Katibu Mkuu wa CCM atoa onyo kwa Membe akimtaka kutokuwa juu ya katiba ya chama

Katibu Mkuu wa CCM atoa onyo kwa Membe akimtaka kutokuwa juu ya katiba ya chama

Ungetusaidia kafanya nini tena safari mpaka hii mikwara ya chama chenye democrasia ya juu inapigwa hivi.'' Niguse ninuke'' [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Eti ile kusema sakata la bombardier yetu kuwa Serikali ya Canada haihusiki ndiyo mipovu yote hiyo kama amesukutua omo. Wale wanafunzi watakuwa wanasikitika sana mwalimu wao kuwehuka hivi.
 
Mtendaji si anaweza akafunga ofisi asiipate hiyo fomu au akashindwa kuirudisha? As simple and childish as that!
Na kweli kwani mbinu hii imewapa ushindi wa 100% kwenye uchafuzi wa serikali za mitaa.
 
1574867645614.png


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemuonya Benard Membe, kutokuwa juu ya katiba ya chama hicho.

Onyo hilo limetolewa leo na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM, wakati akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Konani kinachorushwa na Kituo cha ITV kupitia mitandao yao ya kijamii.

Dk. Bashiru ameeleza kuwa, kama Membe ataendelea kutofuata utaratibu, uongozi wa chama hicho utamlazimisha kufuata utaratibu.

“Membe ni mwanachama mwenye haki ya kikatiba lakini ana wajibu. Kwa hiyo kama anataka kuwa mwanachama wa CCM kama walivyo wengine, lakini wametupa ushindi tunaojivunia afutae utaratibu. Asipofuata utaratibu, atalazimishwa kufuata utaratibu,” ameeleza Dk. Bashiru.

Hata hivyo, Dk. Bashiru amesema Membe hakuwahi kujadiliwa katika vikao vya chama, licha ya kwamba hakuitikia wito wake, alipomtaka kuonana nae akiwa mkoani Geita.

“Hatukuwahi kumjadili na kwenye vikao hakuwahi kufika, kosa halifi kama jinai, kosa halifi unaweza ukadhani limekufa kumbe ni utaratibu wa wakati. Kupitia kwako, naomba kueleza wana CCM tuko makini kulinda utamaduni wa chama, na wanachama kutii viapo vyao,” amesema Dk. Bashiru.
 
Kina Membe wanaogopa kwamba Magufuli akiongoza hadi 2025 nchi hii itakuwa na maendeleo makubwa sana kuwahi kushuhudiwa.Hivyo wanajaribu kumkwamisha njiani.
#2020 ni Magufuli tu#
 
Bashiru asijifananishe na membe bado kijana mdogo sana.
 
Nimeamini msemo Wa lissu, wakimalizana nasi watafuata kwenu wenyewe.huku kunakoelekea ccm mtifuano waja.
 
Naona anaweweseka tuu 2020 tutapata majibu sahihi ya anachokizungumza kwa kuficha ficha...
 
Membe anafaa kugombania urais kupitia upinzani lakini je si itakuwa muendelezo baadae naye kurudi kwao?
 
Back
Top Bottom