TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

Wewe unataka afe baba yako ndio uone kifo kikuume?

Endelea kudhani kwamba kwa akili zako wewe utaishi milele ila Kumbuka bado ni asubuhi na mchana wako, jioni na hata usiku huvijui... viko mikononi mwa muamuzi wa mwisho

Chukua tahadhari na mwombe Mungu sana
Mungu gani mnazungumzia wenzenu wanakufa mnawakejeli..Mungu gani anaagiza kukejeli watu kipindi cha matatizo ikiwa wewe nawewe upo hapo hapo duniani...Yani mwenzio anazika ndugu unadhani mataifa kama marekani au ulaya hakuna watu wa Mungu mpaka mnawakejeli eti leo mnataka kumuomba Mungu!!?

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
yani mkuu miaka hii wangekufa wakina mzee mengi ruge watu wangesema ni corona utazani magonjwa mengine hayauwi Tanzania tuko vizuri au nasema uongo ndugu zanguuuuu
Ikitokea ugonjwa unapita na familia kwann usitilie shaka..space ya mengi na ruge kufa ilichukua muda gani wewe sas leo 2 days 2 public figures kwann usiogope

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
hakuna korona..ts just siku zao zimefika..Tatzo wanakufa kpind korona imeshika hatamu..
Tatizo sio siku kufika tatizo kwann ifike kwa pamoja kwa watu wa umri mmoja sahivi. Ny waafrica hizo dini zilikuja za aina mbili za kweli na za kitumwa naona mmeamua kuchagua za mwisho hizo mnaacha kutumia akili

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
We unadhani kusema jifukizeni inatosha mkuu? Kwa akili yako hiyo ndio hatua watu wanayotaka serikali ichukue?
Jana wafanyakazi wa almashauri Mbeya mjini wamegoma kuingia maofisini, juzi wamepoteza mfanyakazi na jana kadondoka mwengine!
Fikiria mbali acha kuwaza nyungu tu kuwa ndio hatua stahiki wakati hospital PPE's ni chache, motungi ya oxygen haitoshi na wauguzi wako kwenye mazingira mabaya ya kukabiriana na wagonjwa wenye changamoto za kupumua.
sawa.sote tunajua changamoto iko arround.chanjo ndo hizo zina malalamiko kibao.mpaka sasa bado hakuna chanjo inayoaminika kuwa na ufanisi,bado ni trial & error.sasa si bora kuchukua tahadhari?ukigoma Kama huchukui hata jitihada mbadala ni kazi bule.sayansi bado haijapata suluhisho Hadi sasa ,kisayansi hakuna chanjo yenye tija ambayo imewahi kutengenezwa kwa miezi 24,ndio maana sijui hiz Astra zenecca na zngine bado zina malalamiko kibao na Visa vingi.kwa kawaida chanjo yenye ufanisi hughalimu Hadi miezi 60 kuitafiti/kutengenezwa.na mzazi mwelevu hawezi kuwatoa wanae kwa majaribio....janga lipo tuchukue tahadhari mbadala.sio kulalama na kugoma ni ujinga wa akili,na upungu wa maarifa.
 
Unajua kutangaza sio kusema tu ipo asee wewe ndo mjinga kweli hujui kwamba hatua za muhimu lazima zifanywe na serikali kama vile kupiga marufuku mikusanyiko,madaladala kuweka utaratibu level seat na mambo mengine
Utakuwa kajinga pia, mzee alishasema kuweka watu lockdown huo ujinga hatafanya! Sasa ni jukumu letu raia kujichunga! Subiri utangaziwe na serikali tuone kama utasikia!
 
Mweeh Kijazi wa watu. Moja ya viongozi niliokuwa nawaelewa. Kwa kweli hali inatisha sana.

RIP.
Marehemu hasemwi vibaya lakini Hawa ndo wamelelea mfumo mbovu, uliopelekea kuua demokrasia na uchumi
 
Huna mchango wowote wa maana ni utopolo tu, mtu mwenye akili timamu hawezi kuwaza mambo ya kuvunja katiba ili fulani aongezewe muda kwa kipi hasa. Nenda kakojoe ukalale hujui chochote wewe
Ndiyo sina mchango wowote wa maana kwa mtazamo wako. Nakubaliana na wewe 100%. Lakini eh dunia nzima hauko wewe peke yako. Tuko watu karibu bilioni 7 na kati yao kama asilimia moja hivi inawezekana wakawa wanazungumza au kukielewa kiswahili na kati yao kama watu laki tatu ni wasomi wa JF. Sasa wewe huoni kuwa katika hao laki tatu, you are nothing?

Kwa hali hiyo nami ningepenpenda kuchukua nafasi ya kukuuliza wewe mnuka jasho la uswahilini Bongo, katiba ni nini?
Kama binadam anadiriki kubadili maandishi tukufu ya kwenye msaafu na biblia katiba itakuwa ni kitu gani?

Wachina ambao hivi sasa ni number one katika mambo yanayo husu uchumi na maendeleo duniani na ambao wanasaidia kujenga infrastructres za maendeleo ya nchi yako walichukua maamuzi ya kubadili katiba yao, ili kumpa Xi Jiping kutawala maisha nchi kubwa duniani, sembuse sisi, tushindwe hata kumwongezea Rais wetu anayefanya vizuri kukamilisha njozi zake kwa faida yetu sote, miaka mitano tu?

