Elections 2015 Katika Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA 2015, haya ndiyo yaliyoahidiwa

Ngoja tuifanye hiyo biashara uje ujibiwe badae.
 
Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu asiyependa maendeleo ya nchi yake! Tunachokikataa na kukipinga, ni kitendo cha kuwekeza nguvu nyingi kwenye maendeleo ya vitu huku yale ya watu yakipuuzwa!

Angewekeze pande zote mbili, tusingesikia leo hii watumishi wa umma wakilalamika, biashara zikifungwa, nk. Haileti mantiki eti unaamua tu kwa makusudi kuwadhulumu wafanyakazi haki zao za msingi kwa kigezo cha kununua ndege, halafu utegemee wakushangile na kukuona wewe ni shujaa!
 
Kama mliyaona haya yote, ni kwanini mliyaweka katika ilani yenu ya 2015?
Inamaana msingetekeleza ilani hiyo au ndio kila kitu kupinga tu
Hivi kama CDM wangepata urais wa nchi hii alafu wasifanye yaliyoko kwenye ilani ya 2015 kwani tungewafanya nini? Labda wangesema hayo kwenye ilani tulikua tunatania tu.
 
Tangu mmeleta hyo vocabulary "maendeleo ya vitu" ndio imekuwa agenda yenu. By the way hakuna maendeleo ya vitu yasiyo husisha watu. Kwenu ukijenga nyumba or ukinunua Gari faida itabaki kwako "mtu" nasio Nyumba au gari...... ndengelekiiii!!!!!!!
 

..basi muwe wakweli kwamba mmenunua ndege na mnajua kuwa zitatuingizia hasara.

..mimi napendelea utaratibu ule ambapo tulikuwa tunapata faida ktk utalii bila ya kubeba mzigo wa hasara wa kuendesha shirika la ndege.
 
Tangu mmeleta hyo vocabulary "maendeleo ya vitu" ndio imekuwa agenda yenu. By the way hakuna maendeleo ya vitu yasiyo husisha watu. Kwenu ukijenga nyumba or ukinunua Gari faida itabaki kwako "mtu" nasio Nyumba au gari...... ndengelekiiii!!!!!!!

Sasa mbona mnalazimisha kupendwa kama mnafanya maendeleo ya kununua ndege, tena kwa cash? Si mruhusu sasa demokrasia ifanye kazi! Mbona kila siku mnawazuia hao wapinzani kufanya siasa, huku mkijitahidi kuzunguka na hayo manguo yenu ya kijani? Mpaka kwenye misiba! hata aibu hamna!
 
Tumegundua hamna agenda ya tofauti maana ilani yenu ya 2015 pia tumeifanyia kaz. Kuhusu demokrasia nadhani ludi shule ukajifunze what is democracy???!!!..
 
..basi muwe wakweli kwamba mmenunua ndege na mnajua kuwa zitatuingizia hasara.

..mimi napendelea utaratibu ule ambapo tulikuwa tunapata faida ktk utalii bila ya kubeba mzigo wa hasara wa kuendesha shirika la ndege.
Ukweri ni kwamba ndege hazituingizii hasara Bali faida...sio lazima faida upate ndani ya ndege hzo
 
Ahadi zilizopo ndani ya ilani ya CDM zingetekelezeka endapo tu wangalipata ridhaa ya kushika dola. Uwepo wa mfanano wa yaliyotajwa ndani yake na yale yaliyopo ndani ya ilani ya CCM, haina maana yaungwe mkono hata kama yana kasoro luluki na "wrong approach" ktk utekelezaji wake.

Ilani ni sera ambayo ndani kuna mtazamo mpana, shauku na kiu ya kutaka kufanikisha jambi fulani. Hata nabii Musa alikuwa na "vision" kama hiyo. Na aliwaahidi wana wa Israeli kuwa "wanakwenda ktk nchi iliyojaa maziwa na asali". Lakini kilichotokea ktt uhalisia wake, ilikuwa mapambano ya miaka mingi ya kivita na kufanya mateka, na hata Musa mwenyewe hakuweza kufika ktk nchi ya ahadi.
 
Ukweri ni kwamba ndege hazituingizii hasara Bali faida...sio lazima faida upate ndani ya ndege hzo

..mbona unaikana kauli uliyotoa ktk post # 18?

..uwezo wa kuongeza idadi ya watalii bila kujitwisha mzigo wa hasara wa kumiliki shirika la ndege tunao.

..Tz imekuwa ikipata mapato makubwa ktk sekta ya utalii kuzidi Kenya na Rwanda bila kujali kwamba majirani zetu wana mashirika ya ndege.
 
Khaaa nimegundua najibishana na mwanafunzi wa darasa la saba. Et nimeikana kauli yangu katika post #18 hahahaha, Kenya imezidiwa mapato na Tz labda Tangu tumeanza kuleta ndege mpya...DOGO UNANIVUNJIA HESHIMA UJUE, HEBU NENDA JUKWAA LA WATOTO KULE UKACHEZE NAWENZIO HAHAHAAA
 
Sina hakika kama umewahi kufanya biashara yoyote japo ya genge vinginevyo usingeongea huu ujinga
 
WALIBADIRISHIA GIA ANGANI WALIPOTUA HAWAKUWA NA ILANI YOYOTE
Fursa
Uwepo wa kiasi kikubwa cha madini na vyanzo vya nishati hapa nchini. CHADEMA itafanya nini • Tutalenga kuongeza 3,000 MW katika gridi ya taifa katika miaka yetu mitano ya kwanza kwa kutumia umeme wa maji na gesi ambazo vyote vitakuwa na gharama nafuu kwa maendeleo ya viwanda na matumizi ya nyumbani ukiweka maanani kwamba wakati nchi kama Misri inalipiza gharama ya centi 2 za dola za kimarekani kwa KWH Tanzania ni centi 16 za dola za kimarekani kwa KWH na wakati huo huo hatuna budi kushindana nan chi kama soko la pamoja. •
Tutaimarisha uzalishaji na usambazaji wa umeme ili kufikia zaidi ya asili mia (75%) ya Watanzania wote mijini na vijijini. •
Tutalenga kupunguza matumizi ya nishati ya misitu kama kuni na mkaa kwa asilimia themanini kwa kuongeza matumizi ya nishati mbadala kama gesi asilia, mkaa wa mawe na nishati jadidifu. •
Uzalishaji wa nishati ya kutosha na bei nafuu; na matumizi yenye tija ya madini na nishati • Kupunguza bei ya mafuta, gesi na umeme kwa matumizi ya kawaida na uzalishaji kwa kupunguza mrundikano wa kodi na urasimu wa upatikanaji wake ili kupunguza gharama za maisha kwa Watanzania.
 
Kwahiyo ccm wanatekeleza ilani ya CHADEMA ?
 

..tangu awamu ya 4 Tz imekuwa kinara na inaongoza kwa mapato ktk sekta ya utalii afrika mashariki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…