Katiba Mpya ya nini kama hii tuliyonayo hatuiheshimu?

Upo sahihi 💯
 
Umeona jinsi unavyoruka ruka kama maharagwe, yaani WATANZANIA kitu tunachokiweza ni kulaumu laumu n kukosoa wengine.
Sasa ukapinge kitu hujui nini kimeandikwa ndani? Hizo nchi nyingine kuweka mahakama kuu kulinda katiba ya nchi wajinga hao? kazi ya mwanasheria mkuu ni nini? wewe kwa akili yako unadhani kila mtu anaweza kusoma katiba na akailewa kama unasoma gazeti. ndio mikataba inapitiwa na wana sheria sio unakurupuka tuu ku sign kuna lugha inatumika humo na vipengele ni watu waliobobea tu ndio wanaweza kutafsiri sio kila.

Mikataba midogo tu inaandikwa na mwanasheria sembuse katiba. hiyo katiba inauzwa madukani ununue usome, kila kitu kinafichwa tu sehemu pekee naiona inashikwa siku anaapishwa mtu na wala hasomi yeye kaibeba tu naapa kuilinda katiba ukimuuliza unaapa unajuwa kilichopo ndani hawajui. nenda nchi zote zilizoendelea katiba inalindwa na mahakama na bunge.
 
Endelea kusubiri Mahakama iwe inasimamia haki ambazo hata wewe mwananchi unatakiwa kuzilinda.
Mimi sikuelewi unataka nilinde kitu sijawahi kukisoma wala sijui kilichoandikwa ndani? wawakilishi wa wananchi bungeni ndio wanawakilisha watu na wanaapa kulinda maana wako kwa kazi hiyo hawajui kilichomo unataka mimi naye amka asubuhi kutafuta rizki mpaka usiku nikakae nasoma kitabu watoto wale nini? kila jukumu limepangiwa watu wake. wale tunawachagua kutuwakilisha, kutunga sheria na kulinda katiba ya nchi wao wanaweza kupiga hata kura ya kutokuwa na imani na rais ikiwa anavunja sheria sio mimi. Mimi ukiisha uchaguzi imeisha hiyo.
 
Mkuu umemuelewa toa mada? Yeye anauliza hii katiba mbovu tulionayo kuna baadhi ya mambo Rais/na baadhi ya viongozi wanafanya kwa kukiuka katiba na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa

Sasa swali la msingi hiyo katiba mpya ikiwepo na CCM ikaendelea kuvunja katiba ni hatua gani zitafuata au tutaendelea kulalamika JF kwa kuficha majina yetu?
 
Yote hayo unayosema Mahakama kimyaaa kuna Wananchi/Mwananchi yoyote alikwenda kulalamika na Mahakama ikakataa kumsikilza?

Na kama sote Wananchi tunakubali kuwa matendo hayo ni uvunjifu wa amani ni hatua gani tumechukua kuhakikisha kuwa katiba yetu tunailinda? Au sisi ni watu wa bora liende na kupiga mbinja mitandaoni?
 
Kutochukua hatua ndiyo upuuzi wenyewe wa kitanzania
 
Kutochukua hatua ndiyo upuuzi wenyewe wa kitanzania
Na Watanzania kwa jinsi tulivyo hata akija kiongozi wa aina gani atatubuluza tu tunamaneno meeengiiiii tukikaa kwenye vijiwe vya kahawa au JF lakini vitendo 0
 
Mifano uliyotoa ndio sababu ya kudai Katiba Mpya. Hao uliosema wamevunja Katiba ni marais wa nchi yetu na kwa Katiba iliyopo hawawezi kushtakiwa popote kwa lolote watakalotenda wakati wa urais wao. Kwa sababu hiyo kufungua mashtaka dhidi yao ni kupoteza wakati. Ni kama ilivyo sasa hivi kwa Spika ambae nae amepewa immunity na hivyo kumruhusu kufanya lolote atakalo bila kuogopa atawajibika. Katiba mpya hopefully itarekebisha yote haya na kuwarudishia wananchi nguvu za kuwawajibisha viongozi wao pale ambapo wataenda kinyume na matakwa ya Katiba.

Amandla...
 
