Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.
Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.
Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.
========
MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.
Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?
Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.
MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?
MOSES CHITAMA: Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.
View attachment 1657898
Kuzungumza tu bila kuweka data (takwimu) ni kufanya siasa kwenye ishu muhimu inayohusu maisha ya watu...
Walimu wako wa viwango tofauti tofauti vya elimu. Kutolea mwalimu mwenye shahada (digrii) ya chuo kikuu ni kugusa kwa kiasi kidogo sana jambo hili...
Ninavyofahamu mimi kuhusu mishahara ya kada ya ualimu iko hivi;
1. Mwalimu wa ASTASHAHADA (cheti) anapoajiriwa anaanza na mshahara [Gross Net Pay) ya TGTS. B. hauzidi 400,000/= mpaka sasa...
2. Mwalimu wa STASHAHADA (Diploma) akiajiriwa leo, ataanza na Mshahara [Gross Net Pay) ya TGTS. C. ambao hauzidi Tshs. 540,000/= mpaka sasa...
3. Mwalimu mwenye SHAHADA (Digrii) akiajiriwa leo, ataanza na mshahara [Gross Net Pay] ya TGTS. D. ambao hauzidi Tshs. 716,000/= mpaka sasa...
## Sasa tunaweza kujadili kwa kujiuliza maswali kadhaa kama haya:
å Kwamba, ni kigezo gani tunaweza kukitumia kujua huyu ana mshahara mkubwa huyu mdogo?
å Hebu tena tujiulize swali hili muhimu na la msingi sana, kwamba, kwanini mtu anayefanya kazi ni sharti alipwe ujira wake?
JIBU: Ni kwa sababu imeandikwa asiyefanya kazi basi NA ASILE CHAKULA...!!
å Kumbe tunafanya kazi ili TULE CHAKULA. Kama ndivyo hivi, iweje kuwe na tofauti ya malipo kwa watu wanaofanya kazi ileile moja ya ualimu? Mwingine 400,000; mwingine 500,000 na mwingine 700,000? Je, hawa wanakwenda masoko tofauti ya kununulia chakula?
å Swali la mwisho ni hili:
Je, si kwamba kigezo kikuu cha "UKUBWA WA MSHAHARA" wa mtu kinatakiwa kiwe ni kukidhi kwa mahitaji muhimu (chakula, bills mbalimbali, mavazi na malipo ya nyumba) kwa mfanyakazi na familia take ya watu sita (mume + mke + 4 children)??
Je, huyu naibu katibu ametumia kigezo hiki kutoa tamko lake hilo?
SI KWELI, BINAFSI SIKUBALIANI na huyu kiongozi. Jamaa huyu anapiga siasa tu hapa zinazomnufaisha yeye na viongozi wenzake kwa gharama ya walimu...!!!