Katiba ya CCM haina suala la Ukomo wa muda wa uongozi.

Katiba ya CCM haina suala la Ukomo wa muda wa uongozi.

Kuna vikao halali vinavyoruhisiwa kubadili katika lakini siyo kinyemela tunamuachia msajili afanye kazi yake.

una umiza kichwa bureee wameshakwambia tofauti ya2004 na2006
....vikao wanakaa wao wewe na mimi hatupo..waachieni lichama lao mbona husikiii.....
wewe kenya uganda na rwanda wameshaamua wanafanya mikutano yao pekee yao ...sisi tz tunaanza maneno inasaidia nini wakati wameshajitenga wanaendelea na mambo yao
 
Ni katiba ya ajabu muundo wake uko hivi:
-Mtei (mchagga) hakuna ukomo wa M/kiti
-Makani (msukuma) M/kiti vipindi viwili
-Mbowe (mchaga) hakuna ukomo wa M/kiti

Yaani mwenyekiti akiwa mchagga hakuna ukomo ila akiwa kabila nyingine ukomo upo?

 
Ukiangalia kwa makini kwa jicho la tatu utagundua madhaifu ya wanaccm kwenye masuala kadhaa ya msingi.

1. Wako radhi wakomae na matatizo ya chadema kuliko walivyo radhi kukomaa na matatizo ya chama chao. CHADEMA ilishatoa ufafanuzi wa swala la katiba, sisi wana CHADEMA wenyewe hatuna mashaka, wao wana mashaka zaidi na sisi kuliko wanavyopaswa kuwa na mashaka na mambo yao.

2. Hawawapendi viongozi wa juu wa CHADEMA hasa mwenyekiti na katibu ambao misimamo yao na utendaji wao umesaidia sana kuikuza CHADEMA. Hawataki kujifunza ili wakinusuru chama chao juu ya kauli za mwenyekiti wao za kuacha rushwa maana kinaenda kufa, hawataki kuumiza kichwa juu ya tuhuma za katibu wao kuhusishwa na ujangili na yeye kukiri.

3. Ccm wana aina ya viongozi ambao wao ndio wana mahaba nao walioko CHADEMA na wanataka wawe kwenye uongozi wa juu wa CHADEMA kuliko viongozi wengine. Sarakasi za upotoshi wa katiba ni kuwatetea watu wao. Ccm hao hao hawana muda kudeal na matatizo ya kiuongozi ndani ya chama chao. Uongozi ndani ya ccm unapatikana kwa mafurushi ya fedha. Hawana muda na hilo ila wana muda na uongozi utakavyo patikana CHADEMA.

Mengine yanasikitisha zaidi...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
una umiza kichwa bureee wameshakwambia tofauti ya2004 na2006
....vikao wanakaa wao wewe na mimi hatupo..waachieni lichama lao mbona husikiii.....
wewe kenya uganda na rwanda wameshaamua wanafanya mikutano yao pekee yao ...sisi tz tunaanza maneno inasaidia nini wakati wameshajitenga wanaendelea na mambo yao
Wewe na Mwigamba nani alikuwa na nafasi nzuri ya kujua? Mwigamba amesema kuna uchakachuaji.
 
Wewe na Mwigamba nani alikuwa na nafasi nzuri ya kujua? Mwigamba amesema kuna uchakachuaji.

we mwehu mimi na wewe tumsaidie mwigamba asipigwe tena awaachie lichama lao ya nini kungangania
 
Ukiangalia kwa makini kwa jicho la tatu utagundua madhaifu ya wanaccm kwenye masuala kadhaa ya msingi.

1. Wako radhi wakomae na matatizo ya chadema kuliko walivyo radhi kukomaa na matatizo ya chama chao.
Mengine yanasikitisha zaidi...

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Ahsante kwa ukiri Chadema ina matatizo.

 
we mwehu mimi na wewe tumsaidie mwigamba asipigwe tena awaachie lichama lao ya nini kungangania
Asipopigwa Mwigamba watapigwa wengine maana wana madai ya msingi lazima wayaseme.

