Katiba Mpya ya nini kama hii tuliyonayo hatuiheshimu?

Katiba mpya ni muhimu sababu kuu ni moja kwa sasa hakuna mahali watawala wa ngazi ya juu wanaweza kuwajibishwa ipasavyo...

Pia mamlaka makubwa yamejazwa sehemu moja , tukipata katiba ikawa na mgawanyo na zikawepo checks and balances halisi sio hizi za sasa za maigizo ambapo mahakama haina meno na bunge linaendeshwa kama kikao cha familia ...

Hakuna mtawala atakayeshindwa kuogopa maana atakua anajua akivurunda nini kinafuata sio ya sasa unamwambia rais hatoshitakiwa kokote mara matokeo ya ubunge na udiwani yanaweza kuhojiwa mahakamani ila sio ya urais does it make sense na wote wanafanya chaguzi siku moja??
 
Sawa. CCM ndo wanavunja katiba.

What have you done about it?
Mtoa mada kaongea ukweli 100% kaongelea katiba asilimia kubwa hatujui kilichoandikwa ndani tunaenda kuijadili katiba kwa matukio tu hakuna mahakama inayoilinda katiba kwa uhuru katika kuitafsiri hapa sioni hoja ya mpya maana hata hiyo itavunjwa tu. Shida ya sisi wa Tanzania mada imeongelea katiba lakini wachangiaji moja kwa moja wameanza uchama. Hii ni kama ukitaka kuongelea mpira wetu kwa nia nzuri tu watu wanaurukia usimba na uyanga. Lazima tuwe referee asiyekuwa na team kukaa na kuilinda katiba kisheria haijalishi katiba nzuri au mbaya ila lazima ifuatwe na wote.
 
Mimi nimekuwa muumini wa katiba mpya tangu enzi na enzi. Kabla hata JF haijazaliwa.

Niliamini hivyo kwa sababu unapobadili mfumo wa kisiasa, basi ni lazima pia ubadili sheria na taratibu zitazotumika kuuongoza huo mfumo mpya.

Hivyo basi, ilipaswa tokea mwanzo, yaani 1992, tuliporudi tena kwenye mfumo wa vyama vingi, kubadili kabisa katiba ili iendane na hayo mazingira mapya.

Hilo halikufanyika. Kilichofanyika ni kubadili badili tu vitu vidogo vya hapa na pale kwenye katiba iliyokuwepo wakati huo, basi.

Tokea 1995, tumeona ni jinsi gani watawala wa CCM wanavyoweza kuikiuka hii katiba tuliyo nayo.

Mifano ipo mingi. Nitaitaja miwili ya hivi karibuni ambayo wengi mtakuwa mnaikumbuka.

Baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alipiga marufuku watu kufanya shughuli za kisiasa kwa kisingizio kwamba ‘siasa sasa zimeshaisha na ni wakati wa kufanya kazi’. Hiyo ni licha ya kwamba shughuli hizo ni haki za kikatiba kwa Mtanzania yeyote yule.

Baada ya Rais Magufuli kufariki, baadhi ya wajuzi na wajuvi wa mambo ya katiba walituambia kwamba Rais Samia alipaswa kulivunja baraza la mawaziri na kuunda serikali mpya.

Hilo halikufanyika. Hivyo maana yake ni kwamba naye aliikiuka katiba.

Sasa nimewaza: kama hii katiba iliyopo inakiukwa wazi wazi namna hii na hamna lolote la maana linalofanyika kupinga ukiukwaji huo, hiyo katiba mpya inahitajika ili iweje?

Mara karibu zote ambapo katiba imeonekana kukiukwa, hakuna cha maana ambacho wananchi tumefanya zaidi ya kujimwambafy humu kwenye mitandao.

Hakuna aliyethubutu kuingia barabarani na kupinga. Hakuna aliyefungua kesi mahakamani. Tumelia lia tu humu mitandaoni.

Sasa hiyo katiba mpya tukiipata, ikikiukwa ndo itatuwezesha kupata ujasiri wa kupinga kukiukwa kwake?

Nimeanza kudhani pengine tatizo letu si katiba mpya pekee. Tatizo letu kubwa ni sisi wenyewe. Tunaachia tu mambo yaende hata kama yapo kinyume na katiba.

