoja arejee kwa wazazi wake.
Mkuu tuweke vyama pembeni tuangalie maslahi yetu ya muda mrefu kwa faida ya vizazi vijavyoJapo sikupendi kwa jinsi unavyoichukia CDM, kwa hili nakupa hongera. Mara watuite wanyonyaji, nk. Tanganyika kwanza.
Leo umeongea point. Nakuunga mkono 100% Tanganyika kwanza...Mimi ni TANGANYIKA KWANZA mengine baadae.
Lakini kwa jinsi inmavyoonekana Tanzania inaweza kuwa na majeshi ya ulinzi matatu, hapo ndio matatizo yatakapoanzia kwa sababu kila mtu ataiona ana comand upande wake.
Mimi nadhani ni vyema kila nchi ijetegemee kivyake na tubaki marafiki kama kenya na sie . ... Mbona EAST AFRICA ilivunjika?
Mbona Sudan imegawanyika?
Hizi ndoa zenye manung'uniko kila kukicha ndio matokeo yake siku moja unakuta mzazi mmoja kwatilia sumu familia nzima ili wote wakose.
TANGANYIKA KWANZA!
Huyu Pimbi, mbona leo kuna vikosi kule Zanzibar na hatujapigana , am hujui kuwa kuna KMKM, na vingine? Kamtoe Ludovick magereza kwanza.