Katibu Mkuu wa CCM anaijua katiba ya nchi?
Katiba inawapa haki wananchi kuchagua na kuchaguliwa katika uongozi.
Katibu anatoa kauli hizi kwa ujinga tu, kwamba haijui katiba?
Au anatoa kauli hizi kwa ushenzi tu, kwa kutoiheshimu hiyo katiba?
Huyu mtu ana Ph.D ya Political Science, sidhani kwamba haijui katiba ya nchi.
Inaonekana haiheshimu tu.
Kama watu 12 ni wengi sana, idadi sahihi ni watu wangapi? 10? 5? 1?
Kwa nini?
Na hao wengine watakaokosa nafasi ya kugombea, haki yao ya kikatiba tutasema bado wanayo?