Katiba waliyoivuruga UKAWA ilikuwa na sifa hizi hapa

Katiba waliyoivuruga UKAWA ilikuwa na sifa hizi hapa

Sikuona swali bali uchanga wa hoja za upande wa pili. Miaka 30+ ya upinzani wa blaablaa. Ni saccos zaidi kuliko political parties. Akina Sugu wana hotel. Heche ana magari na mashamba, Mbowe ndio usiseme, Lema duuu!, Mdee,.... wengine akina msukuma02 ndio wanaswagwa tu kama kondoo kutoka zizi hile hadi lile. Kuna watu walianzia NCCR wakaburuzwa hadi TLP, kutoka TLP wakaburuzwa tena hadi chadema, kutoka chadema wakaburuzwa hadi CHAUMA, kutoka chauma yakaburuzwa tena kurudi CCM na chadema na mengine hayoooo ACT.
To be honest sijui huwa unaandika utoto gani? Haya uliyoandika yana uhusiano gani na mada yako, ama huyo uliyemjibu?!
 
Action and reaction are equal and opposite. Yaani kama yuko mtu ambae yuko tayari kufanya lolote na chochote ili aende Ikulu lazima awepo pia mtu ambae yuko tayari kufanya lolote na chochote ili kumzuia mtu huyo asiende Ikulu. Baada ya hapo "state quo" inapatikana (win-lose). Njia pekee ya kuepusha hili la the survival of the fittest lisitokee ni kwa mazungumzo (dialogue/kiti na meza) tu. Kwenye dialogue mtu hakosi vyote lakini hapati vyote pia.
 
To be honest sijui huwa unaandika utoto gani? Haya uliyoandika yana uhusiano gani na mada yako, ama huyo uliyemjibu?!
Kuonyesha uchanga kwenye kujenga hoja na kufanya tafakuli tunduizi upande wenu unashindwa ku connect.
 
Sawa, UKAWA walijitoa, CCM mkaendelea, nini kinawazuia kumaliza?
Inclusion issues. Katiba ni ghali sana kuiandika, lazima wadau wote muanze na kumaliza pamoja ili katiba iwe na uhai mrefu.
 
To be honest sijui huwa unaandika utoto gani? Haya uliyoandika yana uhusiano gani na mada yako, ama huyo uliyemjibu?!
Hebu msikikize Mayalla maswali aliyomuuliza Lissu. Kama Lissu angeyajibu vizuri maswali ya Pascal vijana wasingekufa Oct29. Kiburi na kujiona unajua kuliko watu wengine ndicho chanzo cha janga.
 
Ww kichwa maji nilikuambia ww ni bendera fuata upepo huna ujualo. Katiba mpya ipi ilivurigwa na Ukawa? Kwa taarifa yako Ukawa waligomea kuendelea kushiriki kwenye bunge lililokuwa linanajishi maoni halali ya wananchi. Lakini wabunge wa ccm na vibaraka wao chini ya muuaji Samia waliendelea na bunge lile hadi kupata katiba pendekezwa.

Alipoingia dhalimu Magu alikuta katiba pendekezwa ikisuburi kura ya maoni, akasema hakuahidi katiba mpya kwenye kampeni zake, hivyo ikawa mwisho wa hiyo katiba mpya iliyochakuliwa na ccm. Hadi hapo ni wapi Ukawa walivuruga? Ama unadhani kila mtu anaweza kupotoshwa na nyie vichwa maji?
👏👏👏👏
 
To be honest sijui huwa unaandika utoto gani? Haya uliyoandika yana uhusiano gani na mada yako, ama huyo uliyemjibu?!
Kama hujui nilichoandika ndiyo diagnosis yenyewe ya upuyangaji kwenye decission making.
Kaeni chini sasa wanajamvi mfanye evaluation ya No reforms no election imewaletea faida na hasara zipi, chama kimeenda mbele au kimezidi kurudi nyuma. Nani alaumiwe na nani hakufanya nini na the way forward.

