mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Una maana gani? Hakuna aliyewahi kuficha maradhi!! Usitake kutengeneza picha ya uongo!! Tulichosema na kukiri kama Taifa ni kuwa " Mungu ametuponya na janga la Corona!!Mficha malazi kifo humuumbua, nasema uongo ndugu zangu?
Huo ni ukweli mtupu ambao haukanushiki na uko wazi!! Ndio maana vyuo na shule zilifunguliwa, lockdown haikuwepo na tuliachana na barakoa! Duniani kote kwingine shule na vyuo havikufunguliwa na wengine walipojaribu kufungua wakafunga tena Hadi leo!! Je huko mashuleni na vyuoni mmeshuhudia vifo vya halaiki? hakuna kitu kama hicho kwa kuwa Mungu alikuwa ametuponya!
Mungu akikuponya haina maana kuwa huwezi kuugua tena madam bado unaishi!! Suluhisho ni kuwa ukiugua tena unamwomba Mungu tena ili akuponye kama alivyokuponya awali!! wala siyo kwamba ukiugua tena maana yake ni kuwa Mungu alikuwa hajakuponya!! Watanzania tumwombe Mungu tena Kama tulivyofanya awali na atatuponya tena Kama alivyotuponya hapo awali kwa kuwa mapenzi yake kwetu hayabadiliki!
Kuna watu wanakejeli na kubeza na Mungu anawaona!
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso