Elections 2015 Katika Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA 2015, haya ndiyo yaliyoahidiwa

Elections 2015 Katika Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA 2015, haya ndiyo yaliyoahidiwa

..good.

..Je, wakati atcl haitengenezi faida serikali imepanga kulipa shirika RUZUKU kiasi gani?

..na baada ya hiyo miaka mitano ya kubebwa na serikali tunatarajia atcl itengeneze faida kiasi gani?

..Rwanda Airways walikuwa na mpango wa miaka 5. Baadae wakasema miaka 10. Rwanda hawajawahi kupata faida tangu waanzishe shirika lao.Majuzi wamesalimu amri kwa kuingia ubia na Qatar Airways.

..South Africa wana abiria wengi kuliko sisi. Na pia wana uchumi imara kuliko wa kwetu. Miaka miwili iliyopita walilazimika kulipatia shirika lao la ndege usd 300 million ili liweze kujiendesha.

..Bahamas wanapokea watalii wengi mara 4 ya watalii wanaokuja Tz. Shirika lao la ndege mwaka jana limepata faida ya usd 500,000.

..Kwa hiyo mimi kwa maoni yangu nadhani kumiliki shirika la ndege ni BIASHARA KICHAA / PASUA KICHWA. Ina gharama kubwa ktk uwekezaji, na faida kiduchu mno.
Ngoja tuifanye hiyo biashara uje ujibiwe badae.
 
Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyependa maendeleo ya nchi yake! Tunachokikataa na kukipinga, ni kitendo cha kuwekeza nguvu nyingi kwenye maendeleo ya vitu huku yale ya watu yakipuuzwa!

Angewekeze pande zote mbili, tusingesikia leo hii watumishi wa umma wakilalamika, biashara zikifungwa, nk. Haileti mantiki eti unaamua tu kwa makusudi kuwadhulumu wafanyakazi haki zao za msingi kwa kigezo cha kununua ndege, halafu utegemee wakushangile na kukuona wewe ni shujaa!
 
Kama mliyaona haya yote, ni kwanini mliyaweka katika ilani yenu ya 2015?
Inamaana msingetekeleza ilani hiyo au ndio kila kitu kupinga tu
Hivi kama CDM wangepata urais wa nchi hii alafu wasifanye yaliyoko kwenye ilani ya 2015 kwani tungewafanya nini? Labda wangesema hayo kwenye ilani tulikua tunatania tu.
 
Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyependa maendeleo ya nchi yake! Tunachokikataa na kukipinga, ni kitendo cha kuwekeza nguvu nyingi kwenye maendeleo ya vitu huku yale ya watu yakipuuzwa!

Angewekeze pande zote mbili, tusingesikia leo hii watumishi wa umma wakilalamika, biashara zikifungwa, nk. Haileti mantiki eti unaamua tu kwa makusudi kuwadhulumu wafanyakazi haki zao za msingi kwa kigezo cha kununua ndege, halafu utegemee wakushangile na kukuona wewe ni shujaa!
Tangu mmeleta hyo vocabulary "maendeleo ya vitu" ndio imekuwa agenda yenu. By the way hakuna maendeleo ya vitu yasiyo husisha watu. Kwenu ukijenga nyumba or ukinunua Gari faida itabaki kwako "mtu" nasio Nyumba au gari...... ndengelekiiii!!!!!!!
 
Hahahahaha kwa hyo Bahamas wanapata faida kwenye utalii na sio hyo biashara uliyosema KICHAA. nadhani ndio lengo la serikali yetu pia. Sio watalii wapande Kenya Airline watue Nairobi then waletwe na Gari zao Tz. Magu aendelee kununua mandege hata buku. Hii ni kama kuuza Duka unapata hasara ya mafuta ya kupikia faida inatoka kwenye chumvi na viberiti....

..basi muwe wakweli kwamba mmenunua ndege na mnajua kuwa zitatuingizia hasara.

..mimi napendelea utaratibu ule ambapo tulikuwa tunapata faida ktk utalii bila ya kubeba mzigo wa hasara wa kuendesha shirika la ndege.
 
Tangu mmeleta hyo vocabulary "maendeleo ya vitu" ndio imekuwa agenda yenu. By the way hakuna maendeleo ya vitu yasiyo husisha watu. Kwenu ukijenga nyumba or ukinunua Gari faida itabaki kwako "mtu" nasio Nyumba au gari...... ndengelekiiii!!!!!!!

