Katibu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba: Umeme unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu

"Umeme utakaonunuliwa utakuwa na hasara, Lakini hiyo hasara haituhusu"🤔
Hapa kawatukana sana Wa Ethiopia kwamba hawana akili

Na kama sio kuwatukana basi kawaamsha!

Ila huyu Mramba aangalie sana mkataba watakaosaini. Kuna ile namna kwamba unaanza na bei poa.Tanzania ikishakuwa tegemezi na umeme wa Ethiopia ndio wanapandisha bei.
 
Wakuu,

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema uamuzi wa Tanzania kuchukua umeme Ethiopia ni kitu chenye faida na si hasara kama watu wanavyodhani.

Mramba amesema ni faida kwa kuwa baadhi ya vyanzo vya umeme hapa nchini vinazalisha uniti moja kwa bei kubwa kuliko bei ambayo umeme huo utanunuliwa kutoka Ethiopia.

"Huo umeme wa Ethiopia tunanunua kwa senti za Marekani 0.077 lakini tuna vyanzo vingi ambavyo vinazalisha kwa gharama ya juu zaidi, hivyo hii ni nafuu kwetu," amesema na kuongeza umeme utaonunuliwa Ethiopia ni Megawati 100 tu.

Amesema umeme unaopelekwa mikoa ya Kaskazini unapotea kwa kiwango cha megawati 17 ambazo zinatosha kuhudumia Mkoa wa Songwe (unaotumia Mega 14) na zaidi.

"Hata huo wetu unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu, sisi tunanunulia mpakani Namanga, lakini tukipeleka sisi (umeme) tunatumia gharama kubwa," amesema Mramba.
Ameongeza kuwa "wachumi na wataalamu wote waliofanya tathmini juu ya jambo hilo waliona ni faida kubwa kuliko hasara"

Aidha, Mramba alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ununuzi wa umeme huo na kuongeza kuwa ufafanuzi uliotolewa na Msemaji wa Serikali baada kuibuka kwa mjadala huo uko sahihi.

"Maelezo ya msemaji wa Serikali yako sawa, hayana dosari," amesema Mramba na kuongeza kuwa suala la mauziano ya umeme ya nchi na nchi ni la kawaida na mpaka sasa Tanzania inauza na kununua umeme kutoka mataifa tofauti zaidi ya matatu.

Source: Mwananchi
Inasikitisha sana. Nilikua kila siku najiuliza kwa nini vitu vile vile ambavyo vinazalishwa nchi zingine zikizalishwa kwetu ni bei mbaya? Hata zile ambazo huagizi raw material. Kuzalisha umeme Ethiopia na Kuzalisha umeme Tanzania tofauti ipo wapi? Kama ni vifaa na machine wote tunanunua nje. Je wao wamezalishaje umeme bei rahisi?
Jibu ni sisi Wandanganyika tuna-subsidize mafisadi wa CCM, kila kitu ni bei feki na hakiuziki kwa bei nzuri. Ethiopia hawawezi kuuza umeme kwa Hasara, siyo wajinga. Hiyo bei inawezekana wana faida, kusema wanapata Hasara ni uongo.

Angalia hata Barabara- sisi tunajenga hata Barabara kwa gharama za juu sana- kisa - tunapigwa. Ahsante Mramba kwa kutufunua macho.
 
serikali ijaribu kuwatafuta wataalam/wenye ujuzi na masuala ya umeme walieleze
VVizuri hii issue
Wasiwatumie wanasiasa,walipokaji kulizungumziaa maana wana bwabwaja tu na kuwaingiza watu kingi
inawezekana mpango ukawa ni mzuri tu ila uwasilishaji ukawa tofauti

ova
 
Ameongeza kuwa "wachumi na wataalamu wote waliofanya tathmini juu ya jambo hilo waliona ni faida kubwa kuliko hasara"
Huu ndio uhayawani wenyewe!
Hivyo vyanzo vyetu vya umeme ghali kuliko huo wa Ethiopia vitaacha kuzalisha umeme hapo wa Ethiopia utakapowasili?
Kama vyanzo hivyo havitazimwa, umeme huo utapelekwa wapi; na gharama zake atazilipa nani?

Hii mikoa ya Kaskazini, itaanza kujitenga na Tanzania na kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vyao na matumizi majumbani nafuu kuliko sisi wengine wote ndani ya nchi hii?

