Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
R.I.P SG,Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Marry Sule amefariki dunia jana usiku Machi 18, 2025 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Huruma.
Taarifa za kifo chake zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii usiku huohuo zikieleza kuwa Katibu huyo amefariki muda mfupi baada ya kutoka kwenye chumba cha upasuaji kwenye Hospitali ya Huruma, iliyopo wilayani humo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo, Antony Tesha amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.
"Nasikitika kutangaza kifo cha Katibu wa CCM Wilaya, ndugu Mary Sule kilichotokea jana usiku katika Hospitali ya Huruma alikokuwa akipatiwa matibabu,"imeeleza taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rombo
Unatuambia Mungu ndio amefanya kazi ya kumuua? Maneno mengine muwe mnajitafakari kabla ya kusema, sio kukariri na kurudia tu.Rip!
KAZI ya mungu Haina makosa kama ni Mungu kweli!
Kuna wimbi la viongozi wa ccm kutekwa na kufa hapo mwanzo lilivuma kiasi!tunashukuru kutulia walau!
Muumba ndio mwenye pumzi mkuu!!akitaka anaichukua ama lah!!Unatuambia Mungu ndio amefanya kazi ya kumuua? Maneno mengine muwe mnajitafakari kabla ya kusema, sio kukariri na kurudia tu.
Katiba yetu inampa kiburi mwenyekiti!!na kama Kuna kutoafikiana kuhusu mambo fulani hakuna namna ya kumwajibisha kisheria!RIP, nisali nimuombe Mungu aniambie ni kwa nini anapenda kuchukuwa watu wake karibu na uchaguzi?