Zanzibar 2020 Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru ashangaa watu 12 kujitokeza kutaka urais Zanzibar, adai wengine wanatumika na mabeberu kutaka kuvuruga nchi yetu

Zanzibar 2020 Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru ashangaa watu 12 kujitokeza kutaka urais Zanzibar, adai wengine wanatumika na mabeberu kutaka kuvuruga nchi yetu

Huyu ana akili mbovu sasa! Anasahau kama wange limit wachukua fomu 2015, na Rais Magufuli asingelikuwa Rais leo maana hakuwa wa kwanza kuchukua fomu! Hakuwa wa kwanza wala wa pili, wa tatu hata wa tano!
Katibu mkuu wa CCM ashangaa watu ama wanachama 12 kujitokeza ndani ya CCM kuutaka urais.

Anashangaa nafasi ni 1 ya urais watu 12 wanatafta nini? Awatuhumu wengine kua wanatumwa na mabeberu kuvuruga chama na kuleta mvurugano nchini.

Anasema hao wanachama wa CCM 12 wanaoutaka urais wanataka kuvunja umoja wa Chama cha Mapinduzi.

Msikilize hapa.


u
 
Zanzibar CCM wampe Jecha. Huyu kaitendea haki CCM kuliko jiwe, kuliko Bashiru, kuliko Shein, name yeyote.

Jecha oyeee! Uliwatendea yote, ni muda wao sasa kukulipa fadhila zako kwao.
 
Wamesha sahau
Huyu ana akili mbovu sasa! Anasahau kama wange limit wachukua fomu 2015, na Rais Magufuli asingelikuwa Rais leo maana hakuwa wa kwanza kuchukua fomu! Hakuwa wa kwanza wala wa pili, wa tatu hata wa tano!

u
 
Hadi sasa wameshafikia 23
Jina ni langu, kama umelipenda kamrithishe mwanao. Nilichodanganya ni kipi? Huo ukweli unaoujua wewe ni upi?
Angalia hiyo video hapo chini ya Dr. Bashiru akiwa ziarani Zanzibar mwaka jana, na angalia ilikuwa uploaded lini kwenye youtube.

 
Wekeni akili sawa,chaguo la wana ASP ni Ali karume.Ali Karume hana mpinzani.
 
Beberu jeusi ni hatari kuliko beberu mzungu!Sasa kama katiba ya nchi pamoja na katiba ya chama zinaruhusu watu kuchukua form kadri wawezavyo,wakifanya hivyo kuna ubaya gani?!
 
Kwani tatizo liko wapi? Hata wakijitokeza 200 si ndo demokrasia hiyo...? Huyu dokta vepeee? Vinginevyo wangeweka limit kwamba mwisho ni watu 5 ingeeleweka.

Halafu hii kasumba ya kuita watu mabeberu au wanatumwa na mabeberu sijui kwa nini imeshika kasi awamu hii namna hii
 
Very foolish statement, has he seized from being a political scientist? Has he forgotten his vuvuzela times?
 
Mzee Jecha SHIKAMOO popote ulipo Baba harakati zako kuanzia vijana adi wazee wanakutambua na umetia kishindo tena...Nani kama Jechaaaaa...
 
Sasa kwani Bashiru alitaka wangapi wachukue form? pia anasema wanatumiwa na mabeberu ,mbona anapokea ada zao za uanachama kila mwakaa? kumbe michango ruksa kupokea ila wakigombea nafasi za uongozi ubeberu unaonekana?

Lakini si ana mamalaka afanye mchakato wa kuondoa wanachama wote wanao tumiwa na mabeberu mapema asisubiri wachukue form ndio aanze vimameno maneno Dkt vipi?
 
Kwa nafasi yake ya ukatibu mkuu, yeye ni mtendaji mkuu wa chama, kwa hiyo alikuwa anajua kila kilichokua kinaendelea ndani ya chama hasa kwa hao waliokuwa wanajipitisha pitisha kabla ya wakati kwa mujibu wa CCM kuutaka urais wa Zanzibar. Lakini, for your information, mpaka leo hii jumatatu, waliokwishachukua form za kuomba uteuzi wa kugombea urais wa Zanzibar kupitia CCM wameshafika 14, imezidi hiyo idadi aliyokuwa ameisema Dr. Bashiru.
Kwahiyo he was wrong, kama alipata taarifa then his source was wrong too.

Kwani ni dhambi wagombea wengi kuchukua form ?

Haoni kuwa sampling itakuwa nzuri zaid na hivyo kuwa na chance ya kupata kiongozi bora.

Bashiru asiendeshe chama kama familia yake
 
Hadi Jecha mazee..... Dah!!??
Jecha aliamrishwa na mkapa afute matokeo hakuwa ridhaa yake,Sasa naye anautaka huo uraisi akikatwa anatoboa siri na kuleta migongano namakundi, Act wata shinda kiulaini
 
  • Thanks
Reactions: rr4
Back
Top Bottom