Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu adai walimu ndio wanalipwa mishahara mizuri kuliko mtumishi yeyote Serikalini

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.

Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.

========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

View attachment 1657898

Qnet pesa ipo hukuuu njooni msikieee
 
Ulipaji wa mishahara ya serikali pia inategemea chuoni ulisoma miaka mingapi.
Haiwezekani mwalimu aliyesoma miaka mitatu alipwe sawa na mwanasheria au daktari aliyesoma miaka mitano hilo pia lazima tujue.

Tatizo la mishahara midogo sanasana liko kwa watumishi waliopo Tamisemi sababu chukulia walimu wote mmesoma kozi moja miaka mitatu lakini mwenzako akipangwa vyuo vya ualimu (ambavyo viko wizara ya elimu) anakuzidi daraja moja yeye anaanza na E wewe D.

Watu pia wanachanganya serikali kuu na mashirika ya umma ambayo yanajipangia mishahara yenyewe. Ila kwa mtumishi aliyesoma chuoni miaka mitatu siku wanaajiriwa mwalimu anakuwa na mshahara mkubwa zaidi ndicho alichomaanisha katibu. Kwa hiyo shida ni kwamba mishahara ya watumishi wote ni kidogo kwa ujumla wachache Sana Wana nafuu.
 
Hakuna mtumishi anayelipwa mshahara mkubwa serikalini
Daktari, mwalimu, mhasibu, mhandisi nk wote wanalipwa hela ya kujikimu tu
 
Ulipaji wa mishahara ya serikali pia inategemea chuoni ulisoma miaka mingapi.
Haiwezekani mwalimu aliyesoma miaka mitatu alipwe sawa na mwanasheria au daktari aliyesoma miaka mitano hilo pia lazima tujue.
Tatizo la mishahara midogo sanasana liko kwa watumishi waliopo Tamisemi sababu chukulia walimu wote mmesoma kozi moja miaka mitatu lakini mwenzako akipangwa vyuo vya ualimu (ambavyo viko wizara ya elimu) anakuzidi daraja moja yeye anaanza na E wewe D.
Watu pia wanachanganya serikali kuu na mashirika ya umma ambayo yanajipangia mishahara yenyewe.
Ila kwa mtumishi aliyesoma chuoni miaka mitatu siku wanaajiriwa mwalimu anakuwa na mshahara mkubwa zaidi ndicho alichomaanisha katibu.
Kwa hiyo shida ni kwamba mishahara ya watumishi wote ni kidogo kwa ujumla wachache Sana Wana nafuu.
Wewe ni mpotoshashaji, achana na muda wa kusoma chuoni. Chukulia mfano uhasibu kozi ya miaka mitatu, na uwalimu kozi ya miaka mitatu level ya degree mishahara ni tofauti. Tatizo la mishahara kwa watumishi wa umma ni ubaguzi level moja na nyingine ingawa level ya elimu ni ileile. Kiufupi huyu katibu kadanganya
 
Fikiria kabla ya kuandika, wakipiga chini ukoo wako utaingia madarasani?? Siku walimu wataamua kugoma ndiyo mtaujua umuhimu wao!!
Mkuu wewe kumbe Mwalimu mambo ya dollar na wewe wapi na wapi

Kuna mwalimu (sitaki kusema kama nilimwajiri) ila tulikuwa tunaganga njaa pamoja, juzi kaja likizo ananiambia amini usiamini braza nilipokuwa kwako nilikuwa napata hela nyingi kuliko nilivyoajiriwa, sema tu kule huwa napata ya pamoja na kwako nilikuwa napata kila siku.
Nilitaka nisimwamini ila nililazimika kumwamini kwa sababu hakuwahi kunidanganya hata siku moja alipokuwa pamoja nami.
 
Watumishi wowote wawe wa umma au wa sekta binafsi kwa nchi yetu hawawezi ishi kwa mshahara tu. Kwanza kodi (PAYE) ni kubwa sana kulinganisha na nchi zingine, kwa mantiki hiyo watumishi wanategemea posho(allowances) mbalimbali kulingana na mikataba na sheria za watumishi.

