Mr Spider
JF-Expert Member
- Feb 28, 2020
- 1,773
- 3,201
Umegundua nini hapo Chief, hebu tufungue macho na sisi wa Vijiji vya Lyazumbi huku!😀Mizaha hii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umegundua nini hapo Chief, hebu tufungue macho na sisi wa Vijiji vya Lyazumbi huku!😀Mizaha hii
Kuna majitu mengine bora yasiwe yanaongea kabisa. Huyu Mramba kashachafua hali ya hewa.
Sidhani kama umemuelewa.Walau huyu Katibu Mkuu Mramba namwelewa.
Nilitaka kuanzisha mada nzito hasa kuwa Raisi awavurumishe wataalamu wa Tanesco waende Ethiopia wakajifunze kuwa wao kwa nini kilomita zote hizo toka Ethiopia umeme haupotei njiani na kuwapa loss ila wetu kilomita nyingi unapotea na kuipa Tanesco mabilioni ya hasara
Argument ya katibu mkuu ina make sense naikubali Ruksa kanunueni kwa muono wangu huo umeme wa Ethiopia
Katibu mkuu Mramba nimekuelewa
Hiyo ndiyo hasara ya kuimba mama mama mama. Mnafanywa wajinga kwa kila jamboKuna majitu mengine bora yasiwe yanaongea kabisa. Huyu Mramba kashachafua hali ya hewa.
Rudia kusoma nilichoandikaSidhani kama umemuelewa.
Umeambiwa hasara ipo japo haituhusu sisi. Kwa maana hiyo suala la upotevu wa umeme njiani lipo hata kwa hao Ethiopia.
Huyo sasa ndiye MWANANCHI😁😁Alivyofukuzwa kazi akaamua kuwa mchungaji wa kanisa. Nashangaa amerudi serikalini
Kama namwelewa sana KM Mramba. Ufafanuzi usiokuwa na utata wa mhandisi🙏🙏🙏Wakuu,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Felchesmi Mramba amesema uamuzi wa Tanzania kuchukua umeme Ethiopia ni kitu chenye faida na si hasara kama watu wanavyodhani.
Mramba amesema ni faida kwa kuwa baadhi ya vyanzo vya umeme hapa nchini vinazalisha uniti moja kwa bei kubwa kuliko bei ambayo umeme huo utanunuliwa kutoka Ethiopia.
"Huo umeme wa Ethiopia tunanunua kwa senti za Marekani 0.077 lakini tuna vyanzo vingi ambavyo vinazalisha kwa gharama ya juu zaidi, hivyo hii ni nafuu kwetu," amesema na kuongeza umeme utaonunuliwa Ethiopia ni Megawati 100 tu.
Amesema umeme unaopelekwa mikoa ya Kaskazini unapotea kwa kiwango cha megawati 17 ambazo zinatosha kuhudumia Mkoa wa Songwe (unaotumia Mega 14) na zaidi.
"Hata huo wetu unaokuja kutoka Ethiopia utakuwa na hasara lakini hiyo hasara haituhusu, sisi tunanunulia mpakani Namanga, lakini tukipeleka sisi (umeme) tunatumia gharama kubwa," amesema Mramba.
Ameongeza kuwa "wachumi na wataalamu wote waliofanya tathmini juu ya jambo hilo waliona ni faida kubwa kuliko hasara"
Aidha, Mramba alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia ununuzi wa umeme huo na kuongeza kuwa ufafanuzi uliotolewa na Msemaji wa Serikali baada kuibuka kwa mjadala huo uko sahihi.
"Maelezo ya msemaji wa Serikali yako sawa, hayana dosari," amesema Mramba na kuongeza kuwa suala la mauziano ya umeme ya nchi na nchi ni la kawaida na mpaka sasa Tanzania inauza na kununua umeme kutoka mataifa tofauti zaidi ya matatu.
Source: Mwananchi
Hii kazi ya kuutetea umeme wa Ethiopia wapewe machawa. Serikali haitaweza."Umeme utakaonunuliwa utakuwa na hasara, Lakini hiyo hasara haituhusu"🤔
Kazi"Umeme utakaonunuliwa utakuwa na hasara, Lakini hiyo hasara haituhusu"🤔
Mitambo ni mipya ila nyaya za zamani, nisawa na kununua gari jipya ukalipitisha barabara mbovu, bora ukodi bolt tuKwa hiyo transmission costs za kuutoa Ethiopia hadi Namanga watazibeba wakenya halafu watawauzia nyie bei chee kutoka kwao.
Kwamba waethiopia wanazalisha umeme wao kwa gharama ndogo kuliko sisi huku wote vyanzo ni HEP tena sisi ujenzi ni latest!
Au teknolojia tuliyotumia akina Manyuzi wametupiga ni ya 1940s?