Elections 2015 Katika Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA 2015, haya ndiyo yaliyoahidiwa

i dont support kusomesha wajawazito.
Mm nilimchagua Magufuli Kwa kuwa ilani ya CCM kimoja Wapo ilikuwa Ni kumpa elimu mtoto wa kike hata baada ya kuujifungua...lakini ilikuwa Ni utapeli mkubwa Na mijitu haina hata aibu imetulia....Rasmi siyapendi majitu ya hivi
 
Kama mliyaona haya yote, ni kwanini mliyaweka katika ilani yenu ya 2015?
Inamaana msingetekeleza ilani hiyo au ndio kila kitu kupinga tu
....kwamba kila mwenye mtazamo tofauti na serekali lazima awe Chadema!!!?????.......
 
..Jpm alisema alishauriwa na Kagame kununua ndege. Sasa Kagame kaingia hasara mpaka imebidi ajisalimishe kwa Qatar kwa kuingia nao ubia.
Kwa hiyo kwa akili zako za nyumbu, unahisi serikali haikuwa na haja wala plan ya kuwa na national carrier yake hadi kagame alivyoshauri na serikali ndio ikaamua.
You guys sound so ignorant i feel ashamed.
 
maendeleo ya watu... elimu bure.. watu mikopo vyuo vikuu.... vituo vya Afya na Hospitali.. watu Barabara kuuza mazao na kuwahi hospitali za rufaa

wachu tokin about?[emoji12]

🔈🔉🔊🔊🔊🎼🎵🎶🎤🎷🎺 Praise team at work.
 
Walitoa Ilani yao ya uchaguzi,lakini naamini walificha MBINU watakayotumia kutekeleza Ilani hiyo.Kwa hiyo mnapotekeleza Ilani za wenzenu ombeni pia na mbinu(ushauri) walizotaka kutumia.Msiwafanye maadui zenu.Tunajenga nyumba moja,hakuna haja ya kugombea fito.
 
" Sio tuu ilibadilishwa gia angani bali pia na uelekeo ulibadilishwa"......maneno haya yameandikwa katika kitabu kiitwacho "NYUMA YA PAZIA"mbacho muandishi wake ni aliyekuwa katibu mkuu wa chadema Ndg. Dr. Wilbroad Peter Slaa.

Ki msingi, ilani ya chadema iliandaliwa ki ustadi kwa utafiti wa kina kuanzia 2011 chini ya usimamizi wa Katibu mkuu ambaye pia alikuwa akiandaliwa kuwa mgombea urais 2015 akisaidiwa na msaidizi mkuu wa mgombea urais aliyeteuliwa na chama ndg. John Mrema. Wawili hawa walizunguka maeneo mengi ya nchi na nje ya nchi wakifanya maandalizi na zao lake ni hiyo ilani bora kabisa.

Nini kilitokea? Baada ya kubadili gia angani, na uelekeo ulibadilika; ilani ilibaki tuu kwenye makaratasi, wakapachika mapichapicha ya wagombea wa angani waliokuwa sio tuu hawaifahamu vyema ilani ile bali hata yale waliyokuwa wamebahatika kuyaelewa hawakuyaunga mkono. Ndiyo maana ilani hiyo haikunadiwa bali tuliambiwa tusome mitandaoni. Na nidhahili, kuna baadhi ya mambo mazuri zaidi yalifutwa kabisa; CHADEMA ikakosa hoja ya msingi kwa wananchi na kutumia Njia ya hadaa na hamasa kurubuni watu waweze kuwachagua bila kufuata misingi halisi ya chama na hoja zenye mashiko kwa mstakabali wa taifa.

Njia zilizotumika ni kama kuzungusha miko, kuwapakia vijana viroba, kupanda daladala, kula kwa mama ntilie, kudeki rami na kadhalika. Hoja kama kupambana na mafisadi, ubadhirifu, ulinzi wa mali za umma, usimamizi wa rasilimali za taifa, Kudhibiti uzembe katika ofisi za umma ni hoja ambazo sio tuu zilidhibitiwa, ilikuwa ni marufuka kutamkwa. Hata zile nyimbo za hamasa zikikipambanua CHADEMA kupambana na mafisadi zilipigwa marufuku.

Ni dhahiri kuwa walioifahamu vyema ilani hii hawakuwa na nafasi ya kuinadi baada ya gia na uelekeo kubadilikia angani.

Hivyo wana chadema wa kawaida kuwahoji juu ya ilani yao ya 2015 ni kuwaonea, hawaijui. Ili kuwatendea haki, waulize habari ya viroba, kuzungusha mikono na kudeki lami, mambo ya ndembendembe chaliiiiiiiiii, ndivyo vitu walivyo shughulika navyo kipindi chote cha uchaguzi ilani ikiwa kando.

Tujifunze kulinda itikadi, falisafa, imani na misingi ya vyama vyetu tunapokuwa tunataka kuchagua viongozi, lakini pia kuupima uadilifu na uhalali wa wagombea wetu. Tutafanikiwa.

Dunstan Buberwa Ntamilyango.
0759829015.
 
Sasa Mbona kuna wabwekaji humu wanapinga maendeleo? Tena walioahidi!

Nadhani hujaelewa Hoja ya Wakosoaji/Wapinzani wanapinga Mchakato Mchafu unaotumika kufufua Shirika letu la ATCL . Tunahitaji Bunge lipitishe Pesa za Manunuzi, Zinunuliwe na Wakala wa Manunuzi Serikalini( GPSA) zikiisha nunuliwa zikaguliwe na CAG sio Rais ajitwike Majukumu hayo Muhimu ya Bunge, GPSA na CAG.
 
ahaa kwa hiyo think-tank yenu ni CHADEMA, shajua.....shajua.....
 
Ndivyo Lema alivyosema kwenye hiyo clip niliyoambatanisha? Kumbuka post yangu imekuja baada ya kumsikiliza Lema. Kama hujamsikiliza tafadhali msikilize halafu uone kama anachokisema ndicho hiki ulichokiandika hapa.
 
ATCL ilianzishwa au ilifufuliwa bila kua na business plan yoyote ile..point ya msingi ilikua ni kua na shirika ila hakukua na business plan yoyote ile
 
ATCL ilianzishwa au ilifufuliwa bila kua na business plan yoyote ile..point ya msingi ilikua ni kua na shirika ila hakukua na business plan yoyote ile
How sure you are? Can you prove?
 
Hypocrites
 
Mwenyekiti alipoleta neno kubadilisha gia angani alikuwa na maana pana sana!

Wamebadilisha gia angani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…