Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akamatwa na Polisi

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akamatwa na Polisi

Hapo wanasubiri reaction yetu wananchi, wakiona moto umekuwa mkubwa watasema wanamshikilia na ‘upelelezi’ unaendelea.
Hapa ndipo vyombo vyetu vya usalama hunichosha, unamshikilia vipi mtu pasi na kuwa na hati ya mashtaka dhidi yake?

Na hata upelelezi huo ukikamilika kila uchwao yanaibuka mashtaka mapya, BS.
Ule waraka ni mzuri na umeelezea uonevu wanaofanyiwa waislamu na serikali yetu huru, ktk nchi yetu huru ya Tanzania. Ni ajabu viongozi wao zaidi ya 100 wanashikiliwa kwenye magereza zetu,na vyombo vyetu vya dola kwa zaidi ya miaka 6 bila kuhukumiwa na mahakama kwa makosa wanaosemekana kuwa nayo.

Tunaposema tuna serikali ovu kuliko ya mkoloni,basi mtuelewe.

Mimi ni mkristo,lakini sikubali hata kidogo matendo maovu wanayofanyiwa ndugu zetu waislamu na serikali yao.

Kama kuna hoja basi serikali imjibu huyu kiongozi wao kwa hoja na si kwa vituko wanavyofanyia huyo shekhe Ponda
 
Breaking news:
Shekh Issa Ponda amekamatwa na Polisi jioni ya leo Saa 11.
Ikumbukwe hivi juzi kiongozi huyo wa Waislamu Tanzania alitoa WARAKA wa WAISLAMU kuelekea Uchaguzi Mkuu 2020

Kwa Wale ambao hamkusoma habari hii hapa 👇

WAISLAMU TANZANIA WATAKA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI

Julai 09, 2020 15:32 UTC

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ametoa mwito wa kufanyika uchaguzi huru na wa haki mwezi Oktoba mwaka huu nchini humo.

Sheikh Ponda Issa Ponda ametoa mwito huo leo Alkhamisi katika kikao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa, vyombo husika vinapaswa kuhakikisha kuwa uchaguzi huo mkuu unafanyika katika mazingira ya amani, uhuru na haki.

Kuhusu sifa za wagombea wa uchaguzi mkuu, Sheikh Ponda amesema waraka uliotolewa na taasisi hiyo imeorodhesha baadhi ya sifa hizo kama ifuatavyo: mgombea awe mkweli na mwenye utu, awe mwenye kuheshimu kiapo, awe mwenye sifa ya kupiga vita ubaguzi wa aina zote na awe mwenye maarifa ya kutosha ya kuongoza watu na serikali.

Sifa zingine zilizoainishwa kwenye waraka huo wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania ni mgombea awe mwenye kuheshimu uhuru na mawazo ya watu wengine, mbali na kuzijua na kuziheshimu haki za binadamu. Kadhalika taasisi hiyo ya Waislamu wa Tanzania imetaka wananchi wasiwachague watu madikteta na wadhalilishaji katika uchaguzi huo wa Oktoba.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania amesema Waislamu wa Tanzania wanataka haki na usawa na ndipo wamekuwa wakishiriki katika chaguzi mbali mbali za nchi hiyo. Amesema Waislamu wa Tanzania hivi sasa hawaoni nafuu katika uhuru wa kuabudu, uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe, usalama wa viongozi wao, Madrasa zao, Misikiti na watu wao.

Aidha ameeleza bayana kuwa, Waislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki hawaoni usawa wowote katika madaraka na ajira za serikali, na kwamba mfumo wa elimu wa taifa hilo umeshindwa kutoa fursa sawa wala kutenda haki kwa wote.
 
Huo waraka unapatikana wapi ofsa Basi tuusome!

Au huo waraka uligusa maeneo gani hadi Sheikh wetu anapata sulba kiasi hiki?
Ni utopolo mtupu mkuu.. Mwendelezo uleule wa waislamu kulalamika kwamba wanaonewa,! Ila safari hii wamekuja na kingine kwamba ilitakiwa selikali iwape kilo 50 za unga kila kaya katika kipindi cha corona.

Sent from my SM-T585 using JamiiForums mobile app
 
Hapa ndipo nitapoweka comment yangu sasa nikishapata nini cha kusema.
 
Askofu bagonza alitoa waraka wa tume huru ya uchaguzi na kuhamasisha watu kuandamana mnamo tarehe 7/7 na kamanda mruto alitolea ufafanuzi kwa yule atakaye andama atakiona cha moto lakini juzi shura ya maimam wametowa waraka kwa hoja walizoona zinafaa na wakatoa maoni ya nini kifanyike leo hii katiwa mkononi...mbona Askofu bagonza hakutiwa hatia kwa uchochezi wa kuhamasisha watu kuandamana?

Hapa sasa naamini kuwa waislamu walivyoeleza kuhusu wao kufanywa kuwa tabaka la pili katika jamii ya kitanzania....Waislam wana hoja katika hili kuhusu kubaguliwa kwao kwa misingi ya udini katika nchi hii..

Haki uliinua taifa,tuwe na usawa pasi na kuabagua kwa misingi ya kiitikadi,dini ,kabila tuijenge Tanzania yetu pasi na kuleta manung'uniko katika jamii zetu
 
Ule waraka ni mzuri na umeelezea uonevu wanaofanyiwa waislamu na serikali yetu huru, ktk nchi yetu huru ya Tanzania. Ni ajabu viongozi wao zaidi ya 100 wanashikiliwa kwenye magereza zetu na vyombo vyetu vya dola kwa zaidi ya miaka 6 bila kuhukumiwa na mahakama kwa makosa wanaosemekana kuwa nayo.

Tunaposema tuna serikali ovu kuliko ya mkoloni,basi mtuelewe.

Mimi ni mkristo,lakini sikubali hata kidogo matendo maovu wanayofanyiwa ndugu zetu waislamu na serikali yao.

Kama kuna hoja basi serikali imjibu huyu kiongozi wao kwa hoja na si kwa vituko wanavyofanyia huyo shekhe Ponda
Mimi ule waraka kiukwekeli kabisa nimeupenda mnoo...
 
25 May 2020
Dar es Salaam, Tanzania

SHEIKH PONDA AWAPA SOMO WAISLAMU : 'WANASIASA WANATUGAWA’

Sheikh Issa Ponda akitoa elimu ya uraia kuhusu uchaguzi 2020 na hali ya kisiasa iangaliwe kwa mapana gani na kujitayarisha kama kundi-maslahi ktk jamii ya kiTanzania kushiriki ktk masuala ya siasa.

Sheikh Issa Ponda anaelezea wapi, chimbuko la Waraka wa Shura liliasisiwa. Elimu hiyo ya uraia iliyopo ktk kitabu kilichozinduliwa na Abbas Sykes mwana TAA , TANU wa mwanzo kunako mwaka 2010 ktk viwanja vya Mnazi Mmoja ndiyo mwongozo wa waraka wa Shura ya Maimamu.

Sheikh Issa Ponda amewataka Waislamu kujitengenezea mfumo wa kutathimini aina ya viongozi wa kuwachagua kwenye chaguzi mbalimbali hususan uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili kupata kiongozi mwenye kuzingatia haki kwa waumini wa dini hiyo Hayo ameyasema jana tarehe 24 Mei 2020 kwenye Baraza la Eid lilikuwa likilenga kuwa semina ya maimamu mbalimbali jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 
Back
Top Bottom