Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mimi nimekuwa muumini wa katiba mpya tangu enzi na enzi. Kabla hata JF haijazaliwa.
Niliamini hivyo kwa sababu unapobadili mfumo wa kisiasa, basi ni lazima pia ubadili sheria na taratibu zitazotumika kuuongoza huo mfumo mpya.
Hivyo basi, ilipaswa tokea mwanzo, yaani 1992, tuliporudi tena kwenye mfumo wa vyama vingi, kubadili kabisa katiba ili iendane na hayo mazingira mapya.
Hilo halikufanyika. Kilichofanyika ni kubadili badili tu vitu vidogo vya hapa na pale kwenye katiba iliyokuwepo wakati huo, basi.
Tokea 1995, tumeona ni jinsi gani watawala wa CCM wanavyoweza kuikiuka hii katiba tuliyo nayo.
Mifano ipo mingi. Nitaitaja miwili ya hivi karibuni ambayo wengi mtakuwa mnaikumbuka.
Baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alipiga marufuku watu kufanya shughuli za kisiasa kwa kisingizio kwamba ‘siasa sasa zimeshaisha na ni wakati wa kufanya kazi’. Hiyo ni licha ya kwamba shughuli hizo ni haki za kikatiba kwa Mtanzania yeyote yule.
Baada ya Rais Magufuli kufariki, baadhi ya wajuzi na wajuvi wa mambo ya katiba walituambia kwamba Rais Samia alipaswa kulivunja baraza la mawaziri na kuunda serikali mpya.
Hilo halikufanyika. Hivyo maana yake ni kwamba naye aliikiuka katiba.
Sasa nimewaza: kama hii katiba iliyopo inakiukwa wazi wazi namna hii na hamna lolote la maana linalofanyika kupinga ukiukwaji huo, hiyo katiba mpya inahitajika ili iweje?
Mara karibu zote ambapo katiba imeonekana kukiukwa, hakuna cha maana ambacho wananchi tumefanya zaidi ya kujimwambafy humu kwenye mitandao.
Hakuna aliyethubutu kuingia barabarani na kupinga. Hakuna aliyefungua kesi mahakamani. Tumelia lia tu humu mitandaoni.
Sasa hiyo katiba mpya tukiipata, ikikiukwa ndo itatuwezesha kupata ujasiri wa kupinga kukiukwa kwake?
Nimeanza kudhani pengine tatizo letu si katiba mpya pekee. Tatizo letu kubwa ni sisi wenyewe. Tunaachia tu mambo yaende hata kama yapo kinyume na katiba.
A new constitution will not be worth the paper it’s written on if we allow and let the one we have to be breached with impunity!