Katibu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba: Umeme unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu

Katibu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba: Umeme unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu

JPM alimfukuzaga kazi, huyu jamaa, Siku ya mwaka mpya,nikahisi alionewa,kumbe ilikuwa saizi yake
Huyo alikuwa ni mtu wa Lowassa wakati ule wa kampeni za kuelekea uchaguzi wa 2015. Ilikuwa ni lazima JPM amtimue kwa sababu hizo za kisiasa, alihisi jamaa anaifanyia fitina CCM.
 
Ulivyotoa mfano wa nyanya kwenye hoja ya UMEME ndo umeonyesha ujinga wako wote
Umeme unaweza hifadhi godown kama wateja huna mjinga wewe? Umeme na nyanya vinafanana

Unaungurumisha mashine za kuzalisha umeme mkubwa wa kutumia ndani ya nchi usiku na mchana na una umeme wako wa ziada hakuna mnunuzi na hauhifadhiwi godown si bora uuze tu kwa hasara uambulie chochote ?.
Kuliko upotee tu sababu mashine inayozalisha huo umeme wa ndani ya mchi unazalisha na ziada kubwa ambayo huna pa kuuza nje ya nchi

Akitokea mtu anataka kununua kwa bei.ndogo mno yake.atakaye yeye utamgomea kuwa ohh sitaki unipangie bei si atakuachia umeme wako kama ni chipsi kakaange ule mwenyewe

Ndio maana hata mali ghafi zetu wazungu hutupangia bei za madini,mazao.kama pamba ,korosho ,kahawq,Chai nk za kununua wakati sisi hatuwapangiii bei za finished products xao

Wanasema wazi kama unaona mali zako.na nattural resources zako za maana kula mwenyewe kaanga au choma hatununui

Tuone hizo dhahabu na madini yako na mazao yako ghafi utamuuzia nani? tu ki boycott kununua usitubabaishe
 
By Malisa GJ,

Kuhusu Kununua Umeme Nje kwa Mikoa ya Kaskazini.

Kwanza, ieleweke kuwa hili si jambo geni. Hii si mara ya kwanza kununua umeme nje ya nchi. Tunanunua umeme kutoka Zambia kwa ajili ya mkoa wa Rukwa, kutoka Uganda kwa ajili ya mkoa wa Kagera, na kutoka Kenya kwa ajili ya wilaya ya Mkinga, Tanga.

Pili, watanzania tunahoji kwanini tununue umeme nje wakati tuliambiwa bwawa la Nyerere likikamilika tutakuwa na umeme wa kutosha na tutaweza kuuza nje. Je, tulidanganywa?

Ili kujibu swali hilo ni muhimu kujua hali ya uzalishaji wa umeme nchini na vyanzo vyake. Vyanzo vya umeme wa maji (hydroelectric power plants) tulivyonavyo vina uwezo ufuatao:
  • Kidatu inazalisha 204 MW
  • Kihansi 180 MW
  • Mtera 80 MW
  • Hale (Tanga) 68 MW
  • Rusumo 80 MW
  • Julius Nyerere 2,115 MW
  • Nyumba ya Mungu 8 MW

Kwa hiyo, kupitia vyanzo vya maji tuna uwezo wa kuzalisha 2,735 MW. Mahitaji ya umeme nchini yanakadiriwa kuwa 2,200 MW. Hii ina maana kwamba tuna ziada ya karibu 500 MW ambazo tunaweza kuuza nje. Kwa hiyo hatujadanganywa. Umeme wa kuuza nje upo.

Sasa, kwanini tununue umeme nje wakati ndani tuna ziada? Jibu ni kwamba usafirishaji wa umeme unasababisha upotevu njiani. Kusafirisha umeme si sawa na kusafirisha mbaazi. Ukitoa mbaazi Moshi zikiwa 50Kgs, zikifika Dar zitakua hizohizo 50Kgs. Lakini kwa Umeme ni tofauti. Kadri unavyosafirisha umbali mrefu, ndivyo unavyopotea.

Je, kati ya Ethiopia na bwawa la Mwalimu Nyerere, wapi mbali? Kama tunahofia umeme ukisafirishwa kutoka bwawa la Nyerere hadi Arusha utapotea, je unaotoka Ethiopia si utapotea zaidi?

Jibu ni kwamba Tanzania haitahusika na usafirishaji wa umeme huo kutoka Ethiopia. Sisi tutahusika baada ya kuupokea Namanga. Kwa hiyo, kama ni usafirishaji, sisi tutaanzia Namanga kwenda Arusha. Kwahiyo pale Namanga tukipokea 100MWs tutazifikisha Arusha bila kupotea maana ni karibu.

