Kuna watu hawatoi Siri
Wana viapo vya hatari
Kuna watu wanateswa miaka huko Guantanamo prison ila Siri hawaitoi
🤓🤓😂
Ukiona hvyo hawana siri zile konk.
Kuna siri ambazo Adui anazitegemea kufanikisha Jambo hivyo atakuwa anakutesa kwa kipimo cha kukuhofia usije ukafa.
Hapo uta survive tuu.
Wengi hubaki kusema mimi ni mtu wa kawaida, sijui chochote.
Mbaya zaidi watataja wale mnaowafahamu na kuwatafuta.
Mfano, anatafutwa Chid, Suma, na Peter.
Peter akakamatwa.
Peter atasema Suma ndiye alikuwa anakutana naye sehemu Fulani hata kama alikuwa hakutani naye. Anatoa maelezo ambayo yanaendana na kile ambacho tayari mnakijua. Anachoongeza nu kidogo ili mumuamini kwa kiasi.
Ukimuuliza boss wenu ni Nani,
Atasema hajaeahi kukutana naye zaidi ya Suma ndiye aliyekuwa anampa Maelekezo.
Kisha ataacha stori hapo
Mtampiga weewee kisha mtamuacha.
Kesho mtakuja tens, mtampiga weweee atakausha.
Siku inayofuata atajifanya anataka kusema Jambo, atamuongeza Chid.
Atasema Kuna Siku alimsikia Suma akimtaja MTU anayeitwa chid.
Ataulizwa Chid ni Nani, na alizungumziwa vipi na Suma.
Atasema Binafsi hajawahi kumwina Chid, ila alikuwa anasikia akiongea na simu na Suma