Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu adai walimu ndio wanalipwa mishahara mizuri kuliko mtumishi yeyote Serikalini

Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu adai walimu ndio wanalipwa mishahara mizuri kuliko mtumishi yeyote Serikalini

Acha ujinga wako. Mshahara wa mwalimu unaujua? Walimu wangapi nchi hii wenye uwezo wa kutumia mshahara wao na kujiwekea akiba? Unapopata mshahara wa chini ya milioni moja unasema una mshahara mkubwa? Chini ya Dola 430!!! Wakati Rais juzi amesema watu wanalipwa zaidi ya milioni 15, sawa na dola zaidi ya 6500, kwa nini walimu wasilalamike?

Kazi ya ualimu ni ya kutukuka sana wangepaswa Kulipwa wala 2,300,000 kwa mwezi ambazo ni sawa na dolla 1000 tu, maisha yao yangabadilika

Badala yake wanalipwa 756,000 na kuonekana mishahara yao mikubwa!
 
Kwanini analaumiwa huyu jamaa mbona kasema ukweli? Anasema walimu wanalipwa mshahara mkubwa kuliko watumishi wengine wa level ile ile.

Mfano, watu waliosoma na wakamaliza pamoja degree, mmoja akaajiriwa ualimu TGTS D na mwingine akawa Afisa Ustawi wa Jamii TGS D. Mwalimu mwenye TGTS D anamshahara mkubwa kuliko Afisa Ustawi wa jamii mwenye TGS D. Be informed
hapo ulipo sema ni sawa maana hao wote nazini wamesoma 3 yrs degree ila kuna IT wa kompyuta sayansi 3 yrs anaanza TGS E na ambayo ni kubwa kuliko TGTS D
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.

Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.

========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

View attachment 1657898

Wabunge Wanapishana Majukwaani Kutaka Vijana Wajiajiri Hali yakua, Bunge Hili Hilo Lilipitisha Malipo Ya
1. YouTube-1,100,000
2. Blog-1,100,000
3. Mafunzo Ya Drone-1,980,000

Hivi kweli Mna dhamira Ya Kutaka Vijana Wajiajiri au madish huwa yakiyumba mnaropoka chochote.
Hivi Kijana Wa Kitanzania mwanaccm aliyekosa kibarua cha kujibu hoja za wapinzani anatoa Wapi Hizi Fedha?
Busara na majivuno havikai nyumba moja.
 
Nchi ambayo haitambui na haijui umuhimu wa elimu ambayo viongozi wake pamoja na wananchi wake ni hii Tanzania. Hata ukifuatilia michango inavyotolewa humu kuna watu wako hum mchango wa waalim hawauoni wanaona hakuna kazi wanayoifanya.Yote hayo ni laana tuliyonayo sisi watanzania na Afrika kwa ujumla.Hauwezi ukawa unawabeza waalim alafu usivyo na akili unawapeleka wanao shule baadala ya kukaa nao ukawafundisha mwenyewe.

Serikali ya Tanzania viongozi wake hawana huruma na watoto wa watanzania ambao ni maskini ndoo maana wanatamka maneno ya ajabu ,kwa kuwa wanajua hawa walimu hata wakitoa product iliyo mbovu haiwahusu.

Mwalimu mwenye degree anaanza na TGTS D ambayo 756,000, wakati mhasibu, engener,mwanasheria ,Dactari wote wanaanza na TGTS E ambayo 995,000, na hao wana posho za sermina na marupu rupu mengine.

Tiliwahi kuuliza swali hilo kwa viongozi wa juu kuna kipindi walikuja kituyembelea kuhusiana na kupishana kwaishahara walitujibu kuwa hakuna mtu asiependwa walim walipwe vizuri bali nusu nzima ya watumishi wa umma ni waalim ,kwahiyo serilali haiwezi kwa sababu nchi haina pesa ni maskini.

Mapendekezo yalitolewa angalau serikali itoe pesa ya posho kwa asilimia 50% waalimu wa masomo ya sayansi na 40% kwa masomo ya sanaa lakini bado serikali ilishindwa.

Nadhani serikali kipaumbele cha elimu kwao ni option hakina umuhim sana ndoo maana wanashindwa kubadili ,mifumo ya elimu na mambo mengne.

Waalim wanaendelea kubaki wakilalamika na kukata tamaa huku wakitoa product mbaya sana.Leo tunawfanyia mitihani drs 7 ili mradi aende huko likutoke ,leo mwalim hana mpango na wanafunzi amefaulu ahajafaulu ,au ameelewa au hajaelewa ila tutaumia wananchi wote baada ya miaka 15 au 20 ijayo.

Mwenye akili timam asingeshangilia au kukejeli kuhusiana na maslahi ya waalim ,angetamani hata kuandamana ili kila siku anako mpeleka mwane apate maarifa lakini ni uozo.

Ni kweli mshahara haujwahi kutosha lakini akipata posho tarehe 15 au 10 mshahara alioupta utatosha baadhi ya matatizo yatapungua.Mwenye degree ukimlipa huo mshahara anabaki 480,000/= baada ya makato yote sasa itamtosha nini? Lakini akipata posho 250,000/= kati kati ya mwezi mambo yataenda bambam.
 
Ni sahihi kwa maana ya rank, yaani Mfanyakazi mwingine kutoa madaktari na wanasheria. Mshahara wa kuanzia wa Mwal ni mkubwa.

