Rorscharch
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,435
- 3,120
Kuna maradhi ya kimyakimya yanayoshambulia mataifa ya Kiafrika, si kwa mapanga wala risasi, bali kwa nyaraka nzuri zilizopambwa kwa wino wa kimataifa. Maradhi haya si mengine bali ni imani butu kwamba katiba nzuri, yenye maneno matamu ya haki na uhuru, ni tiba ya kila ugonjwa wa taifa. Afrika Kusini ni mgonjwa huyu anayesinzia kwenye kitanda cha katiba yake, akipumulia mashine ya “utawala wa sheria” huku viungo vya maendeleo vikimkatika mmoja baada ya mwingine.
Hili halikutokea kwa bahati mbaya. Lilitabiriwa.
Alikuwa anazungumzia India, lakini alikuwa anatuonya sisi sote: msidhani kuwa mnapopambwa na karatasi za haki, basi mpo salama.
Kwa kutumia darubini ya kisiasa, maneno haya yamekuwa unabii ulioishi Afrika Kusini. Nchi hiyo ilijifungua mwaka 1994 si kwa mapinduzi ya wananchi, bali kwa makubaliano ya meza. Katiba yao haikuchongwa kwa jasho la waathirika, bali kwa peni za mawakili walioketi meza moja na waliowahi kuwatesa. Na hapo ndipo tatizo lilipoanzia.
Tangu hapo, Afrika Kusini imekuwa mfano wa nchi iliyopewa uhuru kwa njia ya nyaraka, si mapambano. Taifa lililopewa haki kabla ya uwezo. Taifa linalofurahia katiba nzuri huku wakazi wake wakililia huduma mbovu. Kila pendekezo la maendeleo hufungwa na taratibu, na kila sauti ya mabadiliko hufunikwa na “mashauriano ya kitaasisi.”
Katika mfumo huu wa "utawala wa sheria uliotukuka", hata majaji wanaojaribu kutumia katiba kutetea wananchi dhidi ya makampuni ya kimataifa huadhibiwa. Kesi ya Jaji Selby Mbenenge, aliyeizuia Shell kuchimba mafuta Eastern Cape kwa kutetea mazingira na jamii za asili, ni somo la aibu. Badala ya sifa, akapewa kamati ya nidhamu, kashfa za WhatsApp, na mashambulizi ya kimfumo.
Hakuadhibiwa kwa kuvunja sheria, bali kwa kuvunja miiko ya kimyakimya inayosema: "Sheria ni nzuri mradi isizue wadosi."
Hapa nyumbani, Tanzania haina mchakato rasmi wa katiba mpya. Kuna shinikizo – tena linatoka kwa wapinzani na wanaharakati wa kiraia – lakini mamlaka bado zimenyamaza kwa ukimya wa heshima. Tunasikia “tuko kwenye majadiliano.” Majadiliano ya miaka ishirini? Ni kama kupika ugali kwa kuni ya mvua.
Lakini hata tukianzisha mchakato huo kesho, je, tutakuwa tumebadili mfumo au tumebadili maandishi tu?
Afrika Kusini ilikuwa na katiba bora zaidi Afrika. Leo hii, wanaangalia katiba hiyo kama kaburi lenye maandishi ya dhahabu huku taifa likioza ndani. Walichokosa ni mfumo wa utekelezaji, si maneno ya matumaini.
Tunaambiwa katiba ni mkataba wa kijamii. Lakini mkataba usiosomwa, usiotekelezwa, una faida gani? Tunaweza kuandika aya nzuri kuhusu haki ya ardhi, lakini bado tukawanyima wakulima ardhi hiyo kwa sababu ya “utaratibu.” Tunaweza kusema kila mtu ana haki ya maji, lakini mkurugenzi akaogopa kuchimba kisima hadi apate “muongozo wa juu.”
Katiba bora bila mfumo wa utekelezaji ni usanii wa kisheria unaolisha midahalo badala ya watoto.
Je, Watanzania tumejiandaa kwa katiba mpya? Au tunatafuta mzinga mwingine wa maneno ya matumaini, huku tabia yetu ya kisiasa na taasisi zetu zikiwa zilezile?
Katiba mpya haitafanya kazi ikiwa kila kiongozi ataendelea kuwa kiongozi wa chama kabla ya kuwa kiongozi wa taifa. Haitasaidia ikiwa kila afisa ataogopa kuchukua hatua hadi apate “baraka.” Hatuwezi kuandika mabadiliko mezani na kuyategemea yatokee barabarani.
Leo, katiba yao imebaki kuwa kaburi lenye maandishi mazuri, huku taifa likioza ndani.
