Katiba Mpya ya nini kama hii tuliyonayo hatuiheshimu?

Katiba Mpya ya nini kama hii tuliyonayo hatuiheshimu?

Kwani kipi kilichotangulia?

Kupigwa marufuku shughuli za kisiasa au hiyo kesi ya Shaibu?
Marufuku ya shughuli za kisiasa. Watu walitambua toka wakati ule kuwa hamna relief itapatikana kutoka Mahakama. Kesi ya Ado ikathibitisha kuwa wangeshitaki ingekuwa sawa na kutupa pesa chooni. Kumbuka wakati huo viongozi wengi wa Chadema walikuwa wameshitakiwa mahakamani. Nadhani wakafanya uamuzi kuweka resourses kwenye kujitetea badala ya kwenye futile kesi ya kikatiba.

Amandla...
 
Ndio hicho hicho, in a round about way. Nilitaka kukuonyesha futility ya kuishitaki serikali ya JMT na viongozi wake kwenye masuala ya kikatiba.

Amandla...
Hakuna futility katika kudai haki aisee!

Ultimately naamini haki hushinda.
 
Mimi nimekuwa muumini wa katiba mpya tangu enzi na enzi. Kabla hata JF haijazaliwa.

Niliamini hivyo kwa sababu unapobadili mfumo wa kisiasa, basi ni lazima pia ubadili sheria na taratibu zitazotumika kuuongoza huo mfumo mpya.

Hivyo basi, ilipaswa tokea mwanzo, yaani 1992, tuliporudi tena kwenye mfumo wa vyama vingi, kubadili kabisa katiba ili iendane na hayo mazingira mapya.

Hilo halikufanyika. Kilichofanyika ni kubadili badili tu vitu vidogo vya hapa na pale kwenye katiba iliyokuwepo wakati huo, basi.

Tokea 1995, tumeona ni jinsi gani watawala wa CCM wanavyoweza kuikiuka hii katiba tuliyo nayo.

Mifano ipo mingi. Nitaitaja miwili ya hivi karibuni ambayo wengi mtakuwa mnaikumbuka.

Baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alipiga marufuku watu kufanya shughuli za kisiasa kwa kisingizio kwamba ‘siasa sasa zimeshaisha na ni wakati wa kufanya kazi’. Hiyo ni licha ya kwamba shughuli hizo ni haki za kikatiba kwa Mtanzania yeyote yule.

Baada ya Rais Magufuli kufariki, baadhi ya wajuzi na wajuvi wa mambo ya katiba walituambia kwamba Rais Samia alipaswa kulivunja baraza la mawaziri na kuunda serikali mpya.

Hilo halikufanyika. Hivyo maana yake ni kwamba naye aliikiuka katiba.

Sasa nimewaza: kama hii katiba iliyopo inakiukwa wazi wazi namna hii na hamna lolote la maana linalofanyika kupinga ukiukwaji huo, hiyo katiba mpya inahitajika ili iweje?

Mara karibu zote ambapo katiba imeonekana kukiukwa, hakuna cha maana ambacho wananchi tumefanya zaidi ya kujimwambafy humu kwenye mitandao.

Hakuna aliyethubutu kuingia barabarani na kupinga. Hakuna aliyefungua kesi mahakamani. Tumelia lia tu humu mitandaoni.

Sasa hiyo katiba mpya tukiipata, ikikiukwa ndo itatuwezesha kupata ujasiri wa kupinga kukiukwa kwake?

Nimeanza kudhani pengine tatizo letu si katiba mpya pekee. Tatizo letu kubwa ni sisi wenyewe. Tunaachia tu mambo yaende hata kama yapo kinyume na katiba.

A new constitution will not be worth the paper it’s written on if we allow and let the one we have to be breached with impunity!
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji817]
 
Kutokufuatwa kwa katiba iliyopo ni kutokana na madhaifu yaliyoko kwenye katiba yenyewe yanayotoa nafasi kwa baadhi ya watu kutokuiheshimu na bado wasiwajibike. Katiba mpya itaziba mianya hiyo.

Mifano ni mingi lakini ya msingi kabisa ni hii ya watendaji wakuu (Rais, Spika, na wenzao) kutokuwajibika kwa makosa YOYOTE wawepo ofisini.

Tume ya uchaguzi, Vyombo vya dola, bunge na mahakama nk kuwajibika kwa serikali ambayoeti ni mhimili uliojichimbia zaidi.

Tunataka katiba yenye kurejesha uwajibikaji wa serikali nzima kwa wananchi. Katiba ambayo mihimili yote ya utawala itakuwa huru.

Ya bwana Nyani Ngabu ni kelele nyingine za watu wale wale, za kujaribu kutuondoa kwenye reli kwa mara nyingine.

Hatudanganyiki!

Habari ndiyo hiyo.
Very well said. Katiba iliyopo inajihalalishia kuvunjwa kwasababu no accountability.

Katiba mpya yenye kuipa mihili yote nguvu zake, ndiyo itakuwa bora. Ya sasahivi, rais ndo kila kitu. Hata yeye anaamuwa kuwa hakutakuwepo kwa uwajibishwaji kwa yeyote kwenye mihimili mingine. Mfano mwendazake alipoamuwa kuwa hata Ndugai hashitakiwi hata akivunja katiba. Mahakama zinafanya kazi na kutoa maamuzi kumfurahisha rais tu.
 