Basi iamliwe hivi: zima vyanzo vyetu vyote vya umeme wenye bei kubwa, na sote tufaidi huo wa $0.077 toka Ethiopia; au unasemaje Bwana Mramba?
Kwa bahati mbaya sana mikoa hii mara zote imekuwa kama wao siyo sehemu ya nchi hii, kwa namna moja au nyingine; kwa nini hasa?
 
Wewe ni mpumbavu na unatetea upumbavu!
.
Ethiopia ni waume zenu kwamba wakusafirishie nyie umeme wa bil. 10 kisha wauze kwa bil. 8 wale hasara ya bil. 2? Kwa vile mnawapa nini.?

Wapumbavu wakubwa nyie.
Hujui biashara wewe sasa angalia ramani ya Ethiopia kote anapakana na nani ? Kote anapakana na maadui sehemu pekee kwake kuuza umeme ni kenya kuja huku chini Tanzania

Jujui hesabu nikupe kirahisi mfano umeme anaozalisha nyanya pipa kumi anazotumia yeye pipa mbili ulitakaje sasa hizo pipa nane za nyanya zimuozee au auze hata kwa bei ya hasara kuliko kumuozea

Umeme anaozal8sha ni mwingi mno ameona heri auze kwa bei ya hasara kuliko.kutouza kabisa
 
Hii mikoa ya Kaskazini, itaanza kujitenga na Tanzania na kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vyao na matumizi majumbani nafuu kuliko sisi wengine wote ndani ya nchi hii?

Basi iamliwe hivi: zima vyanzo vyetu vyote vya umeme wenye bei kubwa, na sote tufaidi huo wa $0.077 toka Ethiopia; au unasemaje Bwana Mramba?
Kwa bahati mbaya sana mikoa hii mara zote imekuwa kama wao siyo sehemu ya nchi hii, kwa namna moja au nyingine; kwa nini hasa?
Hiyo Tanesco ni bei ya jumla ya kununulia umeme Ethiopia haina uhusiano na bei ya rejareja

Bei ya kuuzia umeme kwa wateja nchi nzima bei itakuwa ile ile uwe kaskazini au kusini
 
Sisi tuna vyanzo vinavyozalisha Kwa gharama za juu zaidi. Itabidi tafiti zifanyike wao Ethiopia wanatumia vyanzo Gani ili tujiulize hv na sisi hatukuweza kutumia vyanzo kama vyao ili tuzalishe Kwa gharama nafuu? Km vyanzo ni km vyetu kwann sisi ndani Kwa ndani tunatesana na kununua umeme Kwa gharama kubwa
 
Hiyo Tanesco ni bei ya jumla ya kununulia umeme Ethiopia haina uhusiano na bei ya rejareja

Bei ya kuuzia umeme kwa wateja nchi nzima bei itakuwa ile ile uwe kaskazini au kusini
Sawa sawa.
Tanesco hao hao bado wataendelea kuzalisha umeme aghali au siyo, umeme ambao hautakuwa na mnunuzi! Nafuu hapo kwa Tanesco yenyewe inatoka wapi?
 
Wakuu,

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema uamuzi wa Tanzania kuchukua umeme Ethiopia ni kitu chenye faida na si hasara kama watu wanavyodhani.

Mramba amesema ni faida kwa kuwa baadhi ya vyanzo vya umeme hapa nchini vinazalisha uniti moja kwa bei kubwa kuliko bei ambayo umeme huo utanunuliwa kutoka Ethiopia.

"Huo umeme wa Ethiopia tunanunua kwa senti za Marekani 0.077 lakini tuna vyanzo vingi ambavyo vinazalisha kwa gharama ya juu zaidi, hivyo hii ni nafuu kwetu," amesema na kuongeza umeme utaonunuliwa Ethiopia ni Megawati 100 tu.

Amesema umeme unaopelekwa mikoa ya Kaskazini unapotea kwa kiwango cha megawati 17 ambazo zinatosha kuhudumia Mkoa wa Songwe (unaotumia Mega 14) na zaidi.

"Hata huo wetu unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu, sisi tunanunulia mpakani Namanga, lakini tukipeleka sisi (umeme) tunatumia gharama kubwa," amesema Mramba.
Ameongeza kuwa "wachumi na wataalamu wote waliofanya tathmini juu ya jambo hilo waliona ni faida kubwa kuliko hasara"

Aidha, Mramba alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ununuzi wa umeme huo na kuongeza kuwa ufafanuzi uliotolewa na Msemaji wa Serikali baada kuibuka kwa mjadala huo uko sahihi.

