OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo amesema aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alifanya kazi kubwa wakati akiwa Mkuu wa mkoa ya kujenga Ofisi za Chama hicho Kinondoni na Kigamboni.
“Ni lazima tutambue kuwa aliyekuwa Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es salaam (Paul Makonda) alifanya kazi kubwa sana, tusiwe wanafiki, mnajua na ni lazima tuseme, yeye ndiye alianzisha ujenzi wa Ofisi hizi za Chama hapa Kigamboni na alifanya na Kinondoni, lazima tumpongeze” Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM
My Take
Katibu mbona umemzungumzia upande mmoja tu. Waambie watu na upande mwingine, kama huna habari kazipate GSM, Clouds Media au kwa Kubenea. Hata wewe pia nimekuwekea video hapo juu jinsi ulivyoonja jeuri ya huyu kijana