Katibu Mkuu TABOA; Watanzania Wajiandae Na Nauli Mpya

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Watanzania wajiandae gharama za usafirishaji tutaziongeza kwa sababu ukifika Stendi ya Magufuli ushushe uchukue lori au usafiri mwingine ukodi upeleke ofisini kwako ili yule anayekuja kupokea huo mzigo aukute ofisini kwako.

"Na tunasikitika sana Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba alituomba baada ya mafuta kupanda tuvumilie hasara. Sasa tunajiuliza wale Watanzania ambao alisema tusiwaongezee nauli ni hao Leo wanalazimishwa washuke Magufuli?- Priscus John, Katibu Mkuu wa Wamiliki wa Mabasi ( TABOA) akihojiwa kupitia Cloudstv

nauli.png
 
Naona baadhi ya wadau wanaopinga kutumia stand ya Magufuli wana argument za kipimbi sana
Sijamuelewa kabisa.

Kwamba ukishapanda gari kutoka mwanza kuja Dar ukifika Magufuli wenye basi wanapaswa tena wakutafutie basi lingine wakupeleke labda gongo la mboto au chanika?

Mi ninavyoelewa Magufuli ni destination na mkifika kila abiria atajua yeye anafikaje anapoenda.

Ni kama ukipanda ndege tu ukishashuka kwa Nyerere unapokwenda ni jukumu lako kwa gharama zako sio jukumu la kampuni ya ndege uliyopanda.
 
Watanzania wajiandae gharama za usafirishaji tutaziongeza kwa sababu ukifika Stendi ya Magufuli ushushe uchukue lori au usafiri mwingine ukodi upeleke ofisini kwako ili yule anayekuja kupokea huo mzigo aukute ofisini kwako.

"Na tunasikitika sana Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba alituomba baada ya mafuta kupanda tuvumilie hasara. Sasa tunajiuliza wale Watanzania ambao alisema tusiwaongezee nauli ni hao Leo wanalazimishwa washuke Magufuli?- Priscus John, Katibu Mkuu wa Wamiliki wa Mabasi ( TABOA) akihojiwa kupitia Cloudstv

View attachment 3654382
Mnajuana nyie matajiri
 
Hoja mfu kabisa,, mambo ya abiria wa gongo la mboto na mbagala wewe yanakuhusu nn mmiliki wa bas?
Destination ni Magufuli bus
terminal.
.sio vinginevyo.
Tanga wanashusha na kupakia abiria kange bus terminal,,mbona hawakupandisha nauli?
 
Mimi bado sijaelewa wakuu, kwahiyo mtu kama yupo bunju anataka kwenda Tanga mpaka aende mbezi?
Au mtu Yuko Mbagala anataka kwenda Masasi mpaka aende mbezi? Nikipata hayo majibu nitachagua upande, TABOA au Chalamila.
 
Sijaelewa.

Gari kuishia Magufuli stendi kunaongezaje gharama kwa mmiliki wa basi?
Anamaanisha hivi ukipanda kwenye bus na mizigo yako bus likishafika Magufuli wale abiria wenye mizigo itabidi waende kuisubiria kwenye ofisi kuu ya bus either Shekilango au Magomeni au Kariakoo na kwa vile bus zao haziruhusiwi kwenda mjini hiyo mizigo wataipakia kwenye lori hadi ofisi kuu ya bus hapo ndipo gharama za uendeshaji zinapoongezeka
 
Watanzania wajiandae gharama za usafirishaji tutaziongeza kwa sababu ukifika Stendi ya Magufuli ushushe uchukue lori au usafiri mwingine ukodi upeleke ofisini kwako ili yule anayekuja kupokea huo mzigo aukute ofisini kwako.

"Na tunasikitika sana Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba alituomba baada ya mafuta kupanda tuvumilie hasara. Sasa tunajiuliza wale Watanzania ambao alisema tusiwaongezee nauli ni hao Leo wanalazimishwa washuke Magufuli?- Priscus John, Katibu Mkuu wa Wamiliki wa Mabasi ( TABOA) akihojiwa kupitia Cloudstv

View attachment 3654382
Hivi huyo mbwa ni nani nchi hii mpaka awe na uwezo wa kuongeza nauli? Bila hata hofu wala aibu, eti waziri mkuu alituomba! Hv hii nchi ndiyo imefikia hatua hii? Kwamba matajiri wanaendesha nchi sasa? LATRA imeshafutwa? Ila kweli hatuna Rais, ile kauli ya Magufuli kwamba "mtanikumbuka" ilikuwa ni ya kimaono! Huyu mzanzibari angeondolewa kwa njia yoyote ile mpaka 2030 tutakuwa tumekwisha. RC wa Dsm alifanya kazi ya Waziri wa Uchukuzi na ya LATRA. Matajiri wameiweka serikali mifukoni mwao!
 
Mimi bado sijaelewa wakuu, kwahiyo mtu kama yupo bunju anataka kwenda Tanga mpaka aende mbezi?
Au mtu Yuko Mbagala anataka kwenda Masasi mpaka aende mbezi? Nikipata hayo majibu nitachagua upande, TABOA au Chalamila.
Mtu wa masasi kama yupo mbagala kuna stand za magari ya kusini..

Ila kwa watu wa njia ya Morogoro na chalinze wanapandia Magufuli na kushuka Magufuli bus terminal.
Kama upo bunju sogea Magufuli terminal chukuwa usafiri.
Au kama bus linapita njia ya bagamoyo utapandia njiani.
Kisichotakiwa ni abiria kupanda bus au kushuka mitaani..badala ya stand ya Magufuli
 
Sijamuelewa kabisa.

Kwamba ukishapanda gari kutoka mwanza kuja Dar ukifika Magufuli wenye basi wanapaswa tena wakutafutie basi lingine wakupeleke labda gongo la mboto au chanika?

Mi ninavyoelewa Magufuli ni destination na mkifika kila abiria atajua yeye anafikaje anapoenda.

Ni kama ukipanda ndege tu ukishashuka kwa Nyerere unapokwenda ni jukumu lako kwa gharama zako sio jukumu la kampuni ya ndege uliyopanda.
MizigO
 
Anamaanisha hivi ukipanda kwenye bus na mizigo yako bus likishafika Magufuli wale abiria wenye mizigo itabidi waende kuisubiria kwenye ofisi kuu ya bus either Shekilango au Magomeni au Kariakoo na kwa vile bus zao haziruhusiwi kwenda mjini hiyo mizigo wataipakia kwenye lori hadi ofisi kuu ya bus hapo ndipo gharama za uendeshaji zinapoongezeka
Sasa mimi kusafirisha mzigo kwa gharama zangu kunamuathiri vipi yeye mpaka kuongeza nauli?

Kama basi linaishia Mbezi Magufuli hata mzigo unatakiwa uishie hapo na mwenye mzigo ni jukumu lake kuhakikisha unafika anapokusudia kwa gharama zake na kwa ufahamu wangu ndivyo ilivyo kabla hata hawajaambiwa ni lazima kuishia Magufuli.
 
Back
Top Bottom