Lakini swali linakuja mkubwa wa kukidhi mahitaji kulingana na hali ya maisha na mfumuko wa bei wa Mara kwa Mara? Jibu ni hapana
Na tena hawana no hatuna safari za kikazi wala warsha kwa kipindi chote cha mwaka! zaidi sana kwenda kusahihisha mitihani na kulipwa per script!! na hapo ukitoka na laki nne kwa kazi ya siku zaidi ya 20, unashukuru Mungu.
 
Tusubiri kauli ya katibu mkuu na uongozi mzima wa CWT ambao ndo wanapokea michango kutoka kwa waalimu kwa ajili ya kuwatetea.
Endapo watakaa kimya,basi kuna mawili
1. Ni kweli waalimu wanalipwa vizuri.
2. Chama cha waalimu hakipo kwa maslahi ya waalimu,ni steping stone ya maisha yao wenyewe.
 
Ila kuna kitu hapa hakipo sawa. Suala la mishahara kwa Walimu ni kuwadhihaki. ELIMU wanalipwa tgts d kwenye degree sawa na wengine tu ukiacha madaktari, ARDHI na wanasheria.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.

Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.

========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

View attachment 1657898

Kuzungumza tu bila kuweka data (takwimu) ni kufanya siasa kwenye ishu muhimu inayohusu maisha ya watu...

Walimu wako wa viwango tofauti tofauti vya elimu. Kutolea mwalimu mwenye shahada (digrii) ya chuo kikuu ni kugusa kwa kiasi kidogo sana jambo hili...

Ninavyofahamu mimi kuhusu mishahara ya kada ya ualimu iko hivi;

1. Mwalimu wa ASTASHAHADA (cheti) anapoajiriwa anaanza na mshahara [Gross Net Pay) ya TGTS. B. hauzidi 400,000/= mpaka sasa...

2. Mwalimu wa STASHAHADA (Diploma) akiajiriwa leo, ataanza na Mshahara [Gross Net Pay) ya TGTS. C. ambao hauzidi Tshs. 540,000/= mpaka sasa...

3. Mwalimu mwenye SHAHADA (Digrii) akiajiriwa leo, ataanza na mshahara [Gross Net Pay] ya TGTS. D. ambao hauzidi Tshs. 716,000/= mpaka sasa...

## Sasa tunaweza kujadili kwa kujiuliza maswali kadhaa kama haya:

å Kwamba, ni kigezo gani tunaweza kukitumia kujua huyu ana mshahara mkubwa huyu mdogo?

å Hebu tena tujiulize swali hili muhimu na la msingi sana, kwamba, kwanini mtu anayefanya kazi ni sharti alipwe ujira wake?

JIBU: Ni kwa sababu imeandikwa asiyefanya kazi basi NA ASILE CHAKULA...!!

å Kumbe tunafanya kazi ili TULE CHAKULA. Kama ndivyo hivi, iweje kuwe na tofauti ya malipo kwa watu wanaofanya kazi ileile moja ya ualimu? Mwingine 400,000; mwingine 500,000 na mwingine 700,000? Je, hawa wanakwenda masoko tofauti ya kununulia chakula?

å Swali la mwisho ni hili:

Je, si kwamba kigezo kikuu cha "UKUBWA WA MSHAHARA" wa mtu kinatakiwa kiwe ni kukidhi kwa mahitaji muhimu (chakula, bills mbalimbali, mavazi na malipo ya nyumba) kwa mfanyakazi na familia take ya watu sita (mume + mke + 4 children)??

Je, huyu naibu katibu ametumia kigezo hiki kutoa tamko lake hilo?

SI KWELI, BINAFSI SIKUBALIANI na huyu kiongozi. Jamaa huyu anapiga siasa tu hapa zinazomnufaisha yeye na viongozi wenzake kwa gharama ya walimu...!!!
 
unataka kusema jamaa katuongopea?
Huo uwongo hauhitaji kuwa na elimu ya chuo kikuu kuujua, swali rahisi aulizwe chukua wote wenye degree za kwanza kwa mwalimu, mhasibu, daktari na mhandisi aulizwe viwango vyao vya mshahara. Tungejua nani analipwa zaidi. Walimu ni kundi kubwa lenye watumishi wengi na ndio linaloongozwa kulipwa duni.
 
Yaani huyu Katibu bure kabisa, sijui anamdanganya nani na kwa maslahi ya nani?

Hata kama hujui hesabu unajua kabisa kwamba TGS D anayoanza nayo Mwalimu mwenye bachelor ni ndogo kuliko TGS E anayoanza nayo Land Surveyor, au Engineer aliyeajiriwa na Halmashauri.

You can't fool all the people all the time. Poor him
Kiukweli huyu katibu kadanganya Sana huwezi fananisha mshahara wa mwenye diploma ya uhasibu na diploma ya uwalimu. Diploma ya uhasibu iko juu kimshahara
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.

Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.

========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

View attachment 1657898

Huyu ni kiongozi katika Taifa la TANZANIA AU SOMALIA? Ni hatari kuwa na kiongozi anayeweza kusema uongo hadharani bila kujali chochote. Viongozi walioko juu yake wawe makini ama sivyo wataishia kupewa ripoti za kupotosha muda
 
Back
Top Bottom