Huna mchango wowote wa maana ni utopolo tu, mtu mwenye akili timamu hawezi kuwaza mambo ya kuvunja katiba ili fulani aongezewe muda kwa kipi hasa. Nenda kakojoe ukalale hujui chochote wewe
Ndiyo sina mchango wowote wa maana kwa mtazamo wako. Nakubaliana na wewe 100%. Lakini eh dunia nzima hauko wewe peke yako. Tuko watu karibu bilioni 7 na kati yao kama asilimia moja hivi inawezekana wakawa wanazungumza au kukielewa kiswahili na kati yao kama watu laki tatu ni wasomi wa JF. Sasa wewe huoni kuwa katika hao laki tatu, you are nothing?
Kwa hali hiyo nami ningepenpenda kuchukua nafasi ya kukuuliza wewe mnuka jasho la uswahilini Bongo, katiba ni nini?
Kama binadam anadiriki kubadili maandishi tukufu ya kwenye msaafu na biblia katiba itakuwa ni kitu gani?
Wachina ambao hivi sasa ni number one katika mambo yanayo husu uchumi na maendeleo duniani na ambao wanasaidia kujenga infrastructres za maendeleo ya nchi yako walichukua maamuzi ya kubadili katiba yao, ili kumpa Xi Jiping kutawala maisha nchi kubwa duniani, sembuse sisi, tushindwe hata kumwongezea Rais wetu anayefanya vizuri kukamilisha njozi zake kwa faida yetu sote, miaka mitano tu?
Mimi nilifikiri wewe unaye mpinga Magufuli kwa madai kuwa yeye sio democratic, sikujua kuwa kumbe wewe mwenyewe maana ya democracy huijui.
Katiba ni sheria ambayo inaweza mda wowote ikabadilishwa kulingana na mabadiliko ya mazingira ambayo binadam yana m-favour. Sheria isiyo kwenda na wakati nafikiri hiyo ni sumu kwa maendeleo ya binadam. Nafikiri mfano mzuri unauona hivi sasa kinacho tokea Amerika. Sina haja ya kukueleza mengi, kwani natambua kuwa kama akili yako ni makini katika ku Analyse vitu basi utakuwa umenielewa kitu gani ninakimaanisha.
Siko hapa ku argue na wewe kuhusu katiba bali itoshe tu kuelewa kwamba demokrasia huanza na wewe mwenyewe dhidi ya mtazamo wako kwa maoni ya wenzako. Kama umeshindwa ku maintain hili basi uelewe kuwa hata wewe mchango wako hauna thamani kwa wenzio.
Kuheshimu mawazo ya wenzako ni tunu ya demokrasia unayo ililia. Bila hiyo sudhani kama jamii itakuwa na uwezo wa kuishi pamoja kwa amani na maelewano.