Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akamatwa na Polisi

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda akamatwa na Polisi

Msifanye makosa oktoba,jitokezeni kwa wingi tuondoe hili balaa kwenye nchi yetu .
 
Mbona


Mbona taasisi nyingine za dini huwa zinatoa waraka kila kukicha lakini hatuoni haya ya kukamatwa ksma ilivyo kwa sheikh Ponda! Huyu ndiye sheikh pekee aliyebaki upande wa ukweli #free_sheikh_Ponda
Hivi wewe unajua kweli historia ya Ponda au unaongea tu. Kwa nini polisi hawajawakamata hao waislamu wengine mnaodai wameuandaa huu waraka wamkamate ponda tu. Serikali ina mkono mrefu haiwezi kukurupuka tu kumkamata tu hasa kwenye haya masuala ya kidini.
 
Sheikh Ponda alisema waislam huwa hawana sera, yote wanayokubaliana huwa hayatekelezwi kwasababu wepesi kusalitiana, kwakudanganywa ama kwa pesa au vyeo.

Waraka huo hata kama hakuutoa, "message sent and delivered".
 
Katibu mkuu wa shura ya maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa ponda akamatwa na polisi hivi punde

Amekamatwa akiwa anatoka Msikitini sala ya Alasiri saa kumi na Moja maeneo ya Ilala. Alivyotoka Msikitini anataka kuingia kwenye gari yake ndo Wakamkamata.

Kwa sasa wapo wanasheria wanafuatilia dhamana yake japo inadaiwa wanamhamisha hamisha.

Bado hajajulikana kapelekwa kituo gani.
=======

UPDATES :
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP- Lazaro Mambosasa, ameiambia JamiiForums kwamba ni kweli Polisi wanaye Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda.

"Tunaye sisi Polisi, tumemkamata kwa Mahojiano ya Uchochezi walioutoa kwenye kitu walichokiita Waraka. Tunamhoji kutokana na ule Waraka, Yeye kakubali kwamba ni wake na Taasisi yake lakini Viongozi wote wa Taasisi wameukana kupitia Vituo mbalimbali vya radio na TV. Hivyo tunazidi kumshikilia. Amesema Mambosasa.

Hivi Karibuni, Shura ya Maimamu Tanzania, ilitoa Waraka kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020

Zaidi, Soma;

Uchaguzi 2020 - Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

CUF: Tunatoa pongezi za dhati kwa Waraka uliotolewa na Shura ya Maimamu. Unachora taswira halisi ya hali ilivyo nchini tangu uhuru

Shura ya maimamu yakana kutoa waraka wa uchaguzi, yampongeza Rais Magufuli kwa kuitokomeza Corona
awamu ya 5 inaogopa sana watu makini yaani!
 
Asanteni sana Jeshi la polisi kwa fursa kuhamasisha wadau wengi wafatilie andiko husika ambalo ni mkuki wa moyoni kwa Watawala.
 
Asanteni sana Jeshi la polisi kwa fursa kuhamasisha wadau wengi wafatilie andiko husika ambalo ni mkuki wa moyoni kwa Watawala.
 
Back
Top Bottom