Katibu Mkuu CCM ampiga dodoki Paul Makonda

Katibu Mkuu CCM ampiga dodoki Paul Makonda

Ujenzi wa ofisi za chama siyo kazi ya RC. Hii inaonesha jinsi utawala ulivyopita ambavyo ulikuwa haufuati sheria wala miongozo ya kazi.
Makonda alikuwa jambazi mwenye mamlaka, hayo majengo walikuwa wanajenga GSM na wafanyabiashara wengine kwa kumuogopa Makonda.

Wengi hawana kumbukumbu jengo la makao makuu ya Bakwata ni huyohuyo Makonda kawakaba matajili fulani wajenge makao makuu ya Bakwata ni jengo la ghorofa kadhaa ila sijui utekelezaji wake ukoje.

Kama tungekuwa na viongozi wa dini makini wenye hofu ya Mungu wasingekubali huu ufadhili wa Makonda taasisi ya dini kupokea ufadhili kwa pesa ambayo ni haram anakwenda kuporwa kinguvu mtu mwingine.
 
Huko kwenye chama utendaji wake tunawaachia ninyi wenyewe...

Ishu ipo kwenye utendaji wake kwenye masuala ya umma na namna alivyoishi na wananchi...
Angekubalika kwenye chama kwenye zile kura za maoni angeshinda kwa kishindo.

Maana Tanzania nzima hakuna mgombea yeyote aliyefikia kiwango cha rushwa aliyotowa Makonda, alihonga makatibu wote kwenye jimbo pikipiki moja na million moja kibindoni na wapiga kura waliobaki walilamba laki tano kila mpiga kura, lakini watu walimpa kura za huruma Ndugulile.

Kwa nguvu aliyotumia Makonda kwenye kura za maoni hakuna mtu yeyote yule unaweza kushindana naye zaidi ya upendo tu wa wapiga kura walimpania Makonda na wakampa Ndugulile kura za huruma huku mwili wa baba yake ukiwa monchwari haujazikwa bado.
 
Sasa wakuu wa mikoa wataanza shindana jenga majengo
 
Katiba ipi?

Kwa hiyo Sendiga RC wa Iringa na mwenyekiti wa chama cha ADC ni mjumbe pia katika kamati ya CCM?
Kikatiba....

Mkuu wa mkoa ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM mkoa.....

#Siempre JMT[emoji120]
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amesema aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alifanya kazi kubwa wakati akiwa Mkuu wa Mkoa ya kujenga Ofisi za Chama hicho Kinondoni na Kigamboni.

“Ni lazima tutambue kuwa aliyekuwa Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam (Paul Makonda) alifanya kazi kubwa sana, tusiwe wanafiki, mnajua na ni lazima tuseme, yeye ndiye alianzisha ujenzi wa Ofisi hizi za Chama hapa Kigamboni na alifanya na Kinondoni, lazima tumpongeze,” anasema Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM.

8888888888888

Baada ya kuona hiki alichokifanya Chongolo na tukumbuke kuwa kwenye matukio ya kisiasa huwa hakuna kitu cha bahati mbaya, imekaaje hii wadau? Makonda anarudishwa kwenye system au Makonda bado ana nguvu kwenye system?
 
Aisee.
Screenshot_20220416-004347.jpg
 
View attachment 2195996
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo amesema aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alifanya kazi kubwa wakati akiwa Mkuu wa mkoa ya kujenga Ofisi za Chama hicho Kinondoni na Kigamboni.

“Ni lazima tutambue kuwa aliyekuwa Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es salaam (Paul Makonda) alifanya kazi kubwa sana, tusiwe wanafiki, mnajua na ni lazima tuseme, yeye ndiye alianzisha ujenzi wa Ofisi hizi za Chama hapa Kigamboni na alifanya na Kinondoni, lazima tumpongeze” ——— Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM

My Take
Katibu mbona umemzungumzia upande mmoja tu. Waambie watu na upande mwingine, kama huna habari kazipate GSM, Clouds Media au kwa Kubenea. Hata wewe pia nimekuwekea video hapo juu jinsi ulivyoonja jeuri ya huyu kijana
Katibu mkuu kaka yangu Chongolo, hata haya yasemwe pia
1650295306129.jpg
1650526286254.jpg
1647583947557.jpg
 
Ufikiri wa kipumbavu, na haya ndio matokeo ya elimu ya kipumbavu tunayopewa, hayo yote uliyoyasema yanaamuliwa na mahakama za kisheria, nitajie hata kesi moja ya drug iliyokwenda mahakamani?au maintenance court?,ule ulikua udikiteta uchwara, nchi inahitaji strong &independent institutions!
Ok! Kwa mtazamo wako iko hivyo! Hivi kweli unafikiri taasisi imara na zinazojitegemea zitatokana na mifumo na tawala zilizopo? Huyu alitumia udikteta maana alijua watu walijengewa tabia ya rushwa! Kumbuka anayeuza unga ni bilionea , kupoteza ushahidi ni rahisi mno!
Hata Amerika inasumbuliwa na wauza unga pamoja na taasisi zao imara!
Uasitukane! Jadili!
 
View attachment 2195996
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo amesema aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alifanya kazi kubwa wakati akiwa Mkuu wa mkoa ya kujenga Ofisi za Chama hicho Kinondoni na Kigamboni.

“Ni lazima tutambue kuwa aliyekuwa Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es salaam (Paul Makonda) alifanya kazi kubwa sana, tusiwe wanafiki, mnajua na ni lazima tuseme, yeye ndiye alianzisha ujenzi wa Ofisi hizi za Chama hapa Kigamboni na alifanya na Kinondoni, lazima tumpongeze” ——— Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM

My Take
Katibu mbona umemzungumzia upande mmoja tu. Waambie watu na upande mwingine, kama huna habari kazipate GSM, Clouds Media au kwa Kubenea. Hata wewe pia nimekuwekea video hapo juu jinsi ulivyoonja jeuri ya huyu kijana
Sio hivyo,ukiona Katibu Mkuu anamsifia Makonda ujue ni changa la macho.
Ili siku akizama,wasimhusishe na hilo,ametengeneza cast iron alibi.
 
View attachment 2195996
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo amesema aliyekua Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alifanya kazi kubwa wakati akiwa Mkuu wa mkoa ya kujenga Ofisi za Chama hicho Kinondoni na Kigamboni.

“Ni lazima tutambue kuwa aliyekuwa Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es salaam (Paul Makonda) alifanya kazi kubwa sana, tusiwe wanafiki, mnajua na ni lazima tuseme, yeye ndiye alianzisha ujenzi wa Ofisi hizi za Chama hapa Kigamboni na alifanya na Kinondoni, lazima tumpongeze” ——— Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM

My Take
Katibu mbona umemzungumzia upande mmoja tu. Waambie watu na upande mwingine, kama huna habari kazipate GSM, Clouds Media au kwa Kubenea. Hata wewe pia nimekuwekea video hapo juu jinsi ulivyoonja jeuri ya huyu kijana
Kauli kama hii nawaambia tegemeeni breaking newzz kumhusu Makonda.

Demotion au promotion.

Tumeshaandaliwa kisaikolojia
 
Back
Top Bottom