Katibu mkuu CWT agoma kurudi Temeke kufundisha

Wameamua kumkomalia kisa kukataa teuzi,sio kila mtu ni mtumwa wa teuzi,waache ushamba.

Ungechunguza kujua sababu ya kugomea uteuzi ungegundua kumbe naye ni Ng'ombe tu sio kichwa kama unavyodhani.

Sababu ni hiyo nafasi aliyokuwepo kwa muda anaingiza okoto la uhakika zaidi kuliko kwenye UDC alikotakiwa kwenda,uliza mwalimu yeyote.
 
Unaweza ukafanya ujinga mdogo kwenye maisha na ukakukomoa!

Maisha ya Bongo ni unafki ili uendelee
Hili ni tatizo kubwa na athari zake zinakwenda mbali sana. Maisha ya aina hii hayatoi genuine competition au ku-reward watu kulingana na uchapakazi wao badala yake wanafiki, walaghai na waongo ndiyo wanapendwa na watawala na kuwa rewarded handsomely.
 
Huyo inatakiwa wasiishie hapo, awe mfano kwa wengine wenye tabia kama zake.
Ni mpuuzi, anadhani kama alikua na ubabe wake kwa waliokua chini yake ndio utafanya kazi kila sehemu??

Kwa namna yoyote hii game haitaisha vizuri upande wake...
Kuiba kaiba, haina ubishi, anachotafta ni kufukuliwa makaburi..
Lakini hata wakiamua wamkomeshe kibabe pia hawashindi.
 
Maganga. Kagangamala ngosha ze doni hataki ujinga
 
Waalimu bhanaa wanamlipa katibu wao mil 7 wao wanakula vihela mbuziiii...!! Jamaa kashajipanga hata kama akifukuzwa kazi sawa tu shida kama wataenda kwenye biashara zake na mali zake binafsi.
 
Waalimu bhanaa wanamlipa katibu wao mil 7 wao wanakula vihela mbuziiii...!! Jamaa kashajipanga hata kama akifukuzwa kazi sawa tu shida kama wataenda kwenye biashara zake na mali zake binafsi.
Hivi alikua anakula M7? Huyu kwa ufupi amejitosheleza,
Yeye Angefuata taratibu tuu za kuomba hata kustaafu, atemane nao..

Kosa alilofanya kiuhalisia adhabu yake ni kuachishwa kazi tuu, ila kwakua juu wanajua huyu kazi sio tena kipaombele chake, na hua wanapenda kuhakikisha maamuzi yao yanakuumiza, hapa ndio watamfuta nje ya hapo sasa.
 
Mnamo Januari 25, mwaka huu, Maganga, Makamu wa Rais wa CWT, Dinna Mathaman na Rais wa CWT, Leah Ulaya waliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Wakuu wa Wilaya lakini Maganga na Mathaman hawakufika kuapa.
Mbona huyo Dinna waliyegoma naye kwenda kuapishwa yeye haadhibiwi? Hii ni double standard. Nchi ya kipuuzi sana hii inayopenda kulipiza kisasi ndio maana imelaaniwa kwa sababu za kishetani kama hizi.
 
Mimi nashangaa. Ni hatua gani za kinidhamu wanataka kumchukulia? Mbona sheria ikpo wazi mtu asiporipoti kazini kwa siku 3 mfululizo anakuwa amejiachisha kazi yeye mwenyewe? Wanataka kumfunga jela au wanamtafutia sababu ya uhujumu uchumi wa CWT wamfunge jela za wahujumu uchumi?

Ila hii nchi inapenda kulipiza kisasi sijapata kuona. Nikikumbuka walichomfanyia Tundu Lissu sina hamu nao. Ushetani tupu!
 
Huyo achunguzwe, hawezi kuwa na kiburi cha kiwango hicho kama hajapiga pesa nyingi za CWT.

Maswahili akipata...
Sheria ziko wazi. Mtumishi asipoenda kazini kwa siku 3 mfululizo bila ruhusa anakuwa amejifuta kazi. Huyu hajaenda kazini tangu oktoba mosi halafu anahesabika kuwa ni mtumishi wewe huoni kwamba hapo kuna tatizo? Kuna mahali naye anamtega mwajiri amle kichwa. Tutasikia mengi.

Ni watumishi wangapi wanafukuzwa kazi kimya kimya lakini huyu wanataka suala lake liwe la kitaifa? Mijitu mingine huko serikalini ni kama miendawazimu tu. Hasa hilo limkurugenzi la Temeke. Si wamfute kazi sasa? Wanaogopa nini? Wamfute tu aende mahakamani wamlipe mamilioni. Wapuuzi wakubwa punguani wahed.
 
Ungechunguza kujua sababu ya kugomea uteuzi ungegundua kumbe naye ni Ng'ombe tu sio kichwa kama unavyodhani.

Sababu ni hiyo nafasi aliyokuwepo kwa muda anaingiza okoto la uhakika zaidi kuliko kwenye UDC alikotakiwa kwenda,uliza mwalimu yeyote.
Sasa akama amekataa uteuzi kwa sababu hiyo na amegoma kwenda kazini adhabu yake auawe au afukuzwe kazi? Hebu tuambie sheria za kazi zinasemaje? Kutorudi kazini kwa mujibu wa sheria kuna uhusiano gani na ung'ombe wake na maokoto ya CWT?

Ameishajua mahali serikali walikosea naye anawatega wamfute kazi awaburuze mahakamani. Uidhani yeye bwege kama yalivyo mabwege ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…