Nijuavyo mimi hakuna cha maana sasa hivi mnafanya cha kujenga chama zaidi ya kila mtu anasubiri hukumu ya trh 06 kama mavuno ya garbage in garbage out wakati serikali ikiendelea na ukarabati na ujenzi upya wa miundombinu ya wananchi mliyoharibu.
 
Peleka utoto mbali.
 
Inclusion issues. Katiba ni ghali sana kuiandika, lazima wadau wote muanze na kumaliza pamoja ili katiba iwe na uhai mrefu.
Kwanini hamkuishia pale UKAWA walipoishia, moja mkaamuwa kuendelea hadi kutengeneza rasimu ya katiba pendekezwa. Malizieni.
 
Kwanini hamkuishia pale UKAWA walipoishia, moja mkaamuwa kuendelea hadi kutengeneza rasimu ya katiba pendekezwa. Malizieni.
Pesa ilikuwepo ya kuandika rasimu na kilichokwenda kwa mganga hakirudi. Angalau iko rasimu kama wakikubali tuipeleke ikapigiwe kura.

Utopian politics za kudhani kuwa sisi tukienda Ikulu tutafanya maajabu yanayoambana na miujiza .
 
Aliyewazuia ni nani? Malizieni
Acheni kulalama
 
UKAWA waliawaachia muendelee na ujinga wenu wa kuandika rasimu mnayoitaka nyie, ila mkashindwa. Sasa mjilaumu wenyewe kwa kushindwa kuleta katiba mpya.
 
UKAWA waliawaachia muendelee na ujinga wenu wa kuandika rasimu mnayoitaka nyie, ila mkashindwa. Sasa mjilaumu wenyewe kwa kushindwa kuleta katiba mpya.
CCM haina shida na Katiba ya 1977, milio ya Katiba inatokea upande ule wa seng'enge.
 
Katiba mpya ni Kwa maslahi ya Tanzania na si vyama vya siasa.Ni ajabu kuwa Mijadala mingi humu kuhusu katiba mpya inajikita katika misimamo ya vyama vya siasa.Mzalendo wa kweli ataitaka katiba mpya Kwa maslahi mapana ya nchi.Vyama vya siasa huitaka katiba ambayo wanadhani itawapa unafuu na kushinda kirahisi uchaguzi na kuingia madarakani.
 
CCM haina shida na Katiba ya 1977, milio ya Katiba inatokea upande ule wa seng'enge.
Kwa hivyo unakiri Mwenyekiti wenu wa CCM alidanganya, kuwa ataanza mchakato wa Katiba siku 100 baada ya kuapishwa. Pia kwanini CCM chini ya Kikwete ilikubali kupoteza Trilioni Moja kwenye kitu ambacho hakikuwepo au hawakuamini?.
 
Wananchi akina nani? Mbona wananchi pia walivikataa vyama vingi kwa 80% lakini hawakusikilizwa? Hiyo ya serikali 3 ni maoni binafsi ya mwenyekiti wa tume. Na bahati mbaya sana yeye hayuko tayari kupingwa maana yeye alikuwa sehemu ya G55 ambae hakujionyesha wakati ule kwa kumuogopa Mwalimu.
Nilikuwa nafuatilia hoja zako nione wapi palipovurugwa nafurahi umesema mwenyewe. Kumbe lile bunge lenu uchwara lilijipa mamlaka ya kuamua kipi kilizungumzwa na wananchi na kipi kiliwekwa na mtu mmoja? Kwa nini mlimpa mamlaka makubwa namna hiyo mtu ambaye humumuamini? Hivi ninyi masisiemu mnajikuta akina nani kiasi mnaamini mnajua ni nini kila mwananchi wa nchi hii anataka?
 
Katiba mpya ni Kwa maslahi ya Tanzania na si vyama vya siasa.Ni ajabu kuwa Mijadala mingi humu kuhusu katiba mpya inajikita katika misimamo ya vyama vya siasa.Mzalendo wa kweli ataitaka katiba mpya Kwa maslahi mapana ya nchi.Vyama vya siasa huitaka katiba ambayo wanadhani itawapa unafuu na kushinda kirahisi uchaguzi na kuingia madarakani.
Uko sahihi 100%. Tusiungalie ubaya na uzuri wa Katika kama nyenzo ya kwenda na kuzuia vyama kwenda Ikulu, bali tuangalie maslahi ya wananchi na Taifa yanayopatikana au kunyimwa na Katiba iliyopo.