Je, sisi tutajifunza kabla ya kuzikwa?

Mwaka 2009, Lee Kuan Yew – dikteta mwerevu wa Singapore – alisema:
"India ni ya kidemokrasia mno kupanga, ya kisheria mno kutekeleza, na ya kitaratibu mno kuharakisha."
Alikuwa anazungumzia India, lakini alikuwa anatuonya sisi sote: msidhani kuwa mnapopambwa na karatasi za haki, basi mpo salama.
Kwa kutumia darubini ya kisiasa, maneno haya yamekuwa unabii ulioishi Afrika Kusini. Nchi hiyo ilijifungua mwaka 1994 si kwa mapinduzi ya wananchi, bali kwa makubaliano ya meza. Katiba yao haikuchongwa kwa jasho la waathirika, bali kwa peni za mawakili walioketi meza moja na waliowahi kuwatesa. Na hapo ndipo tatizo lilipoanzia.
Katiba: Mshipa wa Haki au Mnyororo wa Mageuzi?
Tangu hapo, Afrika Kusini imekuwa mfano wa nchi iliyopewa uhuru kwa njia ya nyaraka, si mapambano. Taifa lililopewa haki kabla ya uwezo. Taifa linalofurahia katiba nzuri huku wakazi wake wakililia huduma mbovu. Kila pendekezo la maendeleo hufungwa na taratibu, na kila sauti ya mabadiliko hufunikwa na “mashauriano ya kitaasisi.”
Katika mfumo huu wa "utawala wa sheria uliotukuka", hata majaji wanaojaribu kutumia katiba kutetea wananchi dhidi ya makampuni ya kimataifa huadhibiwa. Kesi ya Jaji Selby Mbenenge, aliyeizuia Shell kuchimba mafuta Eastern Cape kwa kutetea mazingira na jamii za asili, ni somo la aibu. Badala ya sifa, akapewa kamati ya nidhamu, kashfa za WhatsApp, na mashambulizi ya kimfumo.
Hakuadhibiwa kwa kuvunja sheria, bali kwa kuvunja miiko ya kimyakimya inayosema: "Sheria ni nzuri mradi isizue wadosi."
Tanzania Inatafuta Katiba Mpya: Lakini Kwa Nini?
Hapa nyumbani, Tanzania haina mchakato rasmi wa katiba mpya. Kuna shinikizo – tena linatoka kwa wapinzani na wanaharakati wa kiraia – lakini mamlaka bado zimenyamaza kwa ukimya wa heshima. Tunasikia “tuko kwenye majadiliano.” Majadiliano ya miaka ishirini? Ni kama kupika ugali kwa kuni ya mvua.
Lakini hata tukianzisha mchakato huo kesho, je, tutakuwa tumebadili mfumo au tumebadili maandishi tu?
Afrika Kusini ilikuwa na katiba bora zaidi Afrika. Leo hii, wanaangalia katiba hiyo kama kaburi lenye maandishi ya dhahabu huku taifa likioza ndani. Walichokosa ni mfumo wa utekelezaji, si maneno ya matumaini.
Katiba Bila Nguvu ni Kama Biblia Isiyosomwa
Tunaambiwa katiba ni mkataba wa kijamii. Lakini mkataba usiosomwa, usiotekelezwa, una faida gani? Tunaweza kuandika aya nzuri kuhusu haki ya ardhi, lakini bado tukawanyima wakulima ardhi hiyo kwa sababu ya “utaratibu.” Tunaweza kusema kila mtu ana haki ya maji, lakini mkurugenzi akaogopa kuchimba kisima hadi apate “muongozo wa juu.”
Katiba bora bila mfumo wa utekelezaji ni usanii wa kisheria unaolisha midahalo badala ya watoto.
Siyo Katiba Tunayohitaji, ni Tabia Mpya ya Kisiasa
Je, Watanzania tumejiandaa kwa katiba mpya? Au tunatafuta mzinga mwingine wa maneno ya matumaini, huku tabia yetu ya kisiasa na taasisi zetu zikiwa zilezile?
Katiba mpya haitafanya kazi ikiwa kila kiongozi ataendelea kuwa kiongozi wa chama kabla ya kuwa kiongozi wa taifa. Haitasaidia ikiwa kila afisa ataogopa kuchukua hatua hadi apate “baraka.” Hatuwezi kuandika mabadiliko mezani na kuyategemea yatokee barabarani.
Afrika Kusini ilikuwa na kila kitu—haki, uhuru, usawa, katiba—lakini ikasahau kuwa mapambano halisi si ya kisheria, bali ya kiutamaduni wa utawala.