Katibu Mwenezi CCM Paul Makonda aagiza Taa barabarani Zifungwe Bwanga na amezuia kamatakamata ya wauza mikaa

Katibu Mwenezi CCM Paul Makonda aagiza Taa barabarani Zifungwe Bwanga na amezuia kamatakamata ya wauza mikaa

Hivi kazi ya Waziri mkuu au Rais ni ipi?. Maana mawaziri wote wanapokea maagizo kutoka kwa Katibu Mwenezi, akiwemo Waziri Mkuu aliyepewa miezi SITA na Makonda.
Hivi,japo wengine si wabobezi wa siasa,hiyo si dhalau? Inawezekana Makonda kumpa maagizo Kassim?
 
Huyo hajui mchakato wa kumpata mkandarasi? Kwamba apatikane ndani ya siku tano?

Kwamba REA iweke taa barabarani sio Tanroad?

Takataka kabisa
Si hapo nyuma ya pazia atakua ameshaanza safari ya kuja site,watakapoondoka na yeye atakuwa ameshamaliza saveyi
 
Ki itifaki ya chama, Katibu mkuu wa chama ndio mtendaji mkuu hivyo yeye angetoa maagizo ya utekelezaji wa ilani ya chama kisha mwenezi apite kutujulisha mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya chama.

Sasa kama yeye ndio kajipa/kapewa jukumu la kutoa maagizo ya utekelezaji, je ni nani atakayekuja kutupa taarifa ya utekelezaji wa ilani kwa mafanikio na kutushawishi tuendelee kukiweka chama chetu madarakani?!
 
Back
Top Bottom