"Maelezo ya msemaji wa Serikali yako sawa, hayana dosari," amesema Mramba na kuongeza kuwa suala la mauziano ya umeme ya nchi na nchi ni la kawaida na mpaka sasa Tanzania inauza na kununua umeme kutoka mataifa tofauti zaidi ya matatu.
Hiyo hasara ina maana mzalishaji(Ethiopia) ataifidia kwenye bei atakayokuuzia wewe( Tanzania). Hakuna anayefanya biashara ya hasara. Huu ujinga wajaribu kuupangilia upya.
 
Inaelekea watz wengi hawaiamini serikali yao wanajuwa hapa kuna upigaji tu 😄
Hebu TANESCO njooni na ufafanuzi mzuri kupitia wataalam haswa wafafanue hili jambo
msiwaachie wanasiasa sjui msigwa,machawa walisemee

ova
 
Ethiopia haitokubali kula hasara hapo kwenye hiyo biashara, ila nchi itakayokula hasara inajulikana ni Tanzania sababu ya vilaza kama huyu mhandisi.
 
Walau huyu Katibu Mkuu Mramba namwelewa.

Nilitaka kuanzisha mada nzito hasa kuwa Raisi awavurumishe wataalamu wa Tanesco waende Ethiopia wakajifunze kuwa wao kwa nini kilomita zote hizo toka Ethiopia umeme haupotei njiani na kuwapa loss ila wetu kilomita nyingi unapotea na kuipa Tanesco mabilioni ya hasara

Argument ya katibu mkuu ina make sense naikubali Ruksa kanunueni kwa muono wangu huo umeme wa Ethiopia

Katibu mkuu Mramba nimekuelewa
chawa pro , Pwani to Arusha , compare to Ethiopia to Tz , hii ni kukubali kuwa watumwa wa Kenya na Ethiopia , wakikoloma kidogo tunafyata .

MAMBO MENGINE HAYAHITAJI SIASA , MIKOA YOTE YA MPAKAN INATEGEA UMEME WA MAJIRAN. HV WENZETU WAMEWEZAJ SISI TUSHINDWE ?
AKILI ZA SERIKALI ZIPO DAR NA WAMETELEKEZA MIKOA YA MIPAKANI KBS
 
Sidhani kama umemuelewa.

Umeambiwa hasara ipo japo haituhusu sisi. Kwa maana hiyo suala la upotevu wa umeme njiani lipo hata kwa hao Ethiopia.

Sasa kama hasara ipo kwa Ethiopia basi hakuna faida ya wataalam wa Tanesco kwenda kujifunza huko Ethiopia kama ulivyopendekeza.
Kesho tuna mgogoro wa kisiasa na Ethiopia tunaanza ufyata .

KWAMBA JPM NA SAMIA WALIKUWA WEHU KUSEMA WATAZALISHA UMEME MPK WAUZE NJE

NCHI IMETEKWA MAAMUZ MENGI YAMEKAA KIJINGA SANA , KUNA NAMBA NCHI JIRANI YETU KAJIPENYEZA KTK SERIKALI YETU ,

ETHIOPIA ANAWEZAJ UTOA UMEME ETHIOPIA MPK TZ ILA SISI TUSHINDWE HAPO RUFIJI HADI ARUSHA

NA WAJINGA MNAUNGA MKONO

HII NCHI INAELEKEA SHIMONI
 
Hujui biashara wewe sasa angalia ramani ya Ethiopia kote anapakana na nani ? Kote anapakana na maadui sehemu pekee kwake kuuza umeme ni kenya kuja huku chini Tanzania

Jujui hesabu nikupe kirahisi mfano umeme anaozalisha nyanya pipa kumi anazotumia yeye pipa mbili ulitakaje sasa hizo pipa nane za nyanya zimuozee au auze hata kwa bei ya hasara kuliko kumuozea

Umeme anaozal8sha ni mwingi mno ameona heri auze kwa bei ya hasara kuliko.kutouza kabisa
Inabaki kuwa huna akili
 
Ulivyotoa mfano wa nyanya kwenye hoja ya UMEME ndo umeonyesha ujinga wako wote
 
Back
Top Bottom