CHADEMA itafanya nini:
- Kujenga reli mpya na kukarabati zilizopo kwa viwango vya kisasa kwa kuzingatia maslahi ya nchi. Hii ni pamoja na kujenga uwezo wa kuzalisha mataluma ya reli nchini.
- Kuboresha bandari zilizopo na kujenga mpya kama vitega uchumi vya Taifa ili kurejesha biashara tulizopoteza kwa bandari za nchi jirani.
- Kujenga barabara nchini kwa kuzingatia ubora hasa zile za vijijini.
- Kujenga shirika la Ndege la Taifa linalojiendesha kwa misingi ya faida.
- Kujenga miundombinu ya kisasa ili kuondoa misongamano ya magari hasa katika majiji ya Dar es salaam, Mwanza, Kuimarisha usafiri wa majini kwa kuboresha na kuweka miundo mbinu mipya.
Matokeo tarajiwa:
- Bandari kuwa njia kuu ya uchumi kwa kuhudumia kilimo na viwanda. Na pia, kuchangia zaidi ya theluthi moja ya pato la Taifa.
- Shirika la ndege la Taifa (Air Tanzania) kuimarishwa ili kutoa huduma nchini na nje ya nchi huku likijiendesha kibiashara zaidi na kwa fiada.
- Wananchi hasa wa visiwani kupata huduma muhimu za kiuchumi na kijamii.
- Mizigo yote mizito kusafirishwa kwa njia ya reli na meli ili kupunguza gharama na kuongeza tija katika uzalishaji. Kupunguza ajali na kulinda miundo mbinu.
- Barabara zinazodumu na zilizo salama zaidi kwa watumiaji.
Sasa msikilize Lema
Na hii ndio Ilani ya uchaguzi ya Chadema 2015. Pitia ukurasa wa 40 na 41
"
Sio tuu ilibadilishwa gia angani bali pia na uelekeo ulibadilishwa"......maneno haya yameandikwa katika kitabu kiitwacho "NYUMA YA PAZIA"mbacho muandishi wake ni aliyekuwa katibu mkuu wa chadema Ndg. Dr. Wilbroad Peter Slaa.
Ki msingi, ilani ya chadema iliandaliwa ki ustadi kwa utafiti wa kina kuanzia 2011 chini ya usimamizi wa Katibu mkuu ambaye pia alikuwa akiandaliwa kuwa mgombea urais 2015 akisaidiwa na msaidizi mkuu wa mgombea urais aliyeteuliwa na chama ndg. John Mrema. Wawili hawa walizunguka maeneo mengi ya nchi na nje ya nchi wakifanya maandalizi na zao lake ni hiyo ilani bora kabisa.
Nini kilitokea? Baada ya kubadili gia angani, na uelekeo ulibadilika; ilani ilibaki tuu kwenye makaratasi, wakapachika mapichapicha ya wagombea wa angani waliokuwa sio tuu hawaifahamu vyema ilani ile bali hata yale waliyokuwa wamebahatika kuyaelewa hawakuyaunga mkono. Ndiyo maana ilani hiyo haikunadiwa bali tuliambiwa tusome mitandaoni. Na nidhahili, kuna baadhi ya mambo mazuri zaidi yalifutwa kabisa; CHADEMA ikakosa hoja ya msingi kwa wananchi na kutumia Njia ya hadaa na hamasa kurubuni watu waweze kuwachagua bila kufuata misingi halisi ya chama na hoja zenye mashiko kwa mstakabali wa taifa.
Njia zilizotumika ni kama kuzungusha miko, kuwapakia vijana viroba, kupanda daladala, kula kwa mama ntilie, kudeki rami na kadhalika. Hoja kama kupambana na mafisadi, ubadhirifu, ulinzi wa mali za umma, usimamizi wa rasilimali za taifa, Kudhibiti uzembe katika ofisi za umma ni hoja ambazo sio tuu zilidhibitiwa, ilikuwa ni marufuka kutamkwa. Hata zile nyimbo za hamasa zikikipambanua CHADEMA kupambana na mafisadi zilipigwa marufuku.
Ni dhahiri kuwa walioifahamu vyema ilani hii hawakuwa na nafasi ya kuinadi baada ya gia na uelekeo kubadilikia angani.
Hivyo wana chadema wa kawaida kuwahoji juu ya ilani yao ya 2015 ni kuwaonea, hawaijui. Ili kuwatendea haki, waulize habari ya viroba, kuzungusha mikono na kudeki lami, mambo ya ndembendembe chaliiiiiiiiii, ndivyo vitu walivyo shughulika navyo kipindi chote cha uchaguzi ilani ikiwa kando.
Tujifunze kulinda itikadi, falisafa, imani na misingi ya vyama vyetu tunapokuwa tunataka kuchagua viongozi, lakini pia kuupima uadilifu na uhalali wa wagombea wetu. Tutafanikiwa.
Dunstan Buberwa Ntamilyango.
0759829015.