Sasa mbona mnalazimisha kupendwa kama mnafanya maendeleo ya kununua ndege, tena kwa cash? Si mruhusu sasa demokrasia ifanye kazi! Mbona kila siku mnawazuia hao wapinzani kufanya siasa, huku mkijitahidi kuzunguka na hayo manguo yenu ya kijani? Mpaka kwenye misiba! hata aibu hamna!
 
Tumegundua hamna agenda ya tofauti maana ilani yenu ya 2015 pia tumeifanyia kaz. Kuhusu demokrasia nadhani ludi shule ukajifunze what is democracy???!!!..
 
..basi muwe wakweli kwamba mmenunua ndege na mnajua kuwa zitatuingizia hasara.

..mimi napendelea utaratibu ule ambapo tulikuwa tunapata faida ktk utalii bila ya kubeba mzigo wa hasara wa kuendesha shirika la ndege.
Ukweri ni kwamba ndege hazituingizii hasara Bali faida...sio lazima faida upate ndani ya ndege hzo
 
Ahadi zilizopo ndani ya ilani ya CDM zingetekelezeka endapo tu wangalipata ridhaa ya kushika dola. Uwepo wa mfanano wa yaliyotajwa ndani yake na yale yaliyopo ndani ya ilani ya CCM, haina maana yaungwe mkono hata kama yana kasoro luluki na "wrong approach" ktk utekelezaji wake.

Ilani ni sera ambayo ndani kuna mtazamo mpana, shauku na kiu ya kutaka kufanikisha jambi fulani. Hata nabii Musa alikuwa na "vision" kama hiyo. Na aliwaahidi wana wa Israeli kuwa "wanakwenda ktk nchi iliyojaa maziwa na asali". Lakini kilichotokea ktt uhalisia wake, ilikuwa mapambano ya miaka mingi ya kivita na kufanya mateka, na hata Musa mwenyewe hakuweza kufika ktk nchi ya ahadi.
 
Uende mbali think wide! huwezi kufanya hayo yote wakati wananchi hawana maji, you have to srike the balance. There is no striking balance with Jiwe!

Kwani kuna miradi ya maji iliyokwama? If you are not informed doesn't mean there is nothing going on.

miradi_ya_maji.jpg
 
Ukweri ni kwamba ndege hazituingizii hasara Bali faida...sio lazima faida upate ndani ya ndege hzo

..mbona unaikana kauli uliyotoa ktk post # 18?

..uwezo wa kuongeza idadi ya watalii bila kujitwisha mzigo wa hasara wa kumiliki shirika la ndege tunao.

..Tz imekuwa ikipata mapato makubwa ktk sekta ya utalii kuzidi Kenya na Rwanda bila kujali kwamba majirani zetu wana mashirika ya ndege.
 
Khaaa nimegundua najibishana na mwanafunzi wa darasa la saba. Et nimeikana kauli yangu katika post #18 hahahaha, Kenya imezidiwa mapato na Tz labda Tangu tumeanza kuleta ndege mpya...DOGO UNANIVUNJIA HESHIMA UJUE, HEBU NENDA JUKWAA LA WATOTO KULE UKACHEZE NAWENZIO HAHAHAAA
 
Sina hakika kama umewahi kufanya biashara yoyote japo ya genge vinginevyo usingeongea huu ujinga
Katika hali ya kawaida, huwezi kuanza kupata faida kwa muda mfupi kiasi hiki katika investment kubwa kama iliyofanywa kwa ATCL. Mpango mkakati wa miaka mitano kwa ATCL ilikuwa ni kuwekeza katika ununuzi wa ndege. Bila shaka mpango mkakati unaofuata hautakuwa ununuzi tena, bali namna gani ya kuzitumia hizi ndege kutengeneza biashara yenye faida kubwa na kuweza kurudisha pesa yote iliyotumika kufanya investment.
 
