Katibu mkuu CWT agoma kurudi Temeke kufundisha

Una hakika kaiba shilingi ngapi? Ukiitwa kwenda kutoa ushahidi mahakamani utaenda? Punguza utoto ikiwa huwezi kuacha kabisa. Mtu kagoma kwenda kazini tangu tarehe 1 had leo ni tarehe 18 kwanini wasimfukuze wakati sheria ziko wazi? Serikali ya CCM na vibaraka wake mna matatizo sio bure!
 
Wameamua kumkomalia kisa kukataa teuzi,sio kila mtu ni mtumwa wa teuzi,waache ushamba.
Anatakiwa kufuata taratibu tu. Usipofuata sheria na kanuni zitakuumbua tu. Hapo hakuna ushamba wowote. Kama ni ushamba anafanya huyo aliyekuwa CWT
 
Mbona huyo Dinna waliyegoma naye kwenda kuapishwa yeye haadhibiwi? Hii ni double standard. Nchi ya kipuuzi sana hii inayopenda kulipiza kisasi ndio maana imelaaniwa kwa sababu za kishetani kama hizi.
Umeshatafuta ukweli wa huyo Dinna? Pengine bado ana mkataba na CWT, hawawezi kumfanya chochote. Ndiyo sababu hata huyo Maganga alivyokataa uteuzi Feb 2023 hawakuweza kufanya chochote mpaka Mkataba wake na CWT ulivyoisha September 2023 alivyoomba tena wakamnyima na kutakiwa kurudi kituo chake cha kazi.
 
Hawezi kuwaburuza mahakamani. Yeye kashika makali yatamkata.
 
Huyo achunguzwe, hawezi kuwa na kiburi cha kiwango hicho kama hajapiga pesa nyingi za CWT.

Maswahili akipata...
Shule ulienda kusomea ujinga ,unazani kila mtu ni mwizi kwanini hamtaki kutafuta ukweli mnakua kama hamna vichwa ..

Kwa akili ya kawaida nani hapa Afrika anaweza kumkatalia Rais abaki salama ,kilichopo kuna genge lilikua CWT walimuweka Katibu mkuu wao ,baadhi yao ni viongozi wanasiasa wakawa wanachota fedha walimu ,

Baadae TAKUKURU Ikastukia ,ikamkamata aliekua Katibu mkuu Seif ambae ndio alikua mshirika wa ilo kundi la wanasiasa akafungwa miezi sita ,akapoteza nafasi ya kuwa katibu mkuu

Maganga alikua Naibu katibu mkuu ,aka panda kwa mujibu wa katiba yao ,ilo genge likaapa lazima wamtoe waweke mtu wao ,kwa namna yoyote yule ,wakatumia nguvu yao wakamchomekea kwenye Udc watu watatu Rais wa CWT, aliekua Makamu wa Rais (alikua mshirika wa ilo genge ) na Katibu mkuu ,

Rais wa CWT na katibu Mkuu wakamuomba Rais wabaki CWT lile kundi lilotaka kumtoa likaona limeshindwa kumtoa ,wakanunua vyombo vya habari kila siku viandike kuwa amemgomea Rais ,wakaona bado hawafaniki

Sasa wakasema watahakikisha hapati kibali cha nyongeza...ili arudi shuleni

Sasa wanaotumika wanashindwa kujua tofauti ya secondment na leave without pay ..

Maganga hana Secondment ana leave without pay

Pia kuwa Katibu mkuu hana ulazima kubaki kuwa mtu mwenye nasaba na serikali

Yeye alichaguliwa na baadae ajira na chama

Jitahidi kusoma sheria za ajira na mahusiano kazini ,mikataba ya kimataifa kutoka ILO 87 ,98
 
Akirudi ana kuta barua mezani ya uhamisho kwenda swekeni kama sio tukuyu Au huko nkasi basi mabamba mpakani na burundi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Tukuyu sio sweken.
Ushafika Kibondo weye? Kule uchawi, vumbi na silaha nje nje.
 
Naona unaropoka ushuzi tu. Huyo akitumiwa TAKUKURU watamkuta tu na kesi ya kujibu. Usimjaze kiburi akaja kujuta. Na akizidi kuleta ujuaji anaweza kupewa likesi akahangaika nalo hata miaka mitano halafu baadae DPP akasema hana nia ya kuendelea na kesi mchezo ukaishia hapo huku akiwa ameshatepeta.
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘
Hapa sasa nimemuelewa...
 
Achunguzwe ujulikane ukweli, CWT kuna pesa za Walimu wengi sana na kuna madudu mengi yamesharipotiwa huko nyuma.
 
Acha umbeya wa kisagaji wewe bibi. Tabia ya kutoenda kazini kwa siku 3 consecutively adhabu yake ni kufukuzwa kazi. Wewe unataka wamuue kama walivyojaribu kumuua Tundu Lissu. Acha use.nge basi.
Huyo achunguzwe, lazima kuna madudu kayafanya.
 
Walimu wakilalamika makato ya CWT sasa serikali itawasikia kilio chao kuwa kuna wababe wansishi Tz kama wafalme.
 
Serikali pia isitishe kutoa vibali vya likizo bila malipo kupitia kwa katibu mkuu utumishi kwenda CWT.

Makatibu wa CWT wanakimbia ualimu kufundisha wanakimbilia kula fedha za walimu.

Ni muda sasa walimu kuruhusiwa kuchagua chama cha wafanyakazi wanachopenda kujiunga badala ya kulazimishwa kuingia CWT tu.

Ni muda sasa takukuru kufuatilia makato ya 2% ya mishahara ya walimu ysnakopelekwa na yanafanya kaxi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…