Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

Katika jambo kubwa ninalojivunia, ni kutambua kuwa hakunaga UCHAWI

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Nawasikitia sana watu ambao wamebaki kuamini kwamba hapa duniani kuna kitu kinachoitwa uchawi na kinafanya kazi. aisee hakuna kitu kama hicho binadamu ni mnyama tu ana limit zake yako miujiza hawezi tu kufanya mfano kupotea na kwenda kutokea sehemu nyingine au eti kujibadilisha umbo..

kuamini uchawi ni ujinga naini uoga uliopitiliza mimi nimeshapita mazingira mengi sana tu kuanzia makaburini, mabaharini, misituni usiku Kwa usiku na sijawahi kuona badiliko lolote nikalihusisha na eti ni mbinu za kishetani. Maisha yapo tu the way yapo magonjwa yapo ya Kuua so hata Ukifa ghafla hujalogwa tunakupima tunajua ulikuwa na ugonjwa gani..

Zamani kweli mambo mengi yalikuwa hayajagunduliwa maswali yasiyo na majibu yalikuwa mengi.. Pressure, kisukari, kifafa na magonjwa ya akili haya kujulikana hivyo watu akili zao ilibidi ziishie kwenye kuamini uchawi kwamba Ukifa na ugonjwa wasioujua basi umelogwa..

Uchawi upo Kwa dhana kwamba una fanywa (Wana upractice Kwa mazoea yao ila hautendi lolote yaani huwezi ukawa tabora eti umuue mtu yupo dar (hakuna outcome yoyote).

Ndo maana mimi daima napenda mtu ninayefanya naye mijadala awe haamini hakuna uchawi nitamkubali sana nitaona kichwa chake kinaweza ku solve mysterious mbalimbali.. mbona simple tu MUNGU YUPO, UKICHAA UPO, MAARIFA YAPO, NGUVU ZIPO ILA UCHAWI HAUPO LABDA UCHAWA.mwingine unakuta eti kisa tu ana kidonda kilichokataa kupona basi wanaelekeza fikra kwamba ni cha kulogwa cha kichawi mbona ishu kama hiyo ni nyepesi kwamba akili yako haitaki kuamini kama kidonda hakiwezi tu kupona Kwa sababu nyingine za afya au mazingira Mpaka utuhumu uchawi.

Ukiita wa kumi uwaulize wakutajie shida zao kubwa mbili wote watataja hela na afya njema.. Yaani means shida kubwa ya binadamu ni umaskini na maradhi hakuna hata mmoja ambaye atakwambia anasumbuliwa na wachawi kwamba hataki hela ye anataka umuondelee wachawi kwenye maisha yake. ... Kuhusu maradhi karibia yote yanatambuliwa visababishi vyake, dalili na tiba..
 
Nawasikitia sana watu ambao wamebaki kuamini kwamba hapa duniani kuna kitu kinachoitwa uchawi aisee hakuna kitu kama hicho binadamu mnyama tu ana limit zake kuamini uchawi ni ujinga ni uoga mimi nimeshapita mazingira mengi sana sijawahi kuona badiliko lolote nikalihusisha na eti mbinu za kishetani huo ni uongo. Maisha yapo tu the waya yapo magonjwa yapo ya Kuua so hata Ukifa ghafla hujalogwa tu nakupima tunajua ulikuwa na ugonjwa gani. Uchawi upo Kwa dhana kwamba una fanywa (Wana upractice ila hautendi(hakuna outcome yoyote). Yaani mimi daima napenda mtu ninayefanya naye mijadala awe haamini kama hakuna uchawi mbona simple tu MUNGU YUPO, UKICHAA UPO, MAARIFA YAPO, NGUVU ZIPO ILA UCHAWI HAUPO LABDA UCHAWA.
“For every action there is equal and opposite reaction”
 
KWA MFANO MTU KACHANGANYIKIWA FAMILIA ZINAOAMINI UCHAWI UTASIKIA MPELEKENI KWA FUNDI YULE AU FUNDI YULE KUMBE WAKATI HUO HUO UKIWA NA FAMILIA AMBAYO HAIMINI IVYO VITU WATAKUPELEKA KWA PSYCHO PATH DR AKACHUUA HISTORY YAKO UKAPONA # USHAURI WA BURE KUAMINI UCHAWI NI DALILI ZA UMASKINI THE SAME KUAMINI FREEMASON ZINGATIA IMANI YAKO TU ISLAM ,CHRISTIAN ,PAGAN (WATOLO WA IBADA) UTAKUWA CURE NA SAFE
 
Biblia na Quran zenyewe zinasema upo, na hata concept ya shetani, sub component ni uchawi na wachawi. Bahati mbaya wachawi wanalindwa na serikali wasiumbuliwe tangu enzi za witchcraft ordinace ya mkoloni
 
Uchawi haupo ndugu: ni vile waliotangulia kuishi hapa duniani walikuwa nyuma sana kiteknolojia na ndio wakatuletea huu UTOPOLO na UKOLO wao kwa mbeleko ya dini na tamaduni! So kutouamini inahitajika nguvu kubwa sana ya akili kuliko kawaida; Cha kufanya wewe anza na familia yako kuyaendea mambo kisayansi utakuja kunishukuru!


