Katibu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba: Umeme unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu

Katibu Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba: Umeme unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu

"Umeme utakaonunuliwa utakuwa na hasara, Lakini hiyo hasara haituhusu"🤔
😂🤣 Hapa wametengeneza excuse kabisa.

Likitokea la kutokea ambalo lazima litokee huyu Bibi akimaliza muhula wake, watasema tulisema utakuwa na hasara

Yaani Tanzania kwa Afrika ndio mambonda wa mwisho. Tunadanganywa sana na mafisadi.
 
Kulikuwa na ulazima gani wa kujenga Bwawa la Nyerere, kununua umeme wa gharama wa mitambo ya mafuta na gesi na nchi kuingia kwenye mgao mkubwa ikiwa umeme wa kutosha wa bei nafuu na uhakika ulikuwa unapatikana nchi jirani?
 
Sasa nimeamini kitendo cha kuiamini Sisiem au kujiunga nayo kwa jambo lolote,unapoteza uwezo wa kufikiri.Huyu mchaga hakupaswa kusema haya mambo ya ajabu ajabu hivi
 
Kulikuwa na ulazima gani wa kujenga Bwawa la Nyerere, kununua umeme wa gharama wa mitambo ya mafuta na gesi na nchi kuingia kwenye mgao mkubwa ikiwa umeme wa kutosha wa bei nafuu na uhakika ulikuwa unapatikana nchi jirani?
Hivi vitu vinauma sana
 
Kwa hiyo transmission costs za kuutoa Ethiopia hadi Namanga watazibeba wakenya halafu watawauzia nyie bei chee kutoka kwao.

Kwamba waethiopia wanazalisha umeme wao kwa gharama ndogo kuliko sisi huku wote vyanzo ni HEP tena sisi ujenzi ni latest!

Au teknolojia tuliyotumia akina Manyuzi wametupiga ni ya 1940s?
Walioshindwa hisabati utawajua,
 
Wakuu,

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema uamuzi wa Tanzania kuchukua umeme Ethiopia ni kitu chenye faida na si hasara kama watu wanavyodhani.

Mramba amesema ni faida kwa kuwa baadhi ya vyanzo vya umeme hapa nchini vinazalisha uniti moja kwa bei kubwa kuliko bei ambayo umeme huo utanunuliwa kutoka Ethiopia.

"Huo umeme wa Ethiopia tunanunua kwa senti za Marekani 0.077 lakini tuna vyanzo vingi ambavyo vinazalisha kwa gharama ya juu zaidi, hivyo hii ni nafuu kwetu," amesema na kuongeza umeme utaonunuliwa Ethiopia ni Megawati 100 tu.

Amesema umeme unaopelekwa mikoa ya Kaskazini unapotea kwa kiwango cha megawati 17 ambazo zinatosha kuhudumia Mkoa wa Songwe (unaotumia Mega 14) na zaidi.

"Hata huo wetu unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu, sisi tunanunulia mpakani Namanga, lakini tukipeleka sisi (umeme) tunatumia gharama kubwa," amesema Mramba.
Ameongeza kuwa "wachumi na wataalamu wote waliofanya tathmini juu ya jambo hilo waliona ni faida kubwa kuliko hasara"

Aidha, Mramba alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ununuzi wa umeme huo na kuongeza kuwa ufafanuzi uliotolewa na Msemaji wa Serikali baada kuibuka kwa mjadala huo uko sahihi.

"Maelezo ya msemaji wa Serikali yako sawa, hayana dosari," amesema Mramba na kuongeza kuwa suala la mauziano ya umeme ya nchi na nchi ni la kawaida na mpaka sasa Tanzania inauza na kununua umeme kutoka mataifa tofauti zaidi ya matatu.

Source: Mwananchi
Hivi Arusha na Mara au Mwanza kwa kusafirisha umeme wa Gridi wapi mbali au suluhisho la kununua umeme haliwexi kufanya kazi mara kupitia Sirari
Nashauri mikoa ya Mipakani tununue umeme nje.
 
Maswali ya msingi:
1. Je, wananchi wa kaskazini watauziwa umeme huo kwa bei nafuu zaidi tofauti ule wa TANESCO?
2. Kama ni "ndio", kwa nini umeme huo usisambazwe nchi nzima ili kumpa mwananchi na serikali unafuu.
3. kama ni "hapana", unafuu wa umeme wa Ethiopia uko wapi kama bei haipungui kwa mtumiaji wa mwisho, na hela itokanayo na unafuu uliotajwa inamnufaisha nani hapa nchini?
Wakati linajengwa bwawa la Nyerere hizi hadithi hazikuwepo leo ni utapeli tupu
 
Kwa Sarakasi za Tanesco kila kukicha Wananchi wamebaki na maneno ya Megawatts,Kilowatts sasa hivi wameleta kipengele kutumia umeme wa kwao ni hasara kubwa tena wa maji kuliko kununua Nje ya Nchi ambao USD ndio itatumika kwenye malipo yao wawatafute wa kuwadanganya kuhusu hizo mambo zao..
 
Attachments

  • images - 2025-02-28T165906.781.jpeg
    images - 2025-02-28T165906.781.jpeg
    12.5 KB · Views: 1
Umeme unatoka Kariba Dam Mpaka Kitwe huko kaskazini mwa Zambia hizi sanaa sijawahi kuzisikia umeme unatoka Caborabasa dam mpaka SA hakuna hii sanaa ya Tanesco na hizo Nchi umeme upo bei ya kawaida kabisa sasa ninyi wazee wa % mpaka kwenye mali yenu ni kiboko..
 
Maswali ya msingi:
1. Je, wananchi wa kaskazini watauziwa umeme huo kwa bei nafuu zaidi tofauti ule wa TANESCO?
2. Kama ni "ndio", kwa nini umeme huo usisambazwe nchi nzima ili kumpa mwananchi na serikali unafuu.
3. kama ni "hapana", unafuu wa umeme wa Ethiopia uko wapi kama bei haipungui kwa mtumiaji wa mwisho, na hela itokanayo na unafuu uliotajwa inamnufaisha nani hapa nchini?
Labda niongeze swali jingine hapo

4. Hasara walioyokuwa wanapita kuipeleka umeme kaskazini haitakuwepo tena baada ya kununua wa Ethiopia. Je nafuu hiyo itapelekea watumiaji wa umeme wa ndani watapata nafuu?

5. Vyanzo vya Bwawa la Nyumba ya Mungu 8MG, Hale 68MG vitafunwa Kwa sababu Kuna cheap umeme wa Ethiopia?

6. Kama Ethiopia wanazalidha na kusafirisha maelfu ya km na kuweza kuuza Kwa USD 0.077 kwetu sisi tumeshindwa wapi kusafirisha umeme 900km walau tuwe sawa na wao?

Kila mwaka wa uchaguzi suala la umeme linaibuka tutakuwa TU siku ikifika
 
Kwahiyo utakodi bolt pamoja na baraba au utatumia Barabara iliyopo
DIstribution line zilizopo ni za zamani haziwezi kuhimili nguvu kubwa ya umeme, natukilazimisha kutakuwa na upotevu mkubwa a umeme na kuharibu miundombinu iliyopo, ni vyema tukatumia njia mbadala wakati tukitafuta suluhisho la kudumu
 
Back
Top Bottom