Ki itifaki ya chama, Katibu mkuu wa chama ndio mtendaji mkuu hivyo yeye angetoa maagizo ya utekelezaji wa ilani ya chama kisha mwenezi apite kutujulisha mafanikio ya utekelezaji wa ilani ya chama.
Sasa kama yeye ndio kajipa/kapewa jukumu la kutoa maagizo ya utekelezaji, je ni nani atakayekuja kutupa taarifa ya utekelezaji wa ilani kwa mafanikio na kutushawishi tuendelee kukiweka chama chetu madarakani?!