Walimu scales zao za mishahara (TGTS) ni tofauti na baadhi ya scales hasa TGS. Hata hivyo mwalimu halipwi posho yoyote ingawa anafanya kazi zaidi ya masaa 8 ambayo ndiyo masaa halali ya kufanya kazi kwa siku. Posho huwa hazikatwi kodi hivyo kuwapa unafuu kada zingine. Nimeshuhudia baadhi ya walimu wakijishughulisha na kazi ya kuendesha pikipiki (bodaboda) huku akiendelea na kazi yake ya ualimu.

Yuko darasani anafundisha akipigiwa simu na mteja anaacha chaki ubaoni anatoa excuse kwa wanafunzi kuwa kuna mtu amwone mara moja kumbe aenda piga boda halafu arudi baadae. Hii yote ni ili aweze kujikimu. Ni ukweli usiopingika kuwa ualimu sio deal kihivyo, vinginevyo watu wengi wangefanya juu chini wawe walimu kama vile wanavyofanya juu chini wafanye kazi hazina au TRA.
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.

Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.

========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

View attachment 1657898

Ni uoga au unafiki unamfanya asiseme kweli iliyo moyoni mwake. Hyati mwl.J.K Nyerere alitofautisha UJINGA na UPUMBAVU.
 
Kwahiyo Rais mawaziri, wabunge, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wilaya nk wanalipwa chini ya Laki 7?!
 
Kwani muhasibu anayeanza ka
Wewe ni mpotoshashaji, achana na muda wa kusoma chuoni.chukulia mfano uhasibu kozi ya miaka mitatu, na uwalimu kozi ya miaka mitatu level ya degree mishahara ni tofauti.Tatizo la mishahara kwa watumishi wa umma ni ubaguzi level moja na nyingine ingawa level ya elimu ni ileile.Kiufupi huyu katibu kadanganya
Kwani muhasibu anayeanza kazi halmashauri anaanza na shilingi ngapi?
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.

Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.

========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa nafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

View attachment 1657898

Ni kweli wanapata mishahara mikubwa ukiweka effective hours of work (masaa ya kazi) wanayofanya kwa mwaka toa siku shule zimefungwa n.k
Kuna ndugu yangu Mwalimu alinieleza hivyo hivyo
 
Ni sahihi kwa maana ya rank, yaani Mfanyakazi mwingine kutoa madaktari na wanasheria. Mshahara wa kuanzia wa Mwal ni mkubwa.

Lakini swali linakuja mkubwa wa kukidhi mahitaji kulingana na hali ya maisha na mfumuko wa bei wa Mara kwa Mara? Jibu ni hapana
Na mainjini unawaweka wapi mkuu?
 
Hiyo nafasi si amepewa kama peremende na bwana yule? Unataka aongee kinyume na bosi wake kesho ajikute jalalani?
 
Yaani huyu Katibu bure kabisa, sijui anamdanganya nani na kwa maslahi ya nani?

Hata kama hujui hesabu unajua kabisa kwamba TGS D anayoanza nayo Mwalimu mwenye bachelor ni ndogo kuliko TGS E anayoanza nayo Land Surveyor, au Engineer aliyeajiriwa na Halmashauri.

You can't fool all the people all the time. Poor him
Moja ya vigezo vinavyotumika kupanga mishahara serikalini ni degree yako umesoma miaka mingapi(kwa kesi ya degree). Mwalimu anasoma miaka mitatu, mshahara wake utaanza chini kulinganisha na mhandisi anayesoma miaka minne. Vivyo hivyo mhandisi atakua chini kulinganisha na daktari anayesoma miaka mitano. Pamoja na hayo yote mishahara ni midogo ukizingatia kazi kubwa inayofanywa na waalimu. Kazi ya walimu ni pamoja na kuisaidia CCM kushinda kila uchaguzi.
 
Huyu ameongelea kwa watumishi wa halmashauri na wizarani tu.
1. Mwalimu wa degree TGTS D1 = 716,000/=
2. Watumishi wengine wenye degree za miaka mitatu ukiondoa kilimo na computer ni TGS D1 = 710,000/=
Tofauti ni 6,000/= Hivyo mwalimu yuko juu.
ILA SASA:
Ukienda huko kwenye taasisi, mamlaka, wakala na mashirika huko ndio mwalimu hatii pua anaweza kukimbizwa hata na mpishi au mlinzi.
Hawa mishahara yao unakula kwa urefu wa kamba yako.
 
Back
Top Bottom