 
Ni katiba ya ajabu muundo wake uko hivi:
-Mtei (mchagga) hakuna ukomo wa M/kiti
-Makani (msukuma) M/kiti vipindi viwili
-Mbowe (mchaga) hakuna ukomo wa M/kiti


Mtajaribu sana kupandikiza ukabila, haitasaidia...!!
Mtajaribu sana na mengine mwngi, haitasaidia...!!

Katiba ya CCM haina ukomo wa uongozi, huko nako kuna 'ukabila'..??
Poleni sana wana-CCM, Chadema inawasumbua sana.
 
Asante sana Mwanaukweli,angalau umerudisha kumbukumbu, operation chaos!!
Tuwe imara kwa viongozi wetu wenyewe wasije wakakata tamaa,kumbe walijua Mbowe amesurrender kumbe changa la macho.Wanataka kutulazimishia Zitto,sisi hatumtaki( hata kama kaaga kigoma)
 
Katiba ya CCM haina kipengele chochote kinachoweka ukomo wa muda wa mtu kuwa katika uongozi.

attachment.php


Na katika sehemu inayotaja mwenyekiti wa taifa hakuna ukomo.

attachment.php


attachment.php


Kwa kuwa suala la kukosa ukomo katika uongozi katika katiba ya Chadema limeonekana kuwakera sana wapenzi wa CCM na mahasimu wa CHADEMA, kuliko wanachama wa CHADEMA wenyewe.

Je, agenda hiyo imeanzishwa kwa nia njema?

Mmewahi kuona hata siku moja Zemarcopolo, ritz, simiyu yetu, chris lukosi, faizafoxy, chabruma, wakionyesha nia njema yoyote kwa CHADEMA?

Tuchukulie kuwa wamefanya kwa nia nzuri, je kwa nini nia hio njema isiwatume kuhoji katiba ya chama chao wenyewe?

Wana Chadema mnaosoma thread hii, mjue CCM wanatumia kila mbinu kubomoa Chadema. Na inaonekana wanaona uongozi wa sasa wa chadema umekuwa kikwazo kwao kuona upinzani unazorota.

Walijaribu mbinu nyingi za propaganda: kaskazini, ukristu, ukatoliki, ugaidi, kumchafua Slaa, n.k. na zote hizo zikashindwa.

Wana chadema mjue kuwa hii pia ni mbinu nyingine, na kwa hiyo kipindi hiki kinahitaji mshikamano zaidi.

People's --------------------

Usitafute pakutokea, huna. Labda wadanganye misukule, wenye nazo timamu huwezi kuwababaisha kijinga.

Kwa hili naona hata misukule watakucheka. Hebu jisomee mtiririko wa suala la katiba ya chadema na uwache unazi usio na mpango:

HATARIIII SANA,IMEFAHAMIKA DR.SLAA NA TIMU YAKE WAMECHAKACHUA KATIBA YA CHADEMA,AIBU SANAAA

Wana JF,
Kwa siku za karibuni, umezuka mjadala mkali ndani ya mtandao huu pendwa hasa baada ya Samson Mwigamba ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha kuwatuhumu viongozi wa kitaifa wa CHADEMA kuwa wamebadilisha katiba kinyemela kwa kuondoa ukomo wa uongozi wa awamu mbili ili waendelee kubaki madarakani. Mwigamba ametoa shutuma hizo akitumia jina bandia la Maskini Mkulima. Katika shutuma zake Mwigamba amesema yafuatayo;
Wakati tukifanya mabadiliko ya katiba mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitanomitano. Lakini wakati katiba inachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa nayenye athari zisizomithirika kwa chama.

Ni muhimu wanachadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe na Zitto kupigania uenyekiti. Kama kingekuwepoleo Mbowe alikuwa anakatazwa na katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wanachadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.



