Zanzibar 2020 Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru ashangaa watu 12 kujitokeza kutaka urais Zanzibar, adai wengine wanatumika na mabeberu kutaka kuvuruga nchi yetu

Naombeni mnielemishe tofauti ya Beberu na Mhisani!
 
Huyu Bashiru ni Professor wa ajabu sana, huo si ndivyo mchakato ulivyo. Wakati wa Awamu ya nne katika mchakato aliopatikana Magufuli, waliochukua fomu walikuwa wengi, hatukumsikia KINANA akipiga kelele au akilalamika, walizipokea fomu zote na kuzipeleka kwenye kikao. Au hiyo ni kutaka kuhakikisha hawapokei fomu za wagombea bara zaidi ya fomu ya Magufuli.
 
Kwani wamekiuka katiba?
 

Kama kuna kipindi atachanganyikiwa basi ni hiki,atapata moto kuliko kipindi cha hapa nyuma alipokuwa akitishia kujiuzulu. Aendelee kushangaa hivyo hivyo sababu ya CCM ye hayajui kwani ni lini yeye aliwahi kuwa mwanaCCM?

Kilichokuwa kinaiokoa CCM miaka yote ni kuwepo kwa miamba mikubwa mingi ambapo hata wavutane kiasi gani kipindi cha mvutano kikipita wanarudi mezani kuunga juhudi, lakini sio kwa upuuzi ambao umekuwa ukiendelea tangu 2015, watu wamenyang’anywa uwezo wamekaa kimya mioyo ikifukuta, ngoja tuone itakuwaje!
 
Na sasa mwenyekiti kasema inategemea siku hiyo ameamkaje
 
Duh je amesahau kuwa mwaka 2015 walijitokeza wagombea 38 upande wa bara ??
 
Jecha amewavuruga ccm hata hawajui wanachoongea, hawaamin wanachokiona
 

Hii ina make sense.
 
Kwani yeye alitaka nani pekee achukue? Kama wana mtu wao wangeharibu printer kama huku bara.
 
Kumbe ndiyo maana ametengeneza form moja tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…