SAYANSI kutokuwa na majibu ya baadhi ya mambo leo haifanyi kukosa hayo majibu kesho: kumbuka tafiti bado zingali zinafanyika kila leo, hivyo ni Jambo la muda tu kabla ya kila swali kujibiwa kisayansi: Halafu huo ushahidi wa MATATIZO yanayotukuta na kudhani ni matunda ya uchawi kila mtu mzima anao huo ushahidi: Njoo inbox tubadilishane uzoefu wa matatizo na tuone vile tuliyatatua ndipo ujue kuwa huwa tunapigwa sana na WAPIGA RAMLI na MANABII kwa mgongo wa UCHAWI.


Hii 1.(iii) la kuumwa hoi na ugonjwa kutoonekana, tushalileza humu, ngoja turudie kwa msisitizo: Baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha ugonjwa kutoonekana kwa mgonjwa pindi afanyiwapo vipimo ni pamoja na:-
1.Mgonjwa/Muuguzi(ndugu)amekosea kueleza ugonjwa kwa daktari.Hivyo daktari akaelekeza kufanyika vipimo tofauti na vile vya ugonjwa halisi, hapa ugonjwa hautaonekana.
2.Kukosekana kwa wataalamu waliobobea kwenye maabara, kunaweza kusababisa kushindwa kuuona ugonjwa.
3.Uduni wa vipimo vilivyotumika na ujuzi mdogo wa madaktari waliopo katika hospitali husika: Level ya hospitali pia huambatana na ubora wa vifaa-tiba na ubingwa wa madaktari wake;...hivyo ukifanya vipimo kwenye hospitali isiyo na vifaa bora na madaktari bigwa kuna uwezekano mkubwa usiuone ugonjwa unaokusumbua.
4.Mwisho ila sio kwa umuhimu, kuna haya matatizo ya KISAIKOLOJIA mara nyingi yanachanganya sana wagonjwa! Hata kupelekea madaktari washindwe kujua mgonjwa anaumwa nini hata baada ya kumfanyia vipimo.
Iko hivi; Ukiumwa magonjwa yanayoathiri mfumo wa ufahamu(mental-disorder) unaweza kuhisi TUMBO LINAWASHA KWA NDANI na ukaenda hospitali ukaeleza hivyo, na ukakutana na daktari hana ujuzi wa kutosha kumsoma mtu mwenye matatizo ya kisaikolojia hapa lazma ataagiza kufanyika 'ultrasound' na Kama hatoona kitu, ataawambia na mgonjwa akiendelea kulalama atafanyiwa upasuaji, na kisipoonekana kitu, utarudi hapa na kusema UMEROGWA. Ila ukiwa muelewa wa haya magonjwa ya kisaikolojia huwezi kufika kwa wapiga ramli zaidi utaenda hospitali za ngazi za juu zaidi, watakaoweza kugundua tatizo na kulitibu KISAYANSI kabisa!
NB: 1.Ikiwa imetokea umekosa PESA za kwenda Muhimbili/Milembe na akatokea mtu akashauri MGONJWA WA AKILI(mental disorder patient) akatibiwe kwa MAOMBI YA MANABII ama kwa MGANGA wa miti-shamba nenda maana tiba za miti-shamba sio uchawi, ILA KUWA MAKINI SANA na haya:-
(i)Ukiambiwa amerogwa usiamini kabisa(piga kimya, ili huduma iendelee..)
(ii) Fuatilia kwa umakini hatua zote za kumfariji anazofanyiwa mgonjwa wako, maana zingine ni za kidhalilidhaji, hakikisha unamuepusha nazo.
(iii)Wakitoa dawa(mizizi/maji ya baraka) ya kutumia nyumbani,hakikisha wanaoanza kutumia hayo maji ni mifugo na sio mgonjwa, maana baadhi ya mizizi ni sumu na vilivyochanganywa kwenye maji ya upako wewe huvijui.
 
Uchawi haupo na haujawai kuwepo.

Uchawi hakuna. Waliomtengeneza yesu Ndio walioleta neno uchawi. Ni kama movie. Kunakua na steringi na kubwa la maadui. Hapa kwenye movie hii yesu ndo stering na uchawi kubwa la maadui
 
Uchawi ni imani zilizotokana na ujinga. Mjinga asipoelewa kitu anasingizia uchawi. Zamani magonjwa yote yalihusishwa na uchawi. Hata wazungu walikuwa hivyo hivyo wanaamini sana uchawi kwenye karne zilizopita hasa hasa middle age.

Imani za kishirikina zinarudisha sana watu nyuma
 
Sijawahi amini kabisa huo upumbavu, kijijini niliwaambia waniroge nikaishia kuitwa mimi ndo mchawi mwenyewe!
Imani za uchawi zipo direct proportional na ujinga!haki
Hakuna uchawi ila Kuna ujanjaujanja au mazingaumbwe yanayofanywa na watu wenye uwezo wa kufanya au kuonesha mimi au wewe tutakachoshindwa kutambua katika Hali ya kawaida.

Uchawi ni jina tu ila haupo Dunia hii. au upo Kwa wajinga na wapumbavu tu kama waafrika
 
Back
Top Bottom