Mara baada ya taarifa hiyo ambayo ilibebwa kwa jina la Wito kwa wana CHADEMA wote! ambayo ilieleza madhaifu ya chama na kubadilishwa kwa vipengele vya katiba kinyemela, Dr Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA alitoa ufafanuzi ufuatao;
WanaJF,
Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

Hata hivyo, majibu hayo ya Dr Slaa yanaonekana kutofautiana na yale ya JOHN MNYIKA aliposema kuwa kwenye katiba ya 2004 kipengele cha ukomo wa uongozi kiliwekwa lakini hakikuingizwa kwenye katiba ya 2006. John Mnyika anasema;

Kuhusu Katiba, nina nakala mango (hard copy) tu ya katiba ya 2004, ilikuwa na kipengele cha vipindi viwili vya nafasi ile ile. Hata hivyo, katiba mpya iliyoandikwa mwaka 2006 haikuwa na kipengele hicho. Hivyo, sio kwamba kimeondolewa kinyemela ila hakikuwepo kwenye katiba mpya. JJ

Baada ya malumbano hayo, nilifanya utafiti mdogo ili kujiridhisha na hoja zilizotolewa na viongozi hao. kwa msaada mkubwa kutoka kwa wadau muhimu ndani ya CHADEMA, nimefanikiwa kupata nyaraka zifuatazo



  1. Nakala ya Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2004 iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza
  2. Nakala ya Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 iliyoandikwa kwa lugha ya kiswahili
  3. Muhtasari wa Mkutano Mkuu Maalum wa CHADEMA uliofanyika katika ukumbi wa PTA Dar es Salaam tarehe 13, Agosti 2006


Nitajaribu kuweka vipengele muhimu mahsusi kwa mjadala huu. Nitajikita kwenye hoja moja tu ya Mwigamba kuwa Viongozi wamefanya marekebisho ya katiba kinyemela kwa kuondoa ukomo wa madaraka ili waendelee kuwepo madarakani.
Katiba ya mwaka 2004 ipo wazi kabisa katika hoja ya ukomo wa madaraka. Ibara ya 6.3.2 kipengele cha (c) kinasema ifuatavyo; ''Leaders who finish their term of office can be eligible for re-election provided he qualifies but no leader can hold the same post at the same level of the party structure for more than two terms. Kutokana na kipengele hiki, kauli ya Dr Slaa kuwa hakuna katiba ya CHADEMA iliyoweka ukomo wa madaraka ni ya kushangaza ikizingatiwa kuwa yeye ni Katibu Mkuu na hakupaswa kusema uongo mbele ya watu ambao wanaelewa mengi kuhusu katiba hizo.
Katika Mkutano Mkuu Maalum wa mwaka 2006 ambao ulikuwa na ajenda 4 ambazo ni;



  1. Kufungua Mkutano
  2. Maboresho ya Katiba
  3. Maazimio juu ya Katiba Mpya na
  4. Kufunga Kikao


ulijadili vifungu 10 ambavyo vimefanyiwa marekebisho kutoka kwenye katiba ya 2004. Kati ya vipengele hivyo, kipengele cha ukomo wa madaraka hakimo na hii ni kusema kuwa hoja hiyo haikuwa na marekebisho. Vipengele vilivyofanyiwa marekebisho kwa mujibu wa muhtasari huo vimeambatishwa na taarifa hii.
Katiba ya Mwaka 2006 ndiyo inayolalamikiwa kuchakachuliwa kwa vile kipengele cha ukomo wa madaraka hakimo na hakuna mkutano uliojadili hoja hiyo. Kutokana na hali hiyo, ni wazi kuwa hoja za Samson Mwigamba ni sahihi na viongozi wa CHADEMA hususan DR WILBROAD SLAA NA JOHN MNYIKA wametoa majibu ya uongo kupinga hoja za kweli. kwa mantiki hiyo, ni wazi kuwa katiba imechakachuliwa kwa maslahi ya wanaotetea uchakachuaji huo.
Nawasilisha.

