TANZIA Katibu wa CCM Wilaya ya Rombo, Marry Sule, Afariki Dunia akipatiwa matibabu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Marry Sule amefariki dunia jana usiku Machi 18, 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Huruma.

Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku huohuo zikieleza kuwa Katibu huyo amefariki muda mfupi baada ya kutoka kwenye chumba cha upasuaji kwenye Hospitali ya Huruma, iliyopo wilayani humo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, Antony Tesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

"Nasikitika kutangaza kifo cha Katibu wa CCM Wilaya, ndugu Mary Sule kilichotokea jana usiku katika Hospitali ya Huruma alikokuwa akipatiwa matibabu,"imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rombo

Screenshot 2025-03-19 110042.png
 
RIP, nisali nimuombe Mungu aniambie ni kwa nini anapenda kuchukuwa watu wake karibu na uchaguzi?
 
R.I.P SG,

Mwenyezi Mungu akuweke mahali unapostahili, Aimen 🙏
 
Rip!

KAZI ya mungu Haina makosa kama ni Mungu kweli!

Kuna wimbi la viongozi wa ccm kutekwa na kufa hapo mwanzo lilivuma kiasi!tunashukuru kutulia walau!
Unatuambia Mungu ndio amefanya kazi ya kumuua? Maneno mengine muwe mnajitafakari kabla ya kusema, sio kukariri na kurudia tu.
 
RIP, nisali nimuombe Mungu aniambie ni kwa nini anapenda kuchukuwa watu wake karibu na uchaguzi?
Katiba yetu inampa kiburi mwenyekiti!!na kama Kuna kutoafikiana kuhusu mambo fulani hakuna namna ya kumwajibisha kisheria!
Ndio maana nyakati za uchaguzi mengi hutokea!!

Kumbuka viongozi wa Chama ndio wenye kumpigania mwenyekiti sasa unaweza kuona viongozi wa chama waliowengi ndio Rip zinawahusu kipindi hiki!!

Mungu atusaidie tuvuke salama!

Mungu ibariki Tanzania yetu tuipendayo sana!
 
Back
Top Bottom