CHADEMA itafanya nini:
  • Kujenga reli mpya na kukarabati zilizopo kwa viwango vya kisasa kwa kuzingatia maslahi ya nchi. Hii ni pamoja na kujenga uwezo wa kuzalisha mataluma ya reli nchini.
  • Kuboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
  • Kujenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
  • Kujenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
  • Kujenga miundombinu ya kisasa ili kuondoa misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Kuimarisha usafiri wa majini kwa kuboresha na kuweka miundo mbinu mipya.
Matokeo tarajiwa:
  • Bandari kuwa njia kuu ya uchumi kwa kuhudumia kilimo na viwanda. Na pia, kuchangia zaidi ya theluthi moja ya pato la Taifa.
  • Shirika la ndege la Taifa (Air Tanzania) kuimarishwa ili kutoa huduma nchini na nje ya nchi huku likijiendesha kibiashara zaidi na kwa fiada.
  • Wananchi hasa wa visiwani kupata huduma muhimu za kiuchumi na kijamii.
  • Mizigo yote mizito kusafirishwa kwa njia ya reli na meli ili kupunguza gharama na kuongeza tija katika uzalishaji. Kupunguza ajali na kulinda miundo mbinu.
  • Barabara zinazodumu na zilizo salama zaidi kwa watumiaji.
Sasa msikilize Lema

Na hii ndio Ilani ya uchaguzi ya Chadema 2015. Pitia ukurasa wa 40 na 41

WALIBADIRISHIA GIA ANGANI WALIPOTUA HAWAKUWA NA ILANI YOYOTE
Fursa
Uwepo wa kiasi kikubwa cha madini na vyanzo vya nishati hapa nchini. CHADEMA itafanya nini • Tutalenga kuongeza 3,000 MW katika gridi ya taifa katika miaka yetu mitano ya kwanza kwa kutumia umeme wa maji na gesi ambazo vyote vitakuwa na gharama nafuu kwa maendeleo ya viwanda na matumizi ya nyumbani ukiweka maanani kwamba wakati nchi kama Misri inalipiza gharama ya centi 2 za dola za kimarekani kwa KWH Tanzania ni centi 16 za dola za kimarekani kwa KWH na wakati huo huo hatuna budi kushindana nan chi kama soko la pamoja. •
Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme ili kufikia zaidi ya asili mia (75%) ya Watanzania wote mijini na vijijini. •
Tutalenga kupunguza matumizi ya nishati ya misitu kama kuni na mkaa kwa asilimia themanini kwa kuongeza matumizi ya nishati mbadala kama gesi asilia, mkaa wa mawe na nishati jadidifu. •
Uzalishaji wa nishati ya kutosha na bei nafuu; na matumizi yenye tija ya madini na nishati • Kupunguza bei ya mafuta, gesi na umeme kwa matumizi ya kawaida na uzalishaji kwa kupunguza mrundikano wa kodi na urasimu wa upatikanaji wake ili kupunguza gharama za maisha kwa Watanzania.
 
Kwahiyo ccm wanatekeleza ilani ya CHADEMA ?
CHADEMA itafanya nini:
  • Kujenga reli mpya na kukarabati zilizopo kwa viwango vya kisasa kwa kuzingatia maslahi ya nchi. Hii ni pamoja na kujenga uwezo wa kuzalisha mataluma ya reli nchini.
  • Kuboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
  • Kujenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
  • Kujenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
  • Kujenga miundombinu ya kisasa ili kuondoa misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Kuimarisha usafiri wa majini kwa kuboresha na kuweka miundo mbinu mipya.
Matokeo tarajiwa:
  • Bandari kuwa njia kuu ya uchumi kwa kuhudumia kilimo na viwanda. Na pia, kuchangia zaidi ya theluthi moja ya pato la Taifa.
  • Shirika la ndege la Taifa (Air Tanzania) kuimarishwa ili kutoa huduma nchini na nje ya nchi huku likijiendesha kibiashara zaidi na kwa fiada.
  • Wananchi hasa wa visiwani kupata huduma muhimu za kiuchumi na kijamii.
  • Mizigo yote mizito kusafirishwa kwa njia ya reli na meli ili kupunguza gharama na kuongeza tija katika uzalishaji. Kupunguza ajali na kulinda miundo mbinu.
  • Barabara zinazodumu na zilizo salama zaidi kwa watumiaji.
Sasa msikilize Lema

Na hii ndio Ilani ya uchaguzi ya Chadema 2015. Pitia ukurasa wa 40 na 41
 
Khaaa nimegundua najibishana na mwanafunzi wa darasa la saba. Et nimeikana kauli yangu katika post #18 hahahaha, Kenya imezidiwa mapato na Tz labda Tangu tumeanza kuleta ndege mpya...DOGO UNANIVUNJIA HESHIMA UJUE, HEBU NENDA JUKWAA LA WATOTO KULE UKACHEZE NAWENZIO HAHAHAAA

..tangu awamu ya 4 Tz imekuwa kinara na inaongoza kwa mapato ktk sekta ya utalii afrika mashariki.
 
Back
Top Bottom