Kwa lugha rahisi, ni sawa na kuwa na chanzo kipya cha umeme Namanga. Kwa hiyo ni ukweli kwamba kusafirisha umeme kutoka Namanga kwenda Arusha hakutakuwa na upotevu mkubwa njiani kama kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere kwenda Arusha. Hii ni logic ya kawaida ambayo hata mtoto mdogo anaelewa.

Ili tuweze kusafirisha umeme kutoka bwawa la Nyerere au Mtera hadi Arusha bila kupotea sana, inabidi tujenge vituo vya kupoozea njiani (substations) kama ile ya Lemuguru iliyopo Mateves Arusha, ambayo ilianza kujengwa 2019 imekamilika 2024 (miaka mitano) kwa gharama ya karibu bilioni 20. Kwa hiyo kuna suala la muda na gharama.

Je, umeme wa ziada unaozalishwa Tanzania utaenda wapi? Jibu ni kwamba Utauzwa nje ya nchi. Tayari Tanzania imesaini hati ya makubaliano (MoU) na Zambia na Rwanda kuziuzia umeme.

Je, kusafirisha umeme kwenda nchi hizo hakutafanya upotee njiani? Jibu ni kwamba umeme huo utauzwa kutoka vyanzo vya karibu, hivyo hakutakuwa na upotevu mkubwa. Kwa mfano, Rwanda watauziwa umeme kutoka Rusumo na Zambia watapokea umeme kutoka Kihansi ambapo upotevu hauwezi kuwa mkubwa kama kuutoa umeme Kihansi kwenda Arusha au Rusumo kwenda Arusha.

Utaratibu wa kuuziana umeme baina ya nchi na nchi sio jambo geni. Nchi za Afrika Mashariki zimeanzisha Eastern Africa Power Pool (EAPP) ili kuratibu biashara ya umeme na uunganishaji wa gridi kati ya nchi hizo.

Nchi za Ulaya wanayo European Network of Transmission System Operators for Electricity (ENTSO-E) ambayo inaunganisha nchi 35 za Ulaya. Kupitia ENTSO-E nchi inaweza kuuza na kununua umeme kutoka nchi jirani. Kwa mfano, Ujerumani inanunua umeme kutoka Ufaransa, Denmark, na Norway jumla ya 30,000 MW. Lakini Ujerumani hiyohiyo inauza umeme kwa Ufaransa, Austria, na Uholanzi ambao ni 60,000 MW.

Unaweza kujiuliza, kama Ujerumani inaweza kuzalisha umeme na kuuza nje ya nchi, kwanini tena inunue? Jibu ni kwamba inapunguza upotevu wa kusafirisha umeme kwa umbali mrefu ndani ya nchi. Kuliko kutoa umeme Munich na kuusafirisha hadi Humburg (kilomita karibu 800) ni bora wakanunua umeme Dernmark wakapeleka Humburg, halafu ule wanaozalisha Munich ukatumika miji ya jirani na mwingine wakauzia Austria.

Na Tanzania ndicho tulichofanya. Kuliko kutoa umeme Rusumo kuupeleka Kyela, ni bora ule wa Rusumo utumike Kigoma, Kagera, na Geita, halafu unaobaki tuwauzie Rwanda na Burundi. Halafu tununue umeme kutoka Malawi tupeleke Kyela. Tukifanya hivyo tutakua tumeokoa gharama za usafirishaji na upotevu wa umeme njiani.!
 
"Huo umeme wa Ethiopia tunanunua kwa senti za Marekani 0.077
Sintuliambiwa mahesabu yote yafanywe kwa Tanzania Shilings iweje tutajiwe sent za Marekani? Kwa nini hajataja bei ya Umeme tunazozalisha hapa nchini ( sijasikiliza clip)
 
Tukifanya hivyo tutakua tumeokoa gharama za usafirishaji na upotevu wa umeme njiani.!
How to Reduce Transmission Losses:
High-Voltage Transmission:

1. Using high-voltage transmission lines reduces the current required to transmit the same amount of power, minimizing losses due to resistance.

2. Line Optimization:
Installing lines with high-quality conductors can reduce resistance and improve energy transmission efficiency.

3. Optimized Transmission Line Path:
Shortening the distance of transmission lines or placing lines closer to load centers can help to reduce transmission losses.

4. Grid Modernization:
Upgrading the grid with smarter technology can help better manage the flow of power and reduce losses.
====
Kwa kawaida transmission losses kwenye line ni kati ya 8-14%. Lakini hapa tumeambiwa kwa 100 MW loss ni 17 MW why?
Je. Grid yetu tumeifanyia maboresho kama yalivyoorodheshwa hapo juu? Au tuliboresha mawasiliano ndani ya shirika ana wateja tu!?
 
Back
Top Bottom