Mimi nilifikiri wewe unaye mpinga Magufuli kwa madai kuwa yeye sio democratic, sikujua kuwa kumbe wewe mwenyewe maana ya democracy huijui.

Katiba ni sheria ambayo inaweza mda wowote ikabadilishwa kulingana na mabadiliko ya mazingira ambayo binadam yana m-favour. Sheria isiyo kwenda na wakati nafikiri hiyo ni sumu kwa maendeleo ya binadam. Nafikiri mfano mzuri unauona hivi sasa kinacho tokea Amerika. Sina haja ya kukueleza mengi, kwani natambua kuwa kama akili yako ni makini katika ku Analyse vitu basi utakuwa umenielewa kitu gani ninakimaanisha.

Siko hapa ku argue na wewe kuhusu katiba bali itoshe tu kuelewa kwamba demokrasia huanza na wewe mwenyewe dhidi ya mtazamo wako kwa maoni ya wenzako. Kama umeshindwa ku maintain hili basi uelewe kuwa hata wewe mchango wako hauna thamani kwa wenzio.

Kuheshimu mawazo ya wenzako ni tunu ya demokrasia unayo ililia. Bila hiyo sudhani kama jamii itakuwa na uwezo wa kuishi pamoja kwa amani na maelewano.
 
Ni huyu. Nilikua sehemu haina access na habari leo naingia humu nikakuta comment yako ndiyo maana nikauliza.

Amefariki aisee na mazishi leo nadhani utakuwa umeingia mtandaoni moja kwa moja JF, nilielewa maana ilibidi nicheck profile yako nikaona mara ya mwisho ume-comment tarehe 4 February
 
Mkuu sikiliza, acha maneno mengi chukua hatua jilinde. Kama unaona mwendokasi itakuua usipande tafuta njia nyingine au tembea. Hivi ni vita vyako ww na familia yako.

Walioko serikalini wanapanda V8 wanakufa ww unasema mambo ya mwendokasi. Kwa hiyo serikali isipotoa tamko basi ww utajiacha ujifie zako tu?
Hukuona sokoni walivokuwa wanabadilisha mic na watu sokoni afu we unadhani kuambukizana ni lazima mpaka muwe mmejaa kujaa kunakatazwa kwasababu mtaambukizana wengi ila kuambukizwa ni mmoja 2 anatosha

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]....nyungu Tena jaman!!!!! Ama kweli ujinga Ni aghali Sana.
so do you have any means.lete Hapa tuone.mkiambiwa still bado hakuna chanjo yenye ufanisi vichwa vigumu Kama nazi.wazungu wenyewe bado inawaumiza kichwa na bado wako kwenye trial &error ,ndio maana malalamiko ya hiz chanjo ni mengi.sasa si bora kuchukua tahadhari mbadala kuliko kulalama humu ujinga!!?? kweli kukosa maarifa ni hasara kubwa.
 
Naona Corona sasa imeamua kujibu.
Inapiga fresh bara na visiwani.
Poleni wafiwa.
Nani kakuambia ni Corona? Hakuna Jambo hilo kwenye taarifa tuliyopewa.

Inaelekea ungependa sababu ya kifo iwe Corona! Nasema hivyo kwa sababu unakimbilia huko japo hujapewa taarifa hiyo!

Kusema ukweli hata kama mtu alikuwa na virusi vya Corona, akifa haina maana kuwa ameuliwa na ugonjwa wa Corona! Anaweza kufa kwa malaria japo ana Corona, anaweza kufa kwa typhod japo ana Corona, na anaweza kufa kwa ugonjwa mwingine wowote. Ni madaftari tu ndio wanaweza kusema ni ugonjwa upi uliopelekea kifo chake.
 
😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😢😢😢😢😞😞😞
RIP Katibu Mkuu Kiongozi........ My heart is bleeding for the loss.
RIP (in advance) jiwe kuu 😡😡
 
Kuna moja nimetoka Kupenyezewa sasa hivi na nimeanza Kutetemeka kwani huenda Seif akasindikizwa na Mzanzibari Mwenzake mwana Mama, ila Jitu Bishi ameshapatwa na Presha na nasikia anahangaika mno Kumpigia Simu FM wa China Kumlaumu ila hawaelewani kwani Mchina anaongea Kiingereza cha ndani kabisa huku Yeye akichanganya tu Kisubi, Kiswahili na Kisato pamoja na Kisangara chake.
Duuuuuh hali ni mbaya kwa kweli lol.
 
Kuna moja nimetoka Kupenyezewa sasa hivi na nimeanza Kutetemeka kwani huenda Seif akasindikizwa na Mzanzibari Mwenzake mwana Mama, ila Jitu Bishi ameshapatwa na Presha na nasikia anahangaika mno Kumpigia Simu FM wa China Kumlaumu ila hawaelewani kwani Mchina anaongea Kiingereza cha ndani kabisa huku Yeye akichanganya tu Kisubi, Kiswahili na Kisato pamoja na Kisangara chake.
Duuuuuh hali ni mbaya kwa kweli lol.
 
Back
Top Bottom