Masilahi ya msingi ya wananchi na Taifa ni haya yafuatayo:

1. Ardhi: Ardhi ndiyo rasilimali kuwa ya kila mtu, familia, ukoo, kabila na Taifa. Migogoro mingi duniani ya mtu na mtu, familia na familia. Ukoo na ukoo, kabila na kabila na nchi na nchi inatokana na kumiliki, kugawana, kutumia na kulinda ardhi. Je, Katiba yetu hii ina shida kwenye kugawana ardhi?

2. Utawala: Upendeleo katika kuchagua viongozi na kusambaza maendeleo kwa kutumia ukabila, udini na ukanda. Je, Katiba yetu ya sasa inaruhusu viongozi watoke dini, kabila au kanda fulanifulani tu? Je, Katiba inaruhusu kiongozi kupeleka maendeleo kwenye dini, kabila au kanda moja na kuziacha kanda nyingine?

3. Umoja: Utaifa unajengwa na umoja wa wananchi usiozingatia dini, kabila, jinsia wala kanda wanazotoka watu. Je, katiba hii inayo kasoro kwenye kuwaweka watu pamoja na kuwafanya wajione wamoja?

4. Uchumi: Je, Katiba hii ni sababu ya kulifanya kundi moja (vijana, wazee, jinsia, dini, kabila, kanda, elimu) kuwa tajiri na lingine kuwa maskani?

5. Ulinzi wa rasilimali: Katiba lazima ilinde rasilimali za watu na taifa kuwa salama. Je, Katiba hii inao uwezo wa kulinda rasilimali za watu na taifa ziwe salama na zisiibiwe ama na viongozi, kundi la watu au hata nchi nyingine?

6. Haki, amani na utulivu. Katiba lazima imhakikishie kila mtu haki, amani na utulivu. Kila mtu anastahili kundendewa kwa haki baada ya kumaliza kutimiza wajibu wake kama raia au mgeni kutoka nchi nyingine. Je, Katiba ina mapungufu gani kwenye jambo hilo la haki, amani na utulivu yanayostahili kurekebishwa?

7. Dira na uelekeo: Katiba lazima iwaonyeshe wananchi kule wanakotaka kwenda kama taifa na mtu mmojammoja ili wajue kwenye safari hiyo wajiandaje. Wavae viatu vya aina gani na nguo za aina gani. Wasome nini, wale nini, na wabebe nini kwaajili ya safari hiyo?. Je katiba yetu inayo mapungufu kwenye eneo hilo yanayohitaji kubadilishwa?

Inaonekana Katiba yetu hii tuliyonayo ni nzuri sana kwakuwa kelele zetu za kutaka Katiba mpya hazihusiani na mgawano wa ardhi, udini, ukabila, ukanda, jinsia wala upendeleo kwenye maendeleo ya watu. Ni kelele kwaajili ya tume ya uchaguzi tu baasi. Na watu wa vyama wako tayari Katiba irekebishwe kwenye kipengele hicho cha tume tu baaasi. Hii ni kuonyesha Katiba yetu iko vizuri ila kwenye Tume ya uchaguzi tu baasi ili kuruhusu na wengine waweze kwenda Ikulu hata kama hakuna linalowakera.

Kuna kelele nyingine ndogo za serikali tatu, lakini wengi hatuoni namna gani serikali mbili zinavyosababisha umaskini, udini, ukabila, unyimaji haki au mgawanyo mbaya wa ardhi na maendeleo ya upendeleo.

Ndiyo maana watu wengi hawaitafuti katiba waijue kwasababu hawana tatizo na Katiba.

Katiba mpya sio kipaumbe kama ilivyo kwa matibabu, uchumi, maji, umeme, elimu na amani na utulivu.
 
Back
Top Bottom