Nyani Ngabu Mkuu let's be open minded, why we need newer constitution, I say newer because ours is still new, not even 50 years old. Katiba sio msahafu unaweza badilishwa time yoyote ili mradi uwe kwa manufaa ya waTanzania wote.
 
Yaani sasa unasema kitu ambacho kulingana na umuhimu wake na 'exposure' yako eti ni 'kelele', kaaazi kwelikweli....
Hata kuandika ukaeleweka huwezi!

Kusoma na kuelewa ulichokisoma utaweza kweli???
 
Fundi umenielewa kweli?

Sawa, hata kama katiba yetu ya sasa hairuhusu viongozi wetu hao wa juu kushitakiwa kibinafsi, hiyo haina maana ndo wawe wanavunja katiba.

Wanapovunja katiba sasa hivi, kwenda mahakamani dhidi yao si kwa kuwashitaki wao binafsi na wakipatikana na makosa wafungwe jela.

La hasha! Bali lengo ni kutaka kubatilisha hicho walichokifanya ambacho ndo kimekiuka katiba.

Magufuli alikataza watu kufanya shughuli za kisiasa nchi nzima. Jambo ambalo ni kinyume kabisa na katiba.

Nani alienda mahakamani, hata kwa kujaribu tu, kuipinga amri hiyo?

Jambo linaruhusiwa kikatiba. Yeye akalikataza. Kwa nini mahakamani yetu haikutoa tafsiri juu ya uhalali wa katazo hilo?

Kama mtu angeenda mahakamani na kufungua shauri la kupinga katazo hilo, hiyo haina maana kuwa mtu huyo alienda mahakamani kumshitaki Rais Magufuli kama mtu binafsi.

Au labda mimi tu ndo sijui na labda wapo walioenda mahakamani na kupinga katazo hilo na mahakamani ikalitolea uamuzi?

Kwa hiyo, hivyo ndivyo ninavyomaanisha ninaposema kwamba hata hii katiba ya sasa inapokiukwa, hatufanyi chochote kile. Tunaachia tu ikiukwe halafu tunajipa moyo na kujifariji kuwa hatuwezi kufanya chochote kwa sababu Rais hawezi kushitakiwa!

Sasa tukipata katiba mpya na bado ikaendelea kukiukwa, tutafanya nini endapo hii ya sasa huwa inakiukwa na hatufanyi chochote kile?
 
Ado Shaibu akiwakilishwa na Fatma Karume alimshitaki Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa kuvunja Katiba katika uteuzi wake wa Feleshi kuwa Attorney General kwa sababu Feleshi hakuwa na sifa zilizoainishwa kwenye Katiba. Mahakama ika rule kuwa mashtaka hayana mashiko kwa sababu ya immunity ya urais aliokuwa nao mshtakiwa. Baada ya hapo Fatma akashughulikiwa na kunyang'anywa leseni yake ya uwakili.

Amandla...
 
Ok!

Vipi kuhusu kutokufanya siasa kwa vyama vya upinzani?
 
Bado sijaelewa logic ya hoja yako!

Kwamba kama ulikuwa unalala nyumba inayovuja hutakiwi kukarabati kwa sababu nayo itakuja kuvuja!
 
Bado sijaelewa logic ya hoja yako!

Kwamba kama ulikuwa unalala nyumba inayovuja hutakiwi kukarabati kwa sababu nayo itakuja kuvuja!
Katiba siyo nyumba!

Si ajabu ndo maana hujaelewa!!!!
 
Baada ya kupata hiyo shule sidhani kama walijisumbua. Ulikuwa uthibitisho wa walichojua.

Amandla...
Kwani kipi kilichotangulia?

Kupigwa marufuku shughuli za kisiasa au hiyo kesi ya Shaibu?
 
Ok!

Vipi kuhusu kutokufanya siasa kwa vyama vya upinzani?
Mwaka jana Mahakama ya Afrika ilitoa ruling kuwa kuzuia watu kupinga matokeo ya kura za urais ni kuvunja Katiba na hivyo watu waruhusiwe. Kilichofuata ni kutangaziwa kuwa hakuna ruksa kwenda kwenye Mahakama ya Afrika na kuwa Tanzania ina nia ya kujitoa kwenye hiyo Mahakama!

Amandla...
 
Ulichojibu sicho nilichokuuliza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…