TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

Umeandika kwa upole sana
Pole Rais Magufuli na familia yote ya Kijazi. Tetesi za Kijazi na Dr. Mpango kuwa wanaugua Covid-19 zimekuwepo kwa siku kadhaa sasa; Ina maana corona imeingia Ikulu. Rais Magufuli anahitaji kuangalia mkakati wake kwani coronavirus haina heshima na haitakoma hadi idhibitiwe kisayansi.
 
Mungu amlaze kwema, Kama taifa tunapita pagumu kidogo lakini si punde tutavuka Hali ya kua tupo na uzima.
 
Huyu alilazwa na Diwani tatizo la kupumua (Corona) sasa sijui Kipara ana hali gani na ile betri yake
Cabinet nzima wengi wameupata.

Hao wanaokufa jua imeshindikana kweli, tatizo lao wanataka mfurahisha mtu.
Mungu hajaribiwi
 
Pole Rais Magufuli na familia yote ya Kijazi. Tetesi za Kijazi na Dr. Mpango kuwa wanaugua Covid-19 zimekuwepo kwa siku kadhaa sasa; Ina maana corona imeingia Ikulu. Rais Magufuli anahitaji kuangalia mkakati wake kwani coronavirus haina heshima na haitakoma hadi idhibitiwe kisayansi.
Sasa mmeanza kuamini njia za kisayansi badala ya nyungu?
 
Inashtua inatisha. Jamani sisi siyo wajuvi kuliko Dunia nzima.

Tukiri tulifanya makosa, tuwaombe wenzetu waliopitia hii hali, wana uzoefu. Watusaidie. Kuna siku itafiki hata waliosalia watageuka vichaa kwa kuchanganyikiwa.

Corona ni hatari, ni rahisi kama tulivyodhani. Haiwezekani watu wote wasiwe na akili, waogope kisichoogopesha.

Nina hakika hakuna palipo na amani kwa sasa, si ikulu, si jeshini, si mahali popote. Kila mahali ni hofu tupu.
Tulikuwa case study kwa dunia jinsi tulivyoishi na huyu mdudu 2020, naona tena tumerudia kuwa case study kama taifa linalovuna lilichokipanda 2021🤔🤔

Tukaze tu mikanda, billgate alijua huyu mdudu n hatari kiasi gan ndo mana alisema tutakuwa tunaokota maiti. Watu waliomwelewa wakaweka mikakati ili kujikinga but sisi tukapuuza, hili ndo litakalotokea tusipo kuwa care😪😪
 
Kujilinda ni jukumu la mtu binafsi. Ina maana huna sabuni? Huna uwezo wa kununua barakoa ya 500? Huwezi kuweka distance kati yako na mtu mwingine? Unataka Rais akushikie kiboko kufanya hayo? Embu tuwe serious kidogo jamani.
..wananchi watavaa vipi barakoa wakati bwana mkubwa anazikejeli, mpaka anasema zinafanana na matiti ya kina mama?
 
Firauni wa misiri alikua na roho ngumu licha ya kuona miujiza yote mungu aliyokua anaitenda kupitia musa, mpaka pale mwenyezi mungu alipoamua kuumpa pigo kali na la mwisho la kuchukua uzao wa kwanza katika familia za wamisiri.

Itoshe tu kusema kuna viongozi wana roho ngumu Kama za farao wanadhani haya mambo yatapita tu bila kuchukua hatua yoyote, sasa haya ndio matokeo yake mficha ugonjwa kifo umuhumbua
 
Naona comments nyingi humu ni ushabiki na bendera fuata upepo.
1. Wote tunakumbuka jinsi mwaka Jana tulivyo pambana pamoja tulishinda
2. Rais kwa kinywa chake kesha sema tuchukue tahadhari zote, hata wizara ya afya imetoa muongozo, kosa la serikali liko wapi
3. Tukumbuke hii ni new variant, je nani kaleta? Is it only for Africa?
Hebu tuchukue tahadhari tukiwa tunajiuliza maswali.
Hata huko kwenye chanjo bado wanakufa in large numbers
Tuache kulaumu Rais bana. Huo ni ushamba
 
Pole Rais Magufuli na familia yote ya Kijazi. Tetesi za Kijazi na Dr. Mpango kuwa wanaugua Covid-19 zimekuwepo kwa siku kadhaa sasa; Ina maana corona imeingia Ikulu. Rais Magufuli anahitaji kuangalia mkakati wake kwani coronavirus haina heshima na haitakoma hadi idhibitiwe kisayansi.
Kuhusu mikakati ulishausema na kuandika hapa

Andika tena ushauri
 
Back
Top Bottom