Pre GE2025 Katibu Mwenezi CCM Iringa awahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Pre GE2025 Katibu Mwenezi CCM Iringa awahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo mkoa wa Iringa Mwl. Joseph Ryata amewaomba Watanzania kujitokeza kujiandikisha kwenye zoezi la kupata vitambulisho vya Mpiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu mwakani 2025.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya walimu Makada wa CCM mkoani Songwe, Ryata alisema kuwa moja ya jukumu kubwa la walimu ni kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi wajitokeze kujiandikisha kwenye vitambulisho vya mpiga kura.

ccm ccm.png

Ryata alisema kuwa kila mwananchi ana haki ya kuhakikisha anajitokeza kupata kitambulisho cha mpiga kura ili katika uchaguzi ujao aweze kuchagua viongozi anaowataka kuwaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema kuwa mwananchi asipokuwa na kitambulisho cha mpiga kura hatakuwa na haki ya kupiga kura kwa kiongozi yoyote katika uchaguzi mkuu mwakani 2025.

Nao baadhi ya walimu Makada wa CCM mkoa Songwe walisema kuwa wapo tayari kuhakikisha wanatoa elimu kwa kila mwananchi kujitokeza kushiriki zoezi la kupata kitambulisho cha mpiga

Source: Kitenge TV
 
Back
Top Bottom