Chanzo: HABARI KWANZA: HATARIIII SANA,IMEFAHAMIKA DR.SLAA NA TIMU YAKE WAMECHAKACHUA KATIBA YA CHADEMA,AIBU SANAAA

Huu utafiti ni wa Chabruma.
 
Last edited by a moderator:
Usitafute pakutokea, huna. Labda wadanganye misukule, wenye nazo timamu huwezi kuwababaisha kijinga.

Kwa hili naona hata misukule watakucheka. Hebu jisomee mtiririko wa suala la katiba ya chadema na uwache unazi usio na mpango:



Huu utafiti ni wa Chabruma.
Kwa hiyo wewe una uchungu na Chadema? Kwa hiyo wewe unataka Chadema iimarike?

Niambie nia ya wana CCM kushupalia hili ni nini? Kwa nini tunayepambana naye ndie atuchakulie kamanda?
 
Usitafute pakutokea, huna. Labda wadanganye misukule, wenye nazo timamu huwezi kuwababaisha kijinga.

Kwa hili naona hata misukule watakucheka. Hebu jisomee mtiririko wa suala la katiba ya chadema na uwache unazi usio na mpango:

Huu utafiti ni wa Chabruma.

FaizaFoxy, kwanza nikupe pole sana kwa 'kukerwa' na mabadiliko ya katiba Chadema.
Usiwe na wasiwasi, hauko peke yako katika kadhia hii, wengi sana kati ya wana-CCM wamekerwa sana na mabadiliko haya.

Hivyo cheer-up, you are not alone in the depth of sorrow..!! Si unajua tena 'kifo' cha wengi harusi...!!
Otherwise, mabadiliko ndio hayo, mkitaka yaondolewe, basi njooni Chadema muwe wanachama ili mpate haki ya kubadili katiba, vinginevyo, tuonane mwaka 2015 kwenye 'mtanange' wa uchaguzi mkuu..!!
Msalimie sana Ritz ingawa naona leo yuko 'mitini'...!!!
 
Tatizo katiba ya chadema imechakachuliwa kuwa hakuna ukomo wa muda wa mwenyekiti bila ya vikao halali. Umeona tofauti yake hapo?


kwa hiyo mmeo akiwa hakuridhishi unatoka nje na kuanza kupiga yowe au mnamalizana wenyewe!kwanini jirani ndiyo aje kumfundisha jinsi ya kukuridhisha,nahisi umeelewa,mimi ni mfuasi wa Chadema sjaona tatizo liko wapi!na kama lipo nitanyoosha mkono kwenye vikao vya chama na kuhoji,kushauri au kupendekeza,sio mCcm ndiyo ahoji,kama wanaona ni kizuri kipengele hicho wakiweke kwao kwanza,au tuamini kuwa ni uoga wao kwa vichwa vilivyopo(Mbowe,Dr.SLaa),kama umemuelewa mleta mada amekuwekea hadi andishi la W.Malecela hapa kwamba waongeze mashambulizi ili wahakikishe Mbowe na Slaa hawagombei tena,kumbe tatizo kwa maCcm siyo kuchakachua katiba,ni Mbowe na Dr.Slaa kama kawaida yao.
 
You are missing the point dude!

Tatizo sio kuwepo au kutokuwepo kwa kipengele.