Tatizo kubwa ni uelewa wa wananchi kuhusu katiba na umuhimu wake.
Viongozi wengi huvunja katiba kwa faida yao na hakuna wa kuhoji au kuchukua hatua yoyote kuilinda.
Wakati mwingine baadhi ya wananchi wameshangilia uonevu na uvunjifu wa katiba waziwazi, na hili halikuwaacha nyuma viongozi wa dini ambao walitegemewa kuwa watetezi wa haki.
 
Kama huitaki kwanin unawajaza watu ujinga kuwa hata ikija haina faida? Tafsiri yake ni nin
Hujaelewa kabisa ulichokisoma!

Tafuta mtu akusomee na akueleweshe kilichoandikwa.
 
Katiba iliyopa sasa ina kwamisha hata hiyo katiba mpya kuwepo...
 
Ni sahihi kabisa kuwa tunapaswa kupata katiba mpya inayoendana na mazingira ya sasa lkn tusiishie tu ktk katiba ya taifa tunalazimika kubadili na katiba za vyama vyetu ziendane na nyakat,umungu mtu kwenye vyama vyetu umeshamiri mno kuanzia chama tawala mpaka wapinzan huwez pata nafasi yoyote ya uwakilish inayohusu udhamin wa chama mpaka usipingane na mwenyekit kimtazamo hili ni tatizo ambalo wengi wetu hatulizungumzii na wachache wanaothubutu kutoa mtazamo tofauti na mwenyekit lazima ufanyiwe kebehi tena na wale ambao mara zote wanajitanabaisha km wanademokrasia.
 
Katiba siyo nyumba!

Si ajabu ndo maana hujaelewa!!!!
Hoja yako ni kuwa kwa nini tunadai katiba mpya wakati iliyopo haiheshimiwi? Hii ni hoja mfu kwa sababu huenda katiba iliyopo haiheshimiwi kwa kuwa ni mbovu na imepitwa na wakati. Tunataka katiba inayoendana na wakati huu, inakubalika na inatekelezeka.
 
Mimi nimekuwa muumini wa katiba mpya tangu enzi na enzi. Kabla hata JF haijazaliwa.

Niliamini hivyo kwa sababu unapobadili mfumo wa kisiasa, basi ni lazima pia ubadili sheria na taratibu zitazotumika kuuongoza huo mfumo mpya.

Hivyo basi, ilipaswa tokea mwanzo, yaani 1992, tuliporudi tena kwenye mfumo wa vyama vingi, kubadili kabisa katiba ili iendane na hayo mazingira mapya.

Hilo halikufanyika. Kilichofanyika ni kubadili badili tu vitu vidogo vya hapa na pale kwenye katiba iliyokuwepo wakati huo, basi.

Tokea 1995, tumeona ni jinsi gani watawala wa CCM wanavyoweza kuikiuka hii katiba tuliyo nayo.

Mifano ipo mingi. Nitaitaja miwili ya hivi karibuni ambayo wengi mtakuwa mnaikumbuka.

Baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alipiga marufuku watu kufanya shughuli za kisiasa kwa kisingizio kwamba ‘siasa sasa zimeshaisha na ni wakati wa kufanya kazi’. Hiyo ni licha ya kwamba shughuli hizo ni haki za kikatiba kwa Mtanzania yeyote yule.

Baada ya Rais Magufuli kufariki, baadhi ya wajuzi na wajuvi wa mambo ya katiba walituambia kwamba Rais Samia alipaswa kulivunja baraza la mawaziri na kuunda serikali mpya.

Hilo halikufanyika. Hivyo maana yake ni kwamba naye aliikiuka katiba.

Sasa nimewaza: kama hii katiba iliyopo inakiukwa wazi wazi namna hii na hamna lolote la maana linalofanyika kupinga ukiukwaji huo, hiyo katiba mpya inahitajika ili iweje?

Mara karibu zote ambapo katiba imeonekana kukiukwa, hakuna cha maana ambacho wananchi tumefanya zaidi ya kujimwambafy humu kwenye mitandao.

Hakuna aliyethubutu kuingia barabarani na kupinga. Hakuna aliyefungua kesi mahakamani. Tumelia lia tu humu mitandaoni.

Sasa hiyo katiba mpya tukiipata, ikikiukwa ndo itatuwezesha kupata ujasiri wa kupinga kukiukwa kwake?

Nimeanza kudhani pengine tatizo letu si katiba mpya pekee. Tatizo letu kubwa ni sisi wenyewe. Tunaachia tu mambo yaende hata kama yapo kinyume na katiba.

A new constitution will not be worth the paper it’s written on if we allow and let the one we have to be breached with impunity!
I totally agree. In my view, it's not because we're pathetic weaklings and cowards It's because we lack the instructions that hold leaders accountable and protect our freedom to question. Hence even putting issues on the table in risky business, depending on the mood of those in power... and their administrators. [emoji2376]
 
Back
Top Bottom