Hizi dini zinatuvuruga sana.
Tunaambiwa tuamini Biblia, tumefundishwa Amri za Mungu kabla ya Ubatizo wala kuwa Mkiristo unaambiwa uzitaje kwa Kukariri.
Tukija kwenye Maisha ya kawaida, amri moja inarukwa na haitekelezwi ambayo ni amri ya nne.
Wachungaji wanakazana na usizini, usinywe pombe nk.
Viongozi wa dini wanashadadia usizini usiibe lakini hakuna anayesema kuhusu sabato(Sabbath) ukiisema tu unaitwa Msabato sio Mkiristo tena.
Roho inaniuma sana😭
Nilimuuliza Mwalimu wangu wa KKKT kama Jumapili ni Sabato? Akanijibu Jumapili ni siku ya Ufufuo, kwahiyo wao wanasherehekea Ufufuo kama ishara ya kukombolewa.. Hivyo Ni kama kufurahia Ukombozi.. Nawaelewa. Hakina anayesema Jumapili ni Sabato, Wote tunakubaliana Sabato ni Jumamosi
Wasabato naoWananichanganya. wanasema 25 Desemba sio birthday ya Yesu, lakinihawatupi tarehe Mbadala wa kusherehekea birthday ya Yesu lakini wao wanasherehekea za kwako. Wasabato Christmas wanajifanya wapo busy lakini Pilau na Biriani wanapika. Ukiwaambia naenda kanisani Jumapili wananiambia nisiende eti tunaenda kuabudu Jua. Eti Jumapili ni sikukuu ya Jua. So hiyo sikukuu inafanyika kila wiki? 😂
Hapo ndo naiona Vita za kidini kwamba ni biashara.
Huwezi nitoa KKKT.. Mambo ya Imani ni Magumu, kila Mtu afuate thehebu atakalo, tutakutana Mbinguni.
Waislam ndo hata sijui wanayoamini chimbuko lake.. Hata Quran wanasema haijaandikwa ilishushwa toka Mbinguni. Kweli? 🤔
HAPPY SABBATH ❤️