A new constitution will not be worth the paper it’s written on if we allow and let the one we have to be breached with impunity!
Kuna watu wajuaji ukiwaambia Maandamano ya kwenye keyboard hayana tija huwa wanakuwa wakali kama mbogo, fikiria hata yule kiongozi wao wa ushubwada kule twitter Miss Kigogo hana hata ujasiri wa ku reveal identity yake lakini kutwa kucha anajidai kudai Katiba mpya.
 
Katiba yetu inasema mihimili mitatu iko huru lakini sote tunajuwa mihimili mitatu iko lakini sio huru na hakuna muhimili unaotakiwa kuwa huru kama mahakama sehemu pekee mtu anaweza kutafuta haki yake na wajibu wa mahakama kuilinda katiba na wananchi wake. tuanzie hapa je tuna mahakama huru? japo katiba inasema huru, hatukelelezi yaliyopo mapya yatatekelezwa vipi. Kuna safari ndefu sana katika hili japo kuwa kuna watu wanasema tu tume iwe huru je sote tunajuwa nchi hii imegawanyika uwe CCM au uwe mpinzani unazi upo ni vipi tuna define huru? TFF tu tunasikia hawa ni team fulani wanatuhujumu wakija wengine hawa wanahujumu wako team fulani. Mimi nataka mtu aniambie tu tume huru utaichaguwa namna gani? Hapa ni kuipa nguvu mahakama kuwa 100% huru sababu haki hata Mungu kasisitiza na jopo hili la ma judge lifanye maamuzi kuilinda katiba iliyopo au hata itakayokuja kuwe na black and white.
 
Kwa hiyo ni bora iwe inakiukwa kuliko kufuatwa kikamilifu?
Watz walio wengi si waamini wazuri wa utawala wa sheria, hata hao wanaolalamikia Katiba mpya, kuna wakati wanapata michongo kwa shortcuts kutokana na Katiba ya Sasa.
 
Katiba yetu inasema mihimili mitatu iko huru lakini sote tunajuwa mihimili mitatu iko lakini sio huru na hakuna muhimili unaotakiwa kuwa huru kama mahakama sehemu pekee mtu anaweza kutafuta haki yake na wajibu wa mahakama kuilinda katiba na wananchi wake. tuanzie hapa je tuna mahakama huru? japo katiba inasema huru, hatukelelezi yaliyopo mapya yatatekelezwa vipi. Kuna safari ndefu sana katika hili japo kuwa kuna watu wanasema tu tume iwe huru je sote tunajuwa nchi hii imegawanyika uwe CCM au uwe mpinzani unazi upo ni vipi tuna define huru? TFF tu tunasikia hawa ni team fulani wanatuhujumu wakija wengine hawa wanahujumu wako team fulani. Mimi nataka mtu aniambie tu tume huru utaichaguwa namna gani? Hapa ni kuipa nguvu mahakama kuwa 100% huru sababu haki hata Mungu kasisitiza na jopo hili la ma judge lifanye maamuzi kuilinda katiba iliyopo au hata itakayokuja kuwe na black and white.
Uonesha wapi panapoonesha mahakama haipo huru ?
 
Mifano mitatu tu wakati JPM kukataza mikutano ya kisiasa au kuandamana ni haki ya wananchi lakini mahakama kimyaa. Hawa wabunge 19 kila mtu anajuwa katiba imevunjwa mahakama kimyaa. kuna mtu kaachiwa usiku kenda kuapishwa mbunge mahakama kimyaa. DPP anaweza ku bargain kabla ya kufungua mashtaka lakini leo kesi iko mahakamani DPP akawa yeye kama judge anaenda ana bargain mtu anaachiwa kwa makosa ya wizi makubwa tu. kuna watu wamefungwa makosa ya kawaida tu labda mtu aliiba TV mwambia rudisha TV toka, kaiba mbuzi lipa mbuzi toka.
 
Ok ok....Wewe kama mwananchi unayetambua kwamba ile haki yako imevunjwa ulichukua hatua zipi kuitafuta au ndio ulisubiri mahakama ikusemee ?
 
