Katibu wa CWT adai ana Mkataba wa Ajira ya Kudumu katika Chama cha Walimu Tanzania

Katibu wa CWT adai ana Mkataba wa Ajira ya Kudumu katika Chama cha Walimu Tanzania

Huyo fala amechanganyikiwa, hicho kinachoitwa mkataba amejitengenezea mwenyewe. Kwanza hana akili hata ya kuazimwa, yaani sisimizi km hilo ni la kushindana na serikali? Hakuna rangi hataona
Mamamae zake maganga hivi hii CWT ni ya baba ake??Empesiree
 
Teuzi za ovyo za bi chaudele mtu wa kawaida mwenye akili timamu anapaswa kuzikataa bila kufanyiwa mizengwe yoyote! Serikali ya ovyo sana hii!
 
Kufuatia taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke iliyotolewa na Mkurugenzi Elihuruma Mabelya ikielezea kuhusu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Mwalimu Japhet Maganga, ambaye alikuwa ni mwalimu wa Shule ya Msingi Tandika ya Wilayani Temeke, kumezuka maswali iwapo ataendelea kusalia katika uongozi wa CWT au la.

Mwalimu Japheth Maganga ameulizwa kuwa uamuzi wa kumsimamisha kama utamfanya akose sifa ya kuwa Katibu Mkuu wa CWT?

Akijibu maswali ya Waandishi wa Habari, Mwalimu Maganga amenukuu Ibara zilizopo ndani ya Katiba ya CWT akisema yeye ana mkataba wa kudumu wa ajira ya CWT, hivyo ni Mtumishi wa CWT na hata wakati anagombea nafasi aliyonayo hivi sasa alitokea makao makuu ya CWT kama Mhasibu.

Mwalimu Maganga ameendelea kwa kusema kuwa, kwa muujibu wa Katiba ya CWT, Toleo la Mwaka 2014 bado anazo sifa za kuwa Mwanachama wa CWT, hivyo uhalali wa yeye kuendelea na nafasi yake ya sasa hautakoma baada ya kusimamishwa kazi.

"Niliajiriwa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kama mhasibu Januari 1, 2018. Niligombea nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT nikitokea Idara ya Uhasibu CWT- Makao Makuu na si Halmashauri kama ambavyo wengi wanadhani," anasema.

Mwalimu Maganga ameongeza kuwa, kwa mujibu wa Ktiba ya CWT Toleo la Mwaka 2014 ana haki ya kugombea nafasi ya yoyote ndani ya CWT.

"Kwa mujibu wa Ibara ya 6.4 ya Katiba ya CWT ya Mwaka 2014, mimi ni mwanachama maalum na nina haki ya kugombea nafasi yoyote ndani ya CWT, Ibara ya 30 (e) ya Katiba ya inathibitisha hilo."

Itakumbukwa kupitia mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa Desemba 16, 2022 ulimthibitisha kuwa Katibu Mkuu wa CWT.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa kisheria wa kuendelea kusalia madarakani kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa CWT anautoa wapi ikiwa tayari ameshasimamishwa kazi, Mwalimu Maganga amesema:

"Nina haki ya kuendelea kuwa Katibu Mkuu wa CWT kwa mujibu wa Katiba ya CWT Ibara ya 30 (e) Toleo la Mwaka 2014."

Taarifa iliyotolewa Alhamis Desemba 7, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya imeeleza Mwalimu Maganga amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za utoro kazini na kukaidi au kukataa maelekezo halali ya viongozi.

Pia soma
= Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa tuhuma za utoro kazini na kukaidi maelekezo ya viongozi wake
= Katibu mkuu CWT asimamishwa, ni yule aliyekataa uteuzi wa Rais Samia
Yeye sio wa kwanza kupambania ulaji CWT na kafanikiwa. Ngoja tusubiri tuone.
 
Ili uweze kumshinda Maganga yakupasa kurejea kwenye Katiba ya CWT sio porojo kama zako! Kumshinda inabidi ulete Katiba au sheria aliyovunja ila inaonekana mnataka kumfanyia figisu ndiyo maana mnaangaika kupita mipenyoni ili mumuangushe tu
Mwenyewe anakiri alikuwa anaomba kibali kwa mwajiri wake ili kutumikia nafasi kwenye CWT.

Sasa mara ya mwisho amekataliwa kibali cha kuendelea kuitumikia CWT akaamrishwa arejee kazini kwake kama mwalimu ambayo ndiyo ajira yake ya kudumu aliyoajiriwa.

Huoni kukaidi kurejea kazini kwa maelekezo halali ya mwajiri wako ni kuvunja sheria za utumishi wa umma pamoja na sheria za kazi?
 
Huyo fala amechanganyikiwa, hicho kinachoitwa mkataba amejitengenezea mwenyewe. Kwanza hana akili hata ya kuazimwa, yaani sisimizi km hilo ni la kushindana na serikali? Hakuna rangi hataona
Mjibu kwa vifungu mkuu..matusi ya nini
 
Safi sana maganga go go go

Walete amshaamsha haoooo

Jamaa mbishi [emoji1]

Ova
 
Sasa yeye hayaji kurudi kufundisha, sisini Nani tumlazimishe akafundishe?
Ukiona anabisha kiasi like ujue anayo option nyingine.
Plan B muhimu.
Kwanza alisha ajiriwa Kama muhasibu huenda anayo taaluma hiyo ataenda taasisi binafsi.
Kama anayo taaluma anang'ang'ania nini CWT?
 
Huyo fala amechanganyikiwa, hicho kinachoitwa mkataba amejitengenezea mwenyewe. Kwanza hana akili hata ya kuazimwa, yaani sisimizi km hilo ni la kushindana na serikali? Hakuna rangi hataona
Vipi kwani! Mbona kama kachukua nafasi yako aise?!
 
Back
Top Bottom