Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu adai walimu ndio wanalipwa mishahara mizuri kuliko mtumishi yeyote Serikalini

Acha uongo bingwa, mshahara wa mwalimu mwenye Degree haulingani hata kidogo na mshahara wa mtu mwenye diploma fani yoyote alieajiriwa kwenye baadhi ya mashirika kama TAWIRI, TPA, REA, TANAPA na kwingineko.

Hivyo, kama huna data ni busara kutokuchangia!
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kiuhalisia ukichukua watumishi wa kada nyingi serikalini hasa serikali kuu wenye elimu inayofanana na walimu mfano wote degree utakuta walimu wanaanza na salary kubwa kuliko watumishi wengine.
Tofauti inakuja kwenye marupurupu na mazingira ya kufanyia kazi
 
Achana na walioko kwenye wakala na taasisi za serikali zinazojitegemea, hapa wanazungumzwa watumishi wa serikali kuu kwenye mawizara Hadi kwenye Halmashauri ambao ndio wengi.

Huko kwingine ulikotaja kuna watumishi wachache sana na wako kwenye kazi maalumu
 
Ok, nimekupata mkuu, shukrani
 
Kwani ni uongo...GDP ya bakhresa tu sio sawa na ya Shinyanga+Tabora??
 
Ila walimu ni walalamishi aisee utasema ndo waajiriwa tu nchi hii[emoji3]

Acha ujinga wako. Mshahara wa mwalimu unaujua? Walimu wangapi nchi hii wenye uwezo wa kutumia mshahara wao na kujiwekea akiba? Unapopata mshahara wa chini ya milioni moja unasema una mshahara mkubwa? Chini ya Dola 430!!! Wakati Rais juzi amesema watu wanalipwa zaidi ya milioni 15, sawa na dola zaidi ya 6500, kwa nini walimu wasilalamike?

Kazi ya ualimu ni ya kutukuka sana wangepaswa Kulipwa wala 2,300,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na dolla 1000 tu, maisha yao yangabadilika
 
Wambie wakafanye hizo kazi za milioni 15 hawawezi wapige chini kazi waka bet
 
Wambie wakafanye hizo kazi za milioni 15 hawawezi wapige chini kazi waka bet

Fikiria kabla ya kuandika, wakipiga chini ukoo wako utaingia madarasani?? Siku walimu wataamua kugoma ndiyo mtaujua umuhimu wao!!
 
Fikiria kabla ya kuandika, wakipiga chini ukoo wako utaingia madarasani?? Siku walimu wataamua kugoma ndiyo mtaujua umuhimu wao!!
Kama maslahi hayawatoshi kutwa wanalia na kugoma pia hawawezi si upuuzi? Chagueni moja muache kulia kila siku mchape kazi au muache kazi..
 
Kama maslahi hayawatoshi kutwa wanalia na kugoma pia hawawezi si upuuzi? Chagueni moja muache kulia kila siku mchape kazi au muache kazi..
Haahaa kwa wema walioufanya walimu mwaka huu kwa jpm hawakupaswa kudhalilishwa hivi
 
Mkuu Kama hujui Mambo kaa kimya...
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote....
Afisa yupo sawa. Huo ndo ukweli ukiajiriwa leo na degree, mwalimu mwenye degree atakuzidi mshahara. Shida ya mwalimu wengi hawana posho zaidi ya mshahara tu.
 
Kama maslahi hayawatoshi kutwa wanalia na kugoma pia hawawezi si upuuzi? Chagueni moja muache kulia kila siku mchape kazi au muache kazi..

Wenye busara Mara nyingi hujadiliana kuondoa changamoto. Aside na busara anadhani akifukuza ataajiri wengine. Kazi ya ualimu inasadikika ati kila mtu anaiweza, lakini huo ni uongo. Inamchukua mwalimu muda mrefu kumfanya nguli.

Tatizo sio kuacha kazi, bali ni ku reason na watawala waone umuhimu we kuwaongezea mshahara walimu. Ujerumani ndiyo nchi pekee inayowalipa walimu mshahara wa kutosha na sababu ni rahisi.

Walimu ndiyo wanaotengeneza skills za wafanyakazi wengine wote. Hata wewe unayewabeza ni product ya walimu wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…