Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki MOON amshauri JK kuhudhuria Mkutano wa Kampala

Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki MOON amshauri JK kuhudhuria Mkutano wa Kampala

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,895
Reaction score
20,392
Wana JF,

Habari nilizopata hivi punde kutoka vyanzo vya kuaminika ni kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kupitia kwa Mshauri wa UN katika ukanda wa Maziwa Makuu, Bi Mary ROBINSON, amemshauri Rais wa Tanzania JAKAYA KIKWETE kuhudhuria mkutano wa ICGLR unaofanyika Jijini Kampala, Uganda. Sababu zilizotolewa ni kama ifuatavyo

  1. Mkutano huo umepewa baraka zote za UN na kwamba umoja huo umetuma mwakilishi kuhudhuria kikao hicho ambaye ni Bi Mary Robinson
  2. Mkutano huo utajikita katika kujadili jambo moja tu ambalo ni hali ya amani mashariki mwa DRC na hautahusisha mazungumzo baina ya JK na PK kutokana na kupishana kauli katika siku za hivi karibuni.
  3. Kutokana na Tanzania kupeleka kikosi kupambana na waasi wa M23, Tanzania itapewa nafasi ya kuelezea mafanikio yaliyopatikana kutokana na operesheni hiyo na kwamba nchi zote za maziwa makuu zitatakiwa kuunga mkono juhudi za Tanzania
  4. Nchi washiriki watapewa makavu na Bi Mary Robinson kutokana na nchi hizo kuwa na tabia ya kuchochea migogoro DRC. Hapa walengwa wakubwa ni Rwanda na Uganda. itakumbukwa kuwa hivi karibuni Katibu Mkuu wa UN Ban Ki Moon amemshutumu Rais wa Rwanda PK kutokana na kusaidia waasi wa M23. Pia Afrika ya Kati inashutumiwa kusaidia waasi wa LRA.
  5. Usalama wa viongozi wote watakaohudhuria kikao hicho umeimarishwa na utakuwa ni jukumu la UN
  6. Tanzania kama nchi mama ya Maziwa Makuu, ni vema kuhudhuria mkutano huo kwa vile usalama wa nchi jirani unapozorota, ni Tanzania ndiyo inayoathirika hasa kupitia wimbi la wakimbizi, wahamiaji haramu na kuzagaa kwa silaha za kivita.

Kutokana na Mazungumzo hayo ambayo yamefanyika kwa njia ya simu baina ya Rais JK na Bi Mary Robinson, Rais JK amelazimika kusitisha ziara yake Mkoani Mwanza na kupanda ndege kuelekea Kampala Uganda jana jioni (tarehe 4/5/2013). Hivi tunavyozungumza Rais wetu amewasili salama na anahudhuria mkutano huo. Aidha, inaelezwa kuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame mpaka leo asubuhi alikuwa hajathibitisha kuhudhuria na huenda asihudhurie kikao hicho ili kukwepa kibano cha Mwanamama Mary Robinson
 
Hapo patamu!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
utakaaje meza moja na mtu ambaye anawaunga mkono M23?? Hapo UN wamekosea issue hapo ni kuruhusu tu drown dhidi ya Rwanda na M23 wao basi ,hamna haja ya diplomacy tena kila siku PK anaimbiwa wimbo ule ule wa kuwasaidia M23 mimi naona anapewa sifa tu bure ikibidi kwa sababu JWTZ wanao hadi ushahidi wa maafisa wa PK ni kumkamata tu PK aende ICC kilichobaki kama hawawezi wawaachie JWTZ wanaweza kumkama dead or alive hukohuko kigali kwake
 
ni jambo jema , ila hala hala wasitoane manundu au kufanyiana "hijacking" wa ki hibyarimana.
 
Lusewa Tunashukuru sana kwa UN kutambua mchango wa Tanzania katika kusaka amani nchini DRC na kutambua kuwa KAAME ni nyoka. Kila la heri JK.
 
Last edited by a moderator:
Lusewa Kwa mtindo huu, KAGAME hatii mguu huko labda awe anakwenda kumuomba JK msamaha
 
Last edited by a moderator:
Tunawapongeza sana UN kwa jitihada wanazofanya kuimarisha amani mashariki mwa DRC. Juhudi za kijeshi zilizoanza ziendelee
 
JK anavyopenda safari nisingetegemea kukosa hii trip.

Mkuu, kama umesoma vizuri hilo bandiko, JK alikuwa na ziara Mkoani mwanza. Haikuwa dhamira yake kwenda huko na ndo maana ameenda kampala bila ya kuthibitisha
 
Kagame nae aliwasili Uganda jana.

By John Odyek

President Paul Kagame of Rwanda is in Uganda to attend a meeting of regional heads of states geared at resolving violence in the DR Congo.

The heads of states and government of the International Conference on the Great Lakes region will, on 5th September 2013, hold the 7th Extraordinary Summit on security situation in the Eastern Democratic Republic of Congo in Kampala, Uganda.

The Summit will be preceded by parallel meetings on 4th September, 2013, of regional Ministers of Defence and Regional Inter-Ministerial Committee comprising of Ministers of Foreign Affairs from member states. All meetings will take place at Munyonyo Commonwealth Resort, Kampala, Uganda.

Member states of the International Conference on Great Lakes Region include; Angola, Burundi, Central African Republic, Republic of Congo, Democratic Republic of Congo, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudan, Tanzania and Zambia.


Source: newvision.co.ug
 
Ili kuwepo na Amani DRC, nawaomba UN wampe Ruhusa Rais Kikwete aongeze Battalioni kama mbili au 3 ili kutokomeza waasi wa M23 nikiwa na maana ya kwamba JWTZ lifike mpaka Kigali. Lazima tung'oe chanzo na si matawi, Shina na Mzao wa M23 ni kagame. Na huyu Kagame mbele JWTZ hafurukuti.
 
Back
Top Bottom