Kwa hiyo mnalenu jambo nyuma yake mnataka CHADEMA ife sio?
Hakuna Mtanzania mwenye kuitakia mema nchi hii kwa dhati, anayetaka Chadema ife!.
Mzazi anayejali, humcharaza bakora mwanaye anayempenda ili kumrudi asipotee!.
Tunachokifanya akina sisi, tena kwa nia njema na dhamira safi, ni kuitembezea Chadema bakora za nguvu, na kuipitisha kwenye tanuru la moja, kama haijakomaa, acha uingulie humo na kugeuka majivu!, lakini kama imekomaa, itaibuka ikiwa ni chuma cha pua!.
Baada ya miaka 50 ya utuymwa wa CCM, 2015 hatuhitaji kubahatisha!, we need to be definite sure kuhusu capabilities za Chadema!. Better be sure than sorry!, ndio maana Chadema unapofanya madudu, sisi wengine hatuna huruma hata kidogo, ni bakora kwa kwenda mbele!, hata hao tuwatumainia kwa kuwadhania ndio watatuvusha, lazima wapimwe kwa mkono wa chuma!, na sio kubembelezana kwa kupeana pipi na lawalawa za nyimbo za shangwe na mapambio!, they need to be tasked, tested and approved ndipo tuwape!.
Nasisitiza tena tena tena, ni wale wenye uono finyu tuu ndio wanaoamini kuwa watakao inngiza Chadema ikulu ile 2015 ni wanachama, wafuasi na wapenzi wa Chadema tuu, sisi wengine wote tunao i task, hatuitakii mema!. They are wrong!. Watakao iingiza Chadema ikulu hiyo 2015 (if at all!), ni sisi!, (yes ofcourse pamoja na nyinyi!).
Pasco.