Mimi hiyo katiba nimeiona wapi? sijui hata iko wapi mpaka niwe na muda wa kuisoma au unadhani kufungua kesi ni bure hiyo haki tu ina gharama zake. Hiyo sio kazi yangu ni kazi ya mahakama ya katiba kuilinda kuhakikisha hakuna mtu anavunja katiba na sheria.
 
Ni hao viongozi wanaoapa kutwa kuilinda katiba na sheria na kuhifadhi siri kila siku wanaapa na hata sijui siri gani hizo wanalinda.
 
Mimi nimekuwa muumini wa katiba mpya tangu enzi na enzi. Kabla hata JF haijazaliwa.

Niliamini hivyo kwa sababu unapobadili mfumo wa kisiasa, basi ni lazima pia ubadili sheria na taratibu zitazotumika kuuongoza huo mfumo mpya.

Hivyo basi, ilipaswa tokea mwanzo, yaani 1992, tuliporudi tena kwenye mfumo wa vyama vingi, kubadili kabisa katiba ili iendane na hayo mazingira mapya.

Hilo halikufanyika. Kilichofanyika ni kubadili badili tu vitu vidogo vya hapa na pale kwenye katiba iliyokuwepo wakati huo, basi.

Tokea 1995, tumeona ni jinsi gani watawala wa CCM wanavyoweza kuikiuka hii katiba tuliyo nayo.

Mifano ipo mingi. Nitaitaja miwili ya hivi karibuni ambayo wengi mtakuwa mnaikumbuka.

Baada ya kuingia madarakani, Rais Magufuli alipiga marufuku watu kufanya shughuli za kisiasa kwa kisingizio kwamba ‘siasa sasa zimeshaisha na ni wakati wa kufanya kazi’. Hiyo ni licha ya kwamba shughuli hizo ni haki za kikatiba kwa Mtanzania yeyote yule.

Baada ya Rais Magufuli kufariki, baadhi ya wajuzi na wajuvi wa mambo ya katiba walituambia kwamba Rais Samia alipaswa kulivunja baraza la mawaziri na kuunda serikali mpya.

Hilo halikufanyika. Hivyo maana yake ni kwamba naye aliikiuka katiba.

Sasa nimewaza: kama hii katiba iliyopo inakiukwa wazi wazi namna hii na hamna lolote la maana linalofanyika kupinga ukiukwaji huo, hiyo katiba mpya inahitajika ili iweje?

Mara karibu zote ambapo katiba imeonekana kukiukwa, hakuna cha maana ambacho wananchi tumefanya zaidi ya kujimwambafy humu kwenye mitandao.

Hakuna aliyethubutu kuingia barabarani na kupinga. Hakuna aliyefungua kesi mahakamani. Tumelia lia tu humu mitandaoni.

Sasa hiyo katiba mpya tukiipata, ikikiukwa ndo itatuwezesha kupata ujasiri wa kupinga kukiukwa kwake?

Nimeanza kudhani pengine tatizo letu si katiba mpya pekee. Tatizo letu kubwa ni sisi wenyewe. Tunaachia tu mambo yaende hata kama yapo kinyume na katiba.

A new constitution will not be worth the paper it’s written on if we allow and let the one we have to be breached with impunity!
Wasio iheshimu ndio hawaitaki , na Wanao iheshumu wanaona mapungufu , RAIS ANASEMA MIMI NIMEAMUA HIVI NA VILE na si sheria. WTF
 
Ni hao viongozi wanaoapa kutwa kuilinda katiba na sheria na kuhifadhi siri kila siku wanaapa na hata sijui siri gani hizo wanalinda.
Umeona jinsi unavyoruka ruka kama maharagwe, yaani WATANZANIA kitu tunachokiweza ni kulaumu laumu n kukosoa wengine.
 
Mimi hiyo katiba nimeiona wapi? sijui hata iko wapi mpaka niwe na muda wa kuisoma au unadhani kufungua kesi ni bure hiyo haki tu ina gharama zake. Hiyo sio kazi yangu ni kazi ya mahakama ya katiba kuilinda kuhakikisha hakuna mtu anavunja katiba na sheria.
Endelea kusubiri Mahakama iwe inasimamia haki ambazo hata wewe mwananchi unatakiwa kuzilinda.
 
Back
Top Bottom