Chadema uchaguzi wao wa ndani ni baada ya 2015 .Wamekosea kama walikuwa wanadhani wanaweza kupeta kirahisi .Hakuna Uchaguzi wafe tu huko waliko .
Katiba ikiwa chakachuzi ni fake hivyo hayo maoni yako ni bure kama katiba. yenyewe ni fake.Naunga MKONO HOJA! Nashauri chama (CDM)
- kifanye tathimini ya kina na kuona kama kuna uwezekano (KIKATIBA) kuahirisha uchanguzi HADI BAADA YA UCHAGUZI MKUU 2015.
- Pia CDM kifanye tathimini ya kutosha juu ya mazuri na mabaya ya kuwa na uchaguzi huo 2014
- Chama kifanye tathimini juu ya mazuri na mabaya ya kuwa na uchaguzi huo 2015
- Tathimini ikiwa CDM itajipanga kufanya uchaguzi wa ndani 2015 wakati huo huo uchaguzi Mkuu 2015 ukiahirishwa kwa mizengwe.
Hahahahhahahaha Matola acha kunivunja mbavu.
Mbona unamchokoza Mzee Bonafide Genuine.
Hahahahahahaha.
We ndenda kijiwe cha Yericko Nyerere cha Lebnan ukapate mpya za leo toka kwa Snake ze Master.
Hahahahahaha
Mkuu Gideon Jeremiah, haki wewe u miongoni mwa wachache mnaipenda Chadema kwa dhati!. Kuna wengi ambao ni wanachama, wapenzi na mashabiki wa Chadema ambao ni wapambe tuu!, hawana lolote wala hawaisaidii Chadema kwa kuiibia nyimba tuu za sifa na mapambio!, mapenzi ya kweli, yanaonyeshwa pale mtu unapoumia mpaka nafsini na moyoni, ukiona chama unachokitegemea kinafanya madudu!, Mwigamba ameibua madai mazito ya msingi, halafu viongozi wanakujsa humu na majibu ya ....(mepesi) halafu mijitu humu inawashangilia!.
Asante tena Gideon Jeremiah.
Pasco.
Mkuu Mwanaukweli, kila kipengele kinawekwa kwenye katiba for a reason!. Niliwauliuza Chadema what were the reasoms behindi kipengele hicho kuwekwa?.
Kipengele kikishawekwa, kinaweza kuondolewa kama zile sababu hazipo tena!, tena sio kinyemela!.
Tunaikomalia Chadema kwa sababu, kilikuwepo na reasons behind tunazijua!, na kilivanish into thin air with specific ill motives behind!.
CCM inaweza kufanya makosa ya kusema uongo hata mara100 na ikawa not a big deal!, lakini Chadema wakisema uongo hata mara moja tuu, its a big deal!, naamini sababu unazijua!.
Pasco.
Katiba ya Chadema inasema uchaguzi ni kila baada ya miaka 5!, miaka mitano inaisga 2014!, mamlala ya extention mwisho ni mwaka 1!, hivyo ni 2015, baada ya 2015 bila uchaguzi Chadema itakuwa ni illegal party!, piga ua galagaza uchaguzi ni lazima 2014 not beyond, tena tutahakikisha tunashinikiza this time mwenyekiti ni lazima awe Prof. Safari, Arfi or "the one and only best you have!".
Huku sio kuingilia mambo ya ndani ya Chadema, bali kufanya maamuzi fedha zetu zitumikaje?.
Pasco.
Kama kipengele hicho kilikuwepo na kikaondolewa, kwa nini uhoji sababu za kukiondoa wakati hukuhoji sababu za kukiweka? Na kama kuhoji kwa nini siyo vikaoni?
Walipafedha za kuiendesha Chadema!.mtashinikiza nyie kama akina nani?
FaizaFoxy, kwanza nikupe pole sana kwa 'kukerwa' na mabadiliko ya katiba Chadema.
Usiwe na wasiwasi, hauko peke yako katika kadhia hii, wengi sana kati ya wana-CCM wamekerwa sana na mabadiliko haya.
Hivyo cheer-up, you are not alone in the depth of sorrow..!! Si unajua tena 'kifo' cha wengi harusi...!!
Otherwise, mabadiliko ndio hayo, mkitaka yaondolewe, basi njooni Chadema muwe wanachama ili mpate haki ya kubadili katiba, vinginevyo, tuonane mwaka 2015 kwenye 'mtanange' wa uchaguzi mkuu..!!
Msalimie sana Ritz ingawa naona leo yuko 'mitini'...!!!
Katiba ikiwa chakachuzi ni fake hivyo hayo maoni yako ni bure kama katiba. yenyewe ni fake.
Ukweli unauma.we naon aunatafuta BAN kwa lazima. Ukishaandika mara moja inatosha. Sio kusambaza kila thread.
Wewe si mchumia tumbo huko. Ngoja siku wakikubadilikia kwa jina lako tu, ndiyo utakuja kuongea vizuri humu.Ukiangalia kwa makini kwa jicho la tatu utagundua madhaifu ya wanaccm kwenye masuala kadhaa ya msingi. 1. Wako radhi wakomae na matatizo ya chadema kuliko walivyo radhi kukomaa na matatizo ya chama chao. CHADEMA ilishatoa ufafanuzi wa swala la katiba, sisi wana CHADEMA wenyewe hatuna mashaka, wao wana mashaka zaidi na sisi kuliko wanavyopaswa kuwa na mashaka na mambo yao. 2. Hawawapendi viongozi wa juu wa CHADEMA hasa mwenyekiti na katibu ambao misimamo yao na utendaji wao umesaidia sana kuikuza CHADEMA. Hawataki kujifunza ili wakinusuru chama chao juu ya kauli za mwenyekiti wao za kuacha rushwa maana kinaenda kufa, hawataki kuumiza kichwa juu ya tuhuma za katibu wao kuhusishwa na ujangili na yeye kukiri. 3. Ccm wana aina ya viongozi ambao wao ndio wana mahaba nao walioko CHADEMA na wanataka wawe kwenye uongozi wa juu wa CHADEMA kuliko viongozi wengine. Sarakasi za upotoshi wa katiba ni kuwatetea watu wao. Ccm hao hao hawana muda kudeal na matatizo ya kiuongozi ndani ya chama chao. Uongozi ndani ya ccm unapatikana kwa mafurushi ya fedha. Hawana muda na hilo ila wana muda na uongozi utakavyo patikana CHADEMA. Mengine yanasikitisha zaidi... Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Hivi neno Chadema liko kwenye ilani ya uchguzi ya CCM? Hivi ni kwa nini CCM hawatekelezi ilani yao ya uchaguzi baadala yake wambaki kuparamia Chadema?