Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu adai walimu ndio wanalipwa mishahara mizuri kuliko mtumishi yeyote Serikalini

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kiuhalisia ukichukua watumishi wa kada nyingi serikalini hasa serikali kuu wenye elimu inayofanana na walimu mfano wote degree utakuta walimu wanaanza na salary kubwa kuliko watumishi wengine.
Tofauti inakuja kwenye marupurupu na mazingira ya kufanyia kazi
Hiki ndio nachokijua pia na ndio huyo jamaa alichokimaanisha
 
Wenye busara Mara nyingi hujadiliana kuondoa changamoto. Aside na busara anadhani akifukuza ataajiri wengine. Kazi ya ualimu inasadikika ati kila mtu anaiweza, lakini huo ni uongo. Inamchukua mwalimu muda mrefu kumfanya nguli. Tatizo sio kuacha kazi, bali ni ku reason na watawala waone umuhimu we kuwaongezea mshahara walimu. Ujerumani ndiyo nchi pekee inayowalipa walimu mshahara wa kutosha na sababu ni rahisi. Walimu ndiyo wanaotengeneza skills za wafanyakazi wengine wote. Hata wewe unayewabeza ni product ya walimu wako
Piga siasa jukwaa ni lako
 
"Katika watu wenye mishahara mizuri ni walimu, walimu ndio wanalipwa vizuri kuliko mtumishi yeyote wa serikali. Walimu wana mishahara mikubwa".

Hayo yamesemwa na MOSES CHITAMA ambaye ni katibu ofisi ya Rais tume ya utumishi wa walimu.

Chanzo cha habari: East africa tv plus+

===========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

Umeshindwa kupandisha hata kavideo?

Haya nimekusaidia hapo chini..ila ukimwangalia huyo jamaa suti aliyovaa inaeleza mengi namna alivyo na njaa.
 
"Katika watu wenye mishahara mizuri ni walimu, walimu ndio wanalipwa vizuri kuliko mtumishi yeyote wa serikali. Walimu wana mishahara mikubwa".

Hayo yamesemwa na MOSES CHITAMA ambaye ni katibu ofisi ya Rais tume ya utumishi wa walimu.

Chanzo cha habari: East africa tv plus+
Ngoja Nikae siti ya mbele kabisa
 
"Katika watu wenye mishahara mizuri ni walimu, walimu ndio wanalipwa vizuri kuliko mtumishi yeyote wa serikali. Walimu wana mishahara mikubwa"...
Yaani huyu Katibu bure kabisa, sijui anamdanganya nani na kwa maslahi ya nani?

Hata kama hujui hesabu unajua kabisa kwamba TGS D anayoanza nayo Mwalimu mwenye bachelor ni ndogo kuliko TGS E anayoanza nayo Land Surveyor, au Engineer aliyeajiriwa na Halmashauri.

You can't fool all the people all the time. Poor him
 
Afisa yupo sawa. Huo ndo ukweli ukiajiriwa leo na degree,mwalimu mwenye degree atakuzidi mshahara. Shida ya mwalimu wengi hawana posho posho zaidi ya mshahara tu.
Sio kweli Mkuu, mshahara wa Mwalimu mwenye Bachelor anayeanza kazi ni mdogo ukilinganisha na kada nyingine wanapoanza kazi.

Kwa level ya Halmashauri Mwalimu anaanza na TGS D, wakati maafisa ardhi, wakadiria ujenzi au Wanasheria wanaanza na E. Kwahiyo anachokisema huyo Naibu Katibu Mkuu sio kweli.

Vinginevyo kwa kuwa Walimu wenyewe tunao hapa Jamvini waje waseme ukweli.
 
Yaani huyu Katibu bure kabisa, sijui anamdanganya nani na kwa maslahi ya nani?

Hata kama hujui hesabu unajua kabisa kwamba TGS D anayoanza nayo Mwalimu mwenye bachelor ni ndogo kuliko TGS E anayoanza nayo Land Surveyor, au Engineer aliyeajiriwa na Halmashauri.

You can't fool all the people all the time. Poor him

Kwakuwa yeye analipwa mshahara mkubwa na marupu rupu juu basi anaamini kila mwalimu analipwa hivyo hivyo..

Ama kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa..
 
"Katika watu wenye mishahara mizuri ni walimu, walimu ndio wanalipwa vizuri kuliko mtumishi yeyote wa serikali. Walimu wana mishahara mikubwa".

Hayo yamesemwa na MOSES CHITAMA ambaye ni katibu ofisi ya Rais tume ya utumishi wa walimu...
Kwanini analaumiwa huyu jamaa mbona kasema ukweli? Anasema walimu wanalipwa mshahara mkubwa kuliko watumishi wengine wa level ile ile.

Mfano, watu waliosoma na wakamaliza pamoja degree, mmoja akaajiriwa ualimu TGTS D na mwingine akawa Afisa Ustawi wa Jamii TGS D. Mwalimu mwenye TGTS D anamshahara mkubwa kuliko Afisa Ustawi wa jamii mwenye TGS D. Be informed
 
"Katika watu wenye mishahara mizuri ni walimu, walimu ndio wanalipwa vizuri kuliko mtumishi yeyote wa serikali. Walimu wana mishahara mikubwa".

Hayo yamesemwa na MOSES CHITAMA ambaye ni katibu ofisi ya Rais tume ya utumishi wa walimu...
Sawa na watumishi wa TCRA, tanroads,tcaa,TPA, tra,Hazina,latra, tasac Wasemeje.?? Sekta ya Afya bado. Kama ni kweli Baridi Chuo niwe Mwalimu
 
Tatizo hawana safari, OT,pesa ya likizo,wala pesa ya unifomu
 
Ni sahihi kwa maana ya rank, yaani Mfanyakazi mwingine kutoa madaktari na wanasheria. Mshahara wa kuanzia wa Mwal ni mkubwa.

Lakini swali linakuja mkubwa wa kukidhi mahitaji kulingana na hali ya maisha na mfumuko wa bei wa Mara kwa Mara? Jibu ni hapana
nawe hujui kaa kimya MWANASHERIA MSHAHARA WAKE NI WAKAWAIDA TU HAWEZI MZIDI MHANDISI YEYOTE. HATA MHASIBU.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] kiuhalisia ukichukua watumishi wa kada nyingi serikalini hasa serikali kuu wenye elimu inayofanana na walimu mfano wote degree utakuta walimu wanaanza na salary kubwa kuliko watumishi wengine.
Tofauti inakuja kwenye marupurupu na mazingira ya kufanyia kazi
Unajua Mhandisi anaanza shilingi ngapi afu unajua maana ya serikali kuu?
 
Napenda Kumpongeza Sana Sana
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Kuwalipa Vizuri Sana Walimu Mpaka Sasa Hivi Wanafurahi

Baadaye Tutachapa Kazi Tu
😀😁😂🤣😃😄😅😅😄😃🤣😂😀😀
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.

Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.

========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

View attachment 1657898

Attachments

  • VID-20201210-WA0002.mp4
    11.8 MB
Back
Top Bottom