Tatizo ni utaratibu unaotumika kuingiza na kutoa vipengele pamoja na kauli za UONGO zinazotolewa na viongozi waandamizi wa chama kulaghai watu juu ya utaratibu huo.

wewe CDM inakuhusu nini?
Wana-CDM wenyewe hawalalamiki mnapiga kelele nyinyi!
Au mbebadili sera za chama chenu na kuingiza hii ya kuilalamikia CDM ili muonekane mnafanya kazi mbele ya WaTZ?
Kazi yenu nynyi ni kutimiza sera zenu kwa WaTZ sio vinginevyo!
Tunataka elimu bora, muondoe ufisadi, kamateni wauza sembe, mrudishe ela zilizofichwa Uswis, ela za EPA, afay bora, maisha bora kwa kila Mtz.
Kuhujumu CDM haiwasaidii kitu, mnapoteza mda wenu bure ambao mgewatumikia WaTZ!
Au mnafikiri mkifanya hivyo ndio mtapigiwa kura au mtakubalika tena? No way!
Ondoeni udhaifu wote mlioshikilia ambao unalalamikiwa na WaTZ.
Kitendo cha kuhangaika na CDM na in my point of view kinawaondolea sifa zote za kuwa watawala!
Kinaonyesha jinsi mlivyo wavivu na humuwezi ushindani wa dunia ya leo!
Chama chenu ndio kinakusanya kodi yangu inayoendesha serikali hii! badala ya kuniletea maendeleo na kuniondolea matatizo nyinyi mko busy kuhangaika na CDM! Hiyo indio kazi mliyotumwa na WaTZ au mliowahaidi WaTZ?
Jitazameni njia mnayokwenda sio nzuri na haiwasaidii kabisa!
 
Yaani mwenyekiti akiwa mchagga hakuna ukomo ila akiwa kabila nyingine ukomo upo?

Husichanganye madafu tunaongelea CCM, na swali ni kwanini katiba ya CCM haina ukomo wa uongozi??
 
Usitafute pakutokea, huna. Labda wadanganye misukule, wenye nazo timamu huwezi kuwababaisha kijinga.

Kwa hili naona hata misukule watakucheka. Hebu jisomee mtiririko wa suala la katiba ya chadema na uwache unazi usio na mpango:



Huu utafiti ni wa Chabruma.

Msitujazie server.. tunaongelea CCM sio Chadema.. Na swali ni kuwa tangu CCm ilipozaliwa (1977 kama sikosei mpaka ) 2013) kwa nini hiki chama chetu kipendwa hakina ukomo wa madaraka? Nilitegemea chama kikomavu kama CCM kiwe ni mfano wa vyama vichanga. swali ni hilo tu.
 
Asipopigwa Mwigamba watapigwa wengine maana wana madai ya msingi lazima wayaseme.


Umelewe swali lakini? ni kuhusu CCM kutokuwa na ukomo wa madaraka na swali ni kwanini? hayo ya Mwigamba waache wafu wazikane sisi tuongelee juu ya chama chetu kipendwa!
 

Mkuu Mwanaukweli, kila kipengele kinawekwa kwenye katiba for a reason!. Niliwauliuza Chadema what were the reasoms behindi kipengele hicho kuwekwa?.

Kipengele kikishawekwa, kinaweza kuondolewa kama zile sababu hazipo tena!, tena sio kinyemela!.

Tunaikomalia Chadema kwa sababu, kilikuwepo na reasons behind tunazijua!, na kilivanish into thin air with specific ill motives behind!.

CCM inaweza kufanya makosa ya kusema uongo hata mara100 na ikawa not a big deal!, lakini Chadema wakisema uongo hata mara moja tuu, its a big deal!, naamini sababu unazijua!.

Pasco.
Pasco usi -justify. Kama nia yako ni uchaguzi CDM huo haupo!! tutafanya 2015 tukimaliza uchaguzi mkuu - pole kama ulikuwa unautaka uwenyekiti.

Ndege ina-takeoff sasa - hatuwezi kubadilisha wana-anga!!!
 
Usitafute pakutokea, huna. Labda wadanganye misukule, wenye nazo timamu huwezi kuwababaisha kijinga.

Kwa hili naona hata misukule watakucheka. Hebu jisomee mtiririko wa suala la katiba ya chadema na uwache unazi usio na mpango:



Huu utafiti ni wa Chabruma.
Umepiga ngumi kwenye 'pressure point'. Misukule imeona imeingia mitini.
 
Back
Top Bottom