Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu adai walimu ndio wanalipwa mishahara mizuri kuliko mtumishi yeyote Serikalini

Katibu wa Tume ya Utumishi wa walimu adai walimu ndio wanalipwa mishahara mizuri kuliko mtumishi yeyote Serikalini

Moja ya vigezo vinavyotumika kupanga mishahara serikalini ni degree yako umesoma miaka mingapi(kwa kesi ya degree). Mwalimu anasoma miaka mitatu, mshahara wake utaanza chini kulinganisha na mhandisi anayesoma miaka minne. Vivyo hivyo mhandisi atakua chini kulinganisha na daktari anayesoma miaka mitano. Pamoja na hayo yote mishahara ni midogo ukizingatia kazi kubwa inayofanywa na waalimu. Kazi ya walimu ni pamoja na kuisaidia CCM kushinda kila uchaguzi.
Sio kweli mkuu mbona mhasibu anasoma miaka 3 na mwanasheria lakini mishahara yao ni mikubwa kuliko hao waalim ?
 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.

Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.

Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.

========

MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.

Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?

Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.

MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?

MOSES CHITAMA:
Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.

View attachment 1657898


Huyu jamaa anadanganya nani?ngoja walimu humu wamwumbue ili